Wito: Tujiondoe CHADEMA

Wito: Tujiondoe CHADEMA

nafikiri nilivyomuelewa muanzisha uzi ni kwamba pale ambapo kuna kuteleza ndani ya chama wahusika waambiwe ili chama kizidi kujengeka. baadhi ya wanaJF wamekuwa wakieleza wazi CDM ifanye nini katika masuala mbalimbali yanayoonekana kuwa ya hovyo ndani ya chama (mfano ishu ya Tuntemeke, Shibuda na masuala mengineyo)

ila hilo la kujitoa, mh sielewi wajitoe kwenda wapi maana mashabiki sio wanachama sasa wanajitoa kuelekea wapi na vilevile chama ni wnachama na mashabiki...

Kujitoa ni lugha ya fumbo...ambayo maana yake ni kugeuka kiakili na kuiangalia CHADEMA kwa macho mawili...pale inapo fanya vizuri,ipongezwe;na pale inapo fanya vibaya isemwe na kukosolewa na mashabiki ili kujenga chama imara na kitakacho leta manufaa kwa taifa hili pale kitakapo kuwa madarakani.
 
copy that....
 
Imekuwa kawaida sasa kwa vijana wengi kushabikia mno CHADEMA.Hii inapelekea hata kusahau pale chama hiki kinapo boronga,wao hufumba macho na kutanguliza ushabiki mbele.
Jambo hili ni baya kwa mustakabali wa taifa letu,kwani pale ambapo CHADEMA itafanikiwa kuchukua dola,itakumbana na wakati mgumu kwani imezoea kujiona sahihi wakati wote.

Mbaya zaidi wengi wa mashabiki ni wale wasio hata na kadi ya chama,nao wanajiita wana CHADEMA.

Jambo la msingi kukumbushana ni kuwa sisi ni watanzania.Nawasihi mashabiki wa CHADEMA ni bora wakajiondoa CHADEMA na kujiona kama watanzania neutral ambao watashabikia maslahi ya taifa,na chama kinacho yatekeleza ndicho kiungwe mkono.
Hii itawawezesha kuikosoa chadema pale inapo kosea,na hivyo CHADEMA itakuwa imara na kupata nguvu zaidi.

TANZANIA:Nakupenda sana.
jiondoe ww,tuachie chama le2
 
Utanisamehe mkuu.Nimejaribu kurudia rudia ulichoandika lakini sijaona mantiki bado.

Kujitoa chadema maana yake nini?kwani lengo letu la kuwa wana chadema limeshatimia?la hasha,ni mpaka litimie kwanza ndio mengine yafuate.

Kwa taarifa yako wengi sana tulikuwa mashabiki wa JK enzi zile 2005 akiingia madarakani sababu ya umahiri wake kwenye kuzungumza na public.It turns out ameshindwa kutuletea yale maendeleo tuliyotarajia na kamwe huwezi kunishawishi tena kumpenda maana yale mapenzi tuliyokuwa nayo kwake yamefutika.

CCM itoke madarakani kwanza. Hadithi nyingine za abunuwasi zitafuata.
 
Tobaaaa sijui nani kamloga huyu kijana, nafikiri anapima upepo km siyo nepi huyu sijui.
 
kukomenti kwenye hii sredi unaweza ondoka na ban!
WITO: tujiepushe na hii sredi.
 
Mkuu ulilosema lina ukweli,lakini siyo kwa pro-chadema pekee hata uvccm kuna mashabiki wasiyoambilika akina Shimwela.Hawaonekani kusimamia maslahi ya taifa kwani hawaikosoi serikali inapofail bali wanaonekana tu pale ambapo upinzani wanakosea.Na hii ni vema tukaitazama kwa jicho la tatu pasi na kunyosheana vidole eti CHADEMA pekee.Sisi vijana wa CHADEMA tukubali kukosolewa lakini tusikubali kukosolewa tunapogundua mazingira ya ukosoaji yametengenezwa!
 
Mkuu tegemea matusi na kashfa nyingi sana kutoka kwa hawa pro-chadema na bado watakutukana hawa si unajua unakuta mmoja anamiliki account kumi kwa wakati mmoja hapa JF ndivyo sera za mtaa wa UFIPA zinavyosema MATUSI mbele

Hivi hata Lusinde anatokea UFIPA STREET?
 
