Wito kwa Lissu; Jitokeze kwenye vyombo vya habari uwaombe msamaha wafanya kazi kwa kuwaita takataka

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
9,175
2,000
Jpm kapotosha vibaya sana, eti anawapenda wafanyakazi duh.kuna wafanyakazi tangu waajiliwe wana miaka zaidi ya 7 hawajawahi pandishwa madaraja wala kupata nyongeza za mishahara.Mfanyakazi atakayemchagua Jpm hajipenduhata mwenyewe
 

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
9,175
2,000
Hiyo ni weakness kubwa Sana aliyo ifanya Tundu lissu hivyo CCM wameamua kuitumia hiyo weakness kujijengea Imani kwa wafanyakazi na kuwapandikiza chuki dhidi ya Lissu.

Tena Mgombea urais Kupitia CCM amekazia kauli hiyo kwa kuwasemea walimu, manes, madaktari na vyombo vya Dora kuwa wao ndo wanaitwa na lissu takataka kutoka majalalani.

Ogopa Sana watu wanaitwa wanasiasa.
Labda wafanyakazi wasiojitambua
 

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,233
2,000
Wakuu hapa mnaongelea wafanyakazi wa ngazi ipi? Je, mnaongelea wafanyakazi wa serikalini tu? Je, ratio ya wafanyakazi wa Serikalini pamoja na Mashirika ya umma ni asilimia ngapi? Kwa maoni yangu sioni kiongozi yoyote makini kupandisha mishahara bila kuangalia uchumi wa nchi unafanyaje.
 

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,014
2,000
Rais alisema anataka kumpa kakazi kadogo, yeye akajibu kakazi kadogo anapewa aliyetoka jalalani. Akimaanisha yule Bwana aliyesema JPM kamtoa Jalalani.

Yeye anasema jamaa katukana Walimu, wanajeshi na Polisi ina mana hawa ndo wana vikazi vidogo?
 

Kaisari

JF-Expert Member
Nov 13, 2012
3,644
2,000
Wakuu hapa mnaongelea wafanyakazi wa ngazi ipi? Je, mnaongelea wafanyakazi wa serikalini tu? Je, ratio ya wafanyakazi wa Serikalini pamoja na Mashirika ya umma ni asilimia ngapi? Kwa maoni yangu sioni kiongozi yoyote makini kupandisha mishahara bila kuangalia uchumi wa nchi unafanyaje.
Umeambiwa tunajenga reli hatuongezi mshahara, tunajenga bwawa la kuzalisha umeme hatuongezi mshahara.
Hivyo tatizo siyo uchumi ni kipaumbele
 

Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,438
2,000
Mtoa mada unazidi kuiharibia CCM! Ukienda you tube hakuna clip zinazoangaliwa zaidi kwa sasa kama za Lissu. Fuatilia sikiliza ndipo ulete ushawishi.
Kimsingi Lissu atachukua kura za watumishi wanyonge wote ambao ni kweli kwa miaka 5 hawajapewa increment na kutopanda madaraja Tofauti na taratibu za UTUMISHI zilivyo.
Hizo hoja za Ndege ,madaraja, Majengo ni sawa lakini watumishi haziwahusu direct. Wao wanajua kila julai kuna increment ya mshahara hata kama ni 3,000 na baada ya miaka 3 wanapanda daraja na hivyo mshahara kuongezeka. Pale inapotokea umepanda daraja na huku salary imeongezwa ndio furaha huwa kubwa sana.
 

tathmini

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
316
250
Acha kupotosha jamii uliona kawataja kina kabudi katika Matamushi yake au alitaja wafanya kazi kwa ujumla.

Hivi nikweli mpaka umefika hapa hujui kutofautisha wingi na umoja.

Kwapamoja tumushauri lissu apunguze kujishushia hadhi katika jamii.
Katika lugha zote ni kawaida kukejeli mtu kwa kutumia wingi badala ya umoja. Linguistics 101
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,780
2,000
Maendeleo hayana YANA VYAMA...

Kwa Bwana Bwege kule aliyoyasema yote yanaonyesha maendeleo yana CHAMA

Maendeleo yana chama....

Huko Musoma kasema hakule maendeleo kwa sababu walichagua wapinzani....
 

mhuri25

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
1,876
2,000
Humu ndani Watu wachache na wengine wengi huko Tweeter Kila siku nawaeleza kuwa licha ya JPM kuwa na mapungufu mengi tu Ila n Mara 1000 Bora kuliko kumchagua TL sio Presidential Material kabisa huu Ni Ukweli mchungu Ila watakuja tu kupinga TL dharau zinemjaa Sana zaidi huwa anajiona anafikiri vizuri sana kuliko Watu 60M nchi nzima!!!

Mtu anafika Hadi anadharau Walimu wake Huyu sio wa kumpa NCHI kabisa labda dunia iumbwe Mara ya pili Tena!!!
 

