Naomba tuweke siasa pembeni tufanye jambo la maana na sadaka kwa Mwenyezi Mungu;
Kama utakuwa umeangalia taarifa ya habari ya ITV leo saa mbili usiku kuna taarifa imeoneshwa ya Binti mdogo ambaye amezaliwa bila mikono yote miwili hivyo kumfanya kutumia miguu yake kufanya kazi za mikono kama vile kuandika
Binti huyo anaonekana anakili sana za darasani na maisha kwani pamoja na kutumia miguu kuandikia amekuwa akishika namba moja darasani toka akiwa chekechea mpaka darasa la saba.
Naomba tumsaidie huyu binti kupata mikono ya bandia ambayo tumejulishwa inapatikana ujerumani ili binti apate mikono ya kumsaidia kutekeleza shuguli muhimu kama kuoga ukizingatia umri wake unakua hivyo anahitaji privacy ya mwili wake
Baba wa Mtoto kupitia ITV anaomba mchango wa hali na mali kufanikisha binti kupata mikono hiyo.
Naomba ITV au mtu yeyote mwenye clip ya taarifa hiyo aiweke hapa watu wajionee wenyewe na kupata mawasaliano ya kutoa michango yao
kwa kuanzia mimi nitamchangia Binti TSH 50,000/= cash kupitia MPESA ya Baba yake iliyotajwa na ITV.
Kama wana JF naomba tumsaidie huyu binti kwa kiasi chochote kile utakachoguswa ili aweze kupata mikono jamani pia wadau na makampuni mbalimbali mnakaribishwa kuchangia
Mwisho pamoja na michango ya wananchi wa kawaida naiomba na Serikali na Viongozi wa Dini kama Kina ASKOFU Gwajima, Lwakatare, Mzee wa Upako, Kardinali Pengo, Mashehe etc katika ibada za kesho na siku ya ijumaa waandae sadaka maaalum ya kumchangia huyu binti ili aweze kwenda ujerumani
ITV na Mod tunaomba ile clip ya huyu binti ikae katika uzi huu kwa ajili ya kutia hamasa ya michango
Siasa na Dini zetu tuweke pembeni kwenye uzi huu