Wito wa maandamano Dar nje ya Ubalozi wa Marekani kesho

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Baada ya U.K. na maeneo mengine duniani kujiunga kupinga utesaji, mauaji, kutangazwa vibaya na mabeberu kesho ndio kesho namuomba RC wa Dar mh Makonda awe mstari wa mbele maana na yeye alizuiwa kwenda USA kisa tu ni mweusi na tumeona balozi wa USA hapa nchini anavyotusumbua

1. Walikataa WB/IMFkutupa pesa ya MCC kwa umeme wa REA kwa kwa kisingizio cha matokeo ya uchaguzi Zanzibar

2. Walikataa WB wasitupe pesa ya kupambana na corona kwa chuki dhidi ya Rais wetu

3. Waliwazuia baadhi ya watendaji wakuu wa serikali kwenda USA

4. Wamekuwa na matamko mengi ya kusema Tanzania sio salama

5. Wamekuwa na matamko kila siku ya kusema kuwa eti corona ipo sana huku ikiwa imesha ,dhumuni ni kutuchafua th

Ndio muda wa kuonesha hasira dhidi ya mababeru na washirika wake kesho, kila mtanzania huu maana gavana wa Minnesota amesema wazi kuwa sio maandamano ya George pekee bali ni hasira za mateso ya watu weusi duniani na sisi pia tumeathirika na ubabe wa mabeberu

USSR
 
Mabeberu ni lugha iliyotumiwa na makaburu enzi hizo, hebu tumia lugha ya ustaarabu hata kama wanashida
 
Tupo tayari kuandamana kwenda embassy za USA kupinga ufedhuli wa Mabeberu kwa mtu mweusi

Na wale vijakazi wa mabeberu walioko Tanzania wakae sawa
Bora ya huyo beberu mweupe kuliko huyu mweusi aliyetuma polisi kupiga risasi juu kimaajabu halafu zinakata kona zinarudi na kulenga raia asiye na hatia tena mwanafunzi. Halafu hatukuona hiki kiherehere cha kuandamana kwenda Ikulu au Wizara ya Mambo ya ndani. HUU NI UNAFIKI..
 
Back
Top Bottom