Kibororoni

Member
Dec 19, 2019
66
150
Maelezo meeeengi unakuja unakurupuka tu. Kwani mzee aliyeokotwa mavumbini huko kanda ya kati humjui wewe?. Basi ndo huyo aliyesemwa. Danganya wasiofuatilia kampeni hizi tangu kipusa kimegongwa. Tunafuatilia neno kwa neno, herufi kwa herufi, mkato na kituo kila msitari. Tutachagua kwa umakini wa hali ya juu term hii.
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
8,299
2,000
Wewe mkuu siyo mfanya kazi wa serikali kwahiyo kaa kimya maana siyo wewe uliye itwa takataka kutoka jalalani.
Huyo kichaa hajui siasa na ni mtu mshenzi tu. Kuna manyumbu yamekua yanamsifia kama ana akili wakati ni wakili mweledi wa kuuzia wenye hela haki. Siasa hajui wala sio mtu mwadilifu ndio maana amejiuza kutetea mabeberu.
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,559
2,000
Pimbi kweli wewe aache kuomba msamaha aliyeshindwa kuwaongeza mishahara na kuwapandisha madaraja wafanyakazi , ambazo ni haki zao kisheria utafikiri anatoa hela za mfukoni mwake au za familia yake , aje aombe msamaha Lissu? Inaingia akilini ?
 

Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,227
2,000
Tundu Lissu nakuomba Sana Kama unataka upate angalau asilimia 20% za Kura za Watanzania nakuomba Sana jitokeze mbele ya media uombe msamaha kwa wafanyakazi wote wa kuteuliwa na wakuajiriwa na serikali iliyo chini ya rais Magufuli Baada ya kuwaita takataka na majalala.

Tundu Lissu nilikushauri kukaa kimya badala ya Rais Magufuli kukutega na mtego mdogo kabisa wa kusema; "Mwambieni kijana wenu aachane na urais nitampa kazi ndogondogo anayoiweza" Magufuli.
Kwavile nakufahamu vizuri kuhusu matamshi yanayotoka kinywani mwako nilikuja haraka Sana nikakupa ushauri kuwa usijibu chochote juu alichosema Magufuli Bali mpuuze tu ujifanye Kama hujasikia Ila hukisikia ushauri Wangu.

Hatimaye ukaamua kwenda kujibu mbele ya watu kuwa; "mwambieni Rais Magufuli Akawape kazi hao matakataka anao waokota majalalani na siyo Mimi"
Itoshe tu kusema Baada ya kauli yako kundi kubwa la wafanyakazi lililokuwa linakuona wewe Kama mkombozi wao na mpigania haki zao wamepoteza kabisa Imani kwako na wanakuona Kama mnafiki na Sasa hivi hasira zao zimehamia kwako kwa kuwaita wao takataka wanao okotwa majalala.

Mwisho; CCM iliamua ikutege na ukategeka ona Sasa hivi wanaitumia kauli yako kwenye majukwaa kuwanyeshwa Sumu ya kuzidi kukuchukia wafanyakazi ulio waita majalala.

Tundu lissu nakushauri tena usipende kujibu Kila unacho chokonolewa na wapinzani wako, wenzio siasa wanaijua na mbinu wanazo. Wewe siasa huijui Bali Ni mwana harakati mzuri na kwa Nafasi yako hiyo inayogombea uanaharakati siyo mahali pake na wapinzani wako wanaitumia hiyo weakness yako ya uanaharakati kukuchokonoa kwa vijembe vidogo vidogo wakijua wazi kabisa utajibu kiuanaharakati na matusi juu.
Ahsante nawasilisha!
Sidhani ka wafanyakazi watakua na akili ka zako na huyu magufuli wako, Ikiwa ni hivyo nitamuunga mkono Lisu kufumua mfumo wa elimu, maana itakua haijawasaidia. Huyo Magufuli alimpa kazi Kabudi ya kuteuliwa na wakati alikua mwalimu wa chuo cha ajabu anasema anamshukuru Magufuli kumpa kazi maana amemtoa jalalani. Na hakuna sehemu Magufuli alishakanusha kua hapana sikukutoa jalalani ili niliangalia uwezo wako.
Sasa kama hata aliyekua amempa kazi amekubali kua alimtoa jalalani inakuaje kosa kwa Lisu kusema hawape kazi hao hao anaowatoa jalalani?
 

Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,227
2,000
Hiyo ni weakness kubwa Sana aliyo ifanya Tundu lissu hivyo CCM wameamua kuitumia hiyo weakness kujijengea Imani kwa wafanyakazi na kuwapandikiza chuki dhidi ya Lissu.

Tena Mgombea urais Kupitia CCM amekazia kauli hiyo kwa kuwasemea walimu, manes, madaktari na vyombo vya Dora kuwa wao ndo wanaitwa na lissu takataka kutoka majalalani.

Ogopa Sana watu wanaitwa wanasiasa.
Jitahidi kuficha ujinga wako basi, au nenda kijijini kwenu ndo kawadanganye huo ujinga wako
 

Poa 2

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
865
1,000
Wewe mkuu siyo mfanya kazi wa serikali kwahiyo kaa kimya maana siyo wewe uliye itwa takataka kutoka jalalani.
Mimi ni mfanyakazi ila sijaitwa wa jalalani na lisu na sijapewa kazi na magufuli lambda Mh. KABUDI ndio wa jalalani😁😁😁😂
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom