Rais Samia: Sichukulii wapinzani kama maadui. Waliomba kurudi pamoja na kufuta kesi zao, nimefanya hivyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Usa River Mkoani Arusha leo tarehe 05 Machi, 2023 akiwa njiani kurejea jijini Dodoma baada ya kufunga kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu siku ya tarehe 04 Machi, 2023

E9E0181C-6A91-4783-BEAA-B356CDF700CE.jpeg

Samia Suhulu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia amesema kuwa Serikali imesitisha ukataji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kubana bajeti. Badala yake fedha zinazopatikana zinaelekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo ili kuwahudumia wananchi.

Akizungumzia siasa za nchi, Rais Samia amesema Siasa zetu zipo imara sana, tendo la juzi la kurudi kwa mtu wao wa kanda (Godbless Lema) na hakuna kilichotokea hii inaonesha kisiasa tupo imara.

“Mdogo wangu amerudi, kaniambia mama nataka kurudi nikamwambia rudi, akasema mama nina kesi nikamwambia nazifuta, rudi. Amerudi tuimarishe siasa si ndio? Mwanamme ni yule anayejiamini, mwanamke ni yule anayejiamini. Kwahiyo kwenye uwanja wa siasa tunajiamini, tupo vizuri” amesema

Pia, Rais amesisitiza kuwa Mtanzania yeyote, awe chama chochote kinachotofautisha ni mawazo na fikra pekee, pia yeye hachukulii wapinzani kama maadui bali kama watu watakaosaidia kumuonesha changamoto zilipo azitekeleze ili CCM iimarike.

Amewashukuru pia bodaboda waliomsindikiza kuanzia mjini, amesema anawatambua na waendelee na mwendo huohuo hadi 2025.

Awali, Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe amesema kuwa Serikali imekamata viongozi fulani huko Babati wakishirikiana na watumishi wa NRFA wakihujumu mahindi wanayowauzia wananchi ambapo wamekuwa wanayachukua na kuwapa wafanyabiashara. Amesisitiza kuwa mfanyabiashara yoyote atakayekamatwa na mahindi ya NRFA atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola kisha Serikali itataifisha mahindi hayo.

2C6190BE-8328-4724-B7BD-8200D16D93DB.jpeg

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo
Aidha, Waziri Bashe amempa Rais taarifa ya Kukamatwa kwa mtu mmoja Njombe ambaye ndani ya ghala lake ameweka mbolea ambayo imechanganywa na mchanga.

“Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kamati yake ya Ulinzi nimeongea nao sasa hivi. Nimewaambia wamkatamate yule mwenye kiwanda, wamkamate mwakilishi wake, wafunge lile ghala, wawapeleke kwenye vyombo vya dola. Huu ni uhujumu uchumi kama uhujumu uchumi mwingine yoyote”

Amesisitiza kuwa Serikali itasitisha ruzuku kwa mtuhumiwa huyu pamoja na kutembelea wakulima wote walionunua mbolea hiyo ili kujiridhisha ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.
 
Akiwa Usa-River, Jijini Arusha, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Watanzania wa Vyama vyovyote wanatofautiana tuu fikra, hivyo anawachukulia Wapinzani kama watu wanaomuonesha changamoto zilizopo, azishughulikie

Amesema, "Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, akasema Mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi"
 
Mama kama mama
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Usa River Mkoani Arusha leo tarehe 05 Machi, 2023 akiwa njiani kurejea jijini Dodoma baada ya kufunga kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu siku ya tarehe 04 Machi, 2023

Rais Samia amesema kuwa Serikali imesitisha ukataji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kubana bajeti. Badala yake fedha zinazopatikana zinaelekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo ili kuwahudumia wananchi.

Akizungumzia siasa za nchi, Rais Samia amesema Siasa zetu zipo imara sana, tendo la juzi la kurudi kwa mtu wao wa kanda (Godbless Lema) na hakuna kilichotokea hii inaonesha kisiasa tupo imara.

“Mdogo wangu amerudi, kaniambia mama nataka kurudi nikamwambia rudi, akasema mama nina kesi nikamwambia nazifuta, rudi. Amerudi tuimarishe siasa si ndio? Mwanamme ni yule anayejiamini, mwanamke ni yule anayejiamini. Kwahiyo kwenye uwanja wa siasa tunajiamini, tupo vizuri” amesema

Pia, Rais amesisitiza kuwa Mtanzania yeyote, awe chama chochote kinachotofautisha ni mawazo na fikra pekee, pia yeye hachukulii wapinzani kama maadui bali kama watu watakaosaidia kumuonesha changamoto zilipo azitekeleze ili CCM iimarike.

Amewashukuru pia bodaboda waliomsindikiza kuanzia mjini, amesema anawatambua na waendelee na mwendo huohuo hadi 2025.

Awali, Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe amesema kuwa Serikali imekamata viongozi fulani huko Babati wakishirikiana na watumishi wa NRFA wakihujumu mahindi wanayowauzia wananchi ambapo wamekuwa wanayachukua na kuwapa wafanyabiashara. Amesisitiza kuwa mfanyabiashara yoyote atakayekamatwa na mahindi ya NRFA atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola kisha Serikali itataifisha mahindi hayo.

View attachment 2537925
Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo
Aidha, Waziri Bashe amempa Rais taarifa ya Kukamatwa kwa mtu mmoja Njombe ambaye ndani ya ghala lake ameweka mbolea ambayo imechanganywa na mchanga.

“Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kamati yake ya Ulinzi nimeongea nao sasa hivi. Nimewaambia wamkatamate yule mwenye kiwanda, wamkamate mwakilishi wake, wafunge lile ghala, wawapeleke kwenye vyombo vya dola. Huu ni uhujumu uchumi kama uhujumu uchumi mwingine yoyote”

Amesisitiza kuwa Serikali itasitisha ruzuku kwa mtuhumiwa huyu pamoja na kutembelea wakulima wote walionunua mbolea hiyo ili kujiridhisha ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.

Hakuna jiwe litalosalia! Kila jambo litakua wazi kwa namna yake, na wananchi wataelewa nn kiliendelea!!!
 
Na hii ni hbr mbaya san na ni pigo kubwa kwa walinda legacy!!
 
Back
Top Bottom