Wives /Girlfriends Vs Husband's /Boyfriend's phone Privacy

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,625
Habarini wapendwa.

Kwa wale wakazi Dar wa maeneo ya mabondeni salam zenu za pekee najua muda huu mnawaza kama mtatoboa huu usiku wa leo hadi asubuhi bila kitembelewa na mafuriko ya maji ya mvua.

Anyways, twende kwenye topic. Jana nilikuwa na rafiki yangu, tukazungumza mengi sana na mojawapo ambalo lilishika hatamu kwa muda mrefu ilikuwa ni swala la mkewe kupenda kufuatilia simu yake sana na kupekea kuviolate privacy ya mume wake yaani huyu rafiki yangu.

Kimsingi, anasema mkewe anapenda sana kufuatilia simu yake unnecessarily. Yaani amekuwa ni mtu wa kudeal na simu ya mume wake kama vile mtoto anavyodeal na toi lake. Yaani mwanaume akirudi nyumbani anakuwa hana amani na sim yake kiasi kwamba anajikuta anaitumia kwa machale.

Mwanamke ameanzisha kamchezo, anakaa bila kuchaji simu yake halafu mume wake akirejea anajifanya simu yangu imezima chaji niazime simu yako nigoogle kitu.

Au atakuja kumkalia pembeni wakati anatumia simu achungulie mwanaume anafanya nini!

Muda mwingine atashika simu ya mumewe na kuanza kuperuzi picha za kwenye gallery kwa kuzikodolea macho as if anatazama album. Jamaa akiuliza anatafuta nini yeye anamuuliza au hapendi akishika simu yake?

Kuna siku usiku alichukua simu ya mshikaji akajipost, ilikuwa ni siku ya birthday yake. Jamaa anashangaa asubuhi comments za watu kwenye status yake wanamuwish shemeji birthday wishes. Akatazama anakuta picha ya mkewe imepostiwa na yeye hakupost kutazama muda akaona ni usiku ilipostiwa. Ndipo akajua wife amestrike again.

Nikamwambia hata mimi, my lady anapenda complain sana juu ya attention nakuwa simpi kipindi nikiwa nyumbani nae nipo busy na sim.

Yaani anataka muda wote nikiwa nae nisiguse hata sim nimtumbulie macho yeye tu. Tena bora nitazame TV kuliko kutazama simu. Ingawa yeye hanaga tabia ya kupenda shika shika simu yangu kama yule mke wa rafiki yangu.

So, swali kwenu wadau, hivi mnakutana na hii challenge au kuna watu wenu wa karibu wanapitia hii challenge?!
 
Hii challenge niliwahi kushuhudia mwenyewe kuna mdada niliwahi kukutana naye kwenye ujana wangu sikujua kama alikuwa na mme, basi nikamwaga sera zangu yule binti akanielewa na bahati nzuri kumbe yule dada alikuwa wa home kabisa yaani wilaya moja , basi nikawa nachatu naye hadi usiku wa manane ,siku moja nikashangaa napigiwa simu na jamaa ambaye ni dokta kumbe anko wake na yule mdada, yule jamaa aliingia na mikwala ya kunitega kwa kilugha koz alipewa ramani yote na aliyempa mawasiliano yangu, nilimbana hadi akaniambia ukweli kumbe yule dada alikuwa na mumewe na tulikutana siku ile kwenye dala dala akiwa amegombana na mme wake,

Yule jamaa/ anko wa mdada ilibidi anipe ukweli kuwa jamaa alikuwa na wivu sana hasa kwenye simu hadi alim hack, simu zote na sms iwe wasap au za kawaida jamaa alikuwa anaona ! Nilishangaa sana na ikabidi niongee na mwanamke mwenyewe aisee alifunguka, alisema sina amani na ndoa yangu, utumiwe ujumbe unaambiwa ni hawala yangu, unaweza ukawa unachati hata na classmate wako mnafanya yale matani pengine mliwahi tongozana shule mme wake alikuwa anaingilia chatting,,, unashangaa ana stopishwa jamaa anaanza kumfokea, ni mengi aliongea yule dada nikajifunza sana aise, uzuri jamaa naye alikuja kunitafuta akanipa za usoni nikamuelimisha kwanza kufanya hivyo ni kujiongezea stress pia ni kosa kisheria.


Mwisho haya mambo ya mahusiano yanachangamoto sana lakini tuweni na brekiiii si kila chatting ni za michepuko wapo wanaokutana mtandaoni kimatani hasa wanaume tunatabia mno ya kutongoza hovyo kumbe kufanya vile unamletea shida mwenzio. !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ktk maisha yangu sitakuja kushika au kupekua cm ya mwenza wangu, wala yeye kufanya hivyo kweny cm yangu. Cm n privacy ya muhusika. Ts over.
 
Kama tulivyokubaliana, simi ya mwanaume mali yake, ya mke ya familia, ya mchumba yetu except girlfriend. Ila huyu pia unaruhusiwa kupitia.
 
Back
Top Bottom