Ndugu wana chit chat wote, Nikiwa mwenyekiti wa tume ya kuratibu mahusiano na ndoa hapa chit chat napenda kutoa wito kwa wahusika kama ifuatavyo.
i.Hapo kesho jumatano ya 28/11/012 nahitaji kupata ripoti ya SCREENING ya uhusiano kati ya
Madame B na
Chimbuvu ili niweze kupitia kwa ajili ya hatua zaidi. Natumai kamati ya
Mamndenyi The Boss na
Ruhazwe JR mpo na mmeshaiandaa
ii.Kamati ya sheria ya
Judgement Ruttashobolwa na
Kipipi pia nahitaji taarifa ya uhalali wa kisheria wa uhusiano wa
Chimbuvu na
Madame B .
iii.Kamati ya maadili chini ya
BADILI TABIA naomba muandae tathmini ya nidhamu ya wahusika kwa kuzingatia mwenendo wa uhusiano wao na mwitikio wao pale walipokumbushwa mara kadhaa kuhusu hatua za kufuata ili kuhalalisha uhusiano wao.
iv.Wataalamu wa kitengo cha moving na still pictures babu
Asprin na mzee
Mtambuzi kaeni standby kwa ajili ya alhamisi nitakapokuwa nimetoa uamuzi juu ya wahusika
v.kamati ya masuto
Zinduna cacico snowhite gfsonwin lara 1 ,FP pamoja na dereva wenu
Nicas Mtei kaeni mkao wa kazi kwa ajili ya alhamisi.
vi.
Bishanga nitonye Mungi ,
Arushaone ,
C6 ,
Filipo na
tedo mnaombwa kuwa tayari kufadhili zoezi la siku ya alhamisi.
Pia napenda kuzikumbusha kamati za SCREENING kushughulikia haraka suala la
Arushaone na
Mamzalendo ,SHERIA kushughulikia haraka suala la
Bishanga na
The secretary .
Mwisho ninawaomba wana chit chat wote kutoa ushirikiano kwa tume kwa maamuzi yatakayofikiwa kwani yote ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kila mmoja anafurahia maisha ya hapa chit chat.
Wakatabahu!
Baba V MWENYEKITI WA TUME YA KURATIBU MAHUSIANO NA NDOA CHIT CHAT 2012