Wito kwa DPP: Japo ni Ushauri wa Rais kuwasamehe, Tafadhali tumia Nolle kufuta kesi zao, Makubaliano yawe siri ili wapokelewe na Jamii kama Watu Wema

nolle prosequi
 
Asante Paschal umemaliza yote.
 
walengwa wakuu hawatoomba huo msamaha.
Sidhani walengwa ni wawili hao wengine wote ni funika kombe mwanaharamu apite wa kwanza yule kibosile wa mabasi yaendayo kasi maana watu wa msonga walienda kuombea msamaha wa pili Baba mkwee wa Mzee wetu mamvi maana sharti la kurudi nyumbani ameshatimiza ila km kweli nia ni msamaha naomba asamehe wote ili tuanze upya km taifa...
 
Uzuri wakilipwa wanalipwa Kodi yako na sio mshahara wa JPM, lengo kuu la mfanyabiashara Ni kupata pesa Kama anaona atapata pesa kupitia fidia aendelee kukaa jela
 
toka lini mtuhumiwa akasamehewa?
 
Wewe ndiyo utumii akili muhjmiwa hakikili huyo siyo mtuhumiwa tena hao wanatakiwa wakili makosa ili kujivua hutuhumiwa
Kwenda zako. Kajifunze Kiswahili kwanza ndipo uje hapa kubishana na wenye akili zao. Basi na walioua wakiri wasamehewe.
 
Huu sio msamaha, niliambiwa anayekusamehe hakupi masharti. Hizi ni siasa, kutafuta huruma kwa jamii unayoinyanyasa. Butiku kasema watajwe wahusija na wanao au walioshirikuana nao.
Hii ni kumlazimisha mtu kukiri uongo, na uzushi.

Mahakamani mmekosa ushahidi kuwatia hatihani, kila siku kesi hazisomwi kwa kukosa ushahidi, na uchunguzi usio isha, lakini leo wana furahia wao kukiri makosa waliyopewa, waliowabambikia watuhumiwa na yaliyokosa ushahidi usiotia shaka.

Sifurahii hili hata kidogo.

Magufuli atalaaniwa leo na hata milele.
 
Mkuu @P, DPP afute kesi zao kwa sababu wameshalipa hela walizohujumu au afute kwa sababu HAWANA KESI YA KUJIBU?.
 
Anko P japokuwa wewe umetoa wazo zuri.ila hapa sikuuingi mkono kabisa.Nolle prosequi as per section 91(1) ya Cpa ni kumuachia kabisa mtuhumiwa na na anakuwa huru.Sasa hii plea bargaining ni mtuhumiwa anakiri kosa kwa hiari.Akisha kiri kosa Dpp anadili nae kwa mujibu wa sheria.Sasa wewe unataka nolle prosequi Dpp aitumie kwa watu waliopiga madili! .Hizo bilioni mia tatu alizopiga Harbinder Sethi angezitema kama akipewa nolle prosequi? We kula bata huko capetown .Alafu usisahau kupita maeneo ya woodstock kunawabongo wengi sana wamechoka waachie hata pesa ya kula.
 
Mkuu uko sehemu gani? Mimi nipo Durban tutafutane.
 
Pascal Mayalla , Mkuu, nawe umeamua kujifunga mabomu kabisa na hili dude la uhujumu, utakatishaji na ukwepa kodi?
Tatizo watu wengi hawaangalii kwa "Eagle eye" hili dude bali wanaagalia tu serikali iokoe hela au watu warudi uraiani. Tazameni hilo jambo kwa ufahamu.

Yalabi, hili dude litakula vichwa vya watu hasa wasomi uchwara.
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 

Hili jambo, tumelipigia Sana kelele, tumepandisha ma thread na mathreads, makala na makala hatimaye Leo kimefanyika kitu.

wa kilichofanyika leo, Ile Nolle ya Mbowe, hongera Sana DPP, utabarikiwa, aliyekutuma atabarikiwa, Tanzania tutabarikiwa. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana na haki ikaonekana imetendeka.

Mungu ibariki Tanzania,
Pasco
 
Hapa nilizungumzia justice for sale in Tanzania!.
Watu wanasubirì hadi madudu yafukunyuliwe ndipo waseme!, sisi tulioyaona yakifanyika, tulipigia kelele na haikusaidia kitu!, sijui kama hiyo barua itasaidia kitu maana post aliyopo sasa has a security of tenure, anaweza kuteuliwa tuu, hawezi kutenguliwa!, na post iliyotangulia ya DPP ina kinga ya kutohojiwa na yeyote au kushitakiwa!.
Huku ni kutwanga tuu maji kwenye kinu!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…