Mwaka 1979 profesa Mazrui alisema kuwa watanzania wameathiriwa na ugonjwa aliouita 'tanzalphilia' Ugonjwa huu ni wakuona kila kitu chetu ni kizuri kuliko chochote [siasa, utamaduni,sera za uchumi n.k] aidha afrika au dunia nzima.
tulimmbeza sana lakini sasa hata mimi ninaamini alichokisema ni kweli kabisa kwani tabia hii imetufanya tushindwe hata kuchambua mambo. Mwanachama wa ccm atammbeza wa upinzani hata kama alichosema ni hoja nzuri na Chadema na vyama vingine ni hivyo hivyo. kama hatutobadilika [hasa vizazi vipya] basi tumeangamia maana wenzetu wanakimbia sisi bado tunapiga soga tu.
Nilikuwa kigali last month ile nchi inavyokwenda is unbelievable na kwa sasa hasa wale waliokwenda kile kipindi cha matatizo hawawezi kuamini kama kama hiyo ni rwanda. Miaka 5 ijayo itakuwa mbali na kutupita vibaya sana be it kwenye elimu, afya, nguvu kazi, uchumi, kilimo etc you name it bado watakuwa ahead.
Na sisi kazi yetu ni kupingana tuu.

Point...speak out loudly.
 
Ondoka wewe, hatuondoki mpaka tuone muujiza Mungu ameshatuahidi ukombozi sasa ni sisi tu kuwa wavumilivu. Tukishindwa hapa basi life has gone Tanzania will never change. We are at the peak of changes. Kilichobaki ni kuona nchi ya ahadi yenye maziwa na asali na kufunguliwa na kuwa huru kutoka kwenye minyororo ya ccm.

Hiyo miujiza si rahisi kutokea kwa hali ilivyo sasa!
Ni lazima wadau wa CHADEMA kubadilika kimtazamo na kuiangalia CHADEMA kama taasisi inayo ongozwa na binadamu wenye uwezekano wa kufanya makosa,hivyo kuwakosoa.
Mtazamo wa sasa kuwa mkosoaji wa chadema ni "gamba" hautawapatia watanzania ukombozi takikana.
 
imekula kwenu ccm! Peooooples!! Poweer ndo hivyo inachukua nchi mlizoea kutuibia sasa tunawakataa!
 
Imekuwa kawaida sasa kwa vijana wengi kushabikia mno CHADEMA.Hii inapelekea hata kusahau pale chama hiki kinapo boronga,wao hufumba macho na kutanguliza ushabiki mbele.
Jambo hili ni baya kwa mustakabali wa taifa letu,kwani pale ambapo CHADEMA itafanikiwa kuchukua dola,itakumbana na wakati mgumu kwani imezoea kujiona sahihi wakati wote.

Mbaya zaidi wengi wa mashabiki ni wale wasio hata na kadi ya chama,nao wanajiita wana CHADEMA.

Jambo la msingi kukumbushana ni kuwa sisi ni watanzania.Nawasihi mashabiki wa CHADEMA ni bora wakajiondoa CHADEMA na kujiona kama watanzania neutral ambao watashabikia maslahi ya taifa,na chama kinacho yatekeleza ndicho kiungwe mkono.
Hii itawawezesha kuikosoa chadema pale inapo kosea,na hivyo CHADEMA itakuwa imara na kupata nguvu zaidi.

TANZANIA:Nakupenda sana.

Acha mawazo mgando, hicho chama ulicho wewe, kiweke wazi tukifahamu. Na hapo kwenye red chunga sana, hatubahatishi this time.
 
ninakubaliana na comment ya jamaa mmoja that "inabidi kuwe na malipo kwa kila anayetaka kuweka post hapa JF"..hivi huyu jamaa anasahau kuwa hata wakati wa kudai uhuru hali ilikuwa hivihivi?
 
Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa.saa ya ukombozi imefika.tusimlaumu sana upeo wake umekoma hapo.m4c ,mwendo mdundo.
 
Una akili sana wewe. Huu ushabiki is too much, sasa naona umeshika kasi. hakuna aliye mtakatifu hapa duniani sasa iweje hawa wanaojiita wanachadema wasione mapungufu ya chadema? au ndio kusema hayapo? acheni ushabiki bwana wekeni maslahi ya taifa mbele.

Nahisi Mmesahau KANGA na KOFIA ZA CCM nyie
 
Back
Top Bottom