Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Pongezi kwa DPP Mpya, Ikikupendeza, Anza na Nolle Kusafisha Uchafu Ulioukuta.jpg

Wanabodi, kama kawaida yangu, kila nipatapo nafasi, huwa nawaletea zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huandikwa kwa swali, na kukuachia wewe msomaji uhuru wa kuchangia na kutoa jibu lolote. Makala hizi zitakuwa zinatoka kwenye Gazeti la Nipashe, kila siku za Jumapili.

Makala ya Jumapili ya leo, ni ya pongezi kwa DPP wetu mpya, kwa vile DPP huyu ameipokea ofisi ya DPP, ikiwa imechafuka kwa kesi za kubambikia na mlolongo wa kesi zinazo suasua, wanabodi mnaonaje, jee tumshauri DPP wetu, kama ataona itampendeza, anze kazi akiwa mahali pasafi, hivyo kwa kutumia mamlaka yake ya Nolle, kazi yake ya kwanza iwe ni usafi, kusafisha malundo ya uchafu wote wa mtangulizi wake aliokuta mezani kwake, ili apate fursa ya kuanza upya kwa usafi, au, kwa vile kwa mujibu wa sheria iliyounda ofisi ya DPP, DPP, anatakiwa kufanya kazi yake independently bila kuulizwa, kuingiliwa au kushinikizwa na yeyote, na kwa faida ya wengi, ni DPP na Rais wa JMT, ndio watu wawili pekee, wenye mamlaka ya kufanya chochote bila kuulizwa au kutakiwa kutoa sababu kwa yoyote.

Mamlaka ya Rais kufanya chochote bila kuuliziwa au kutoa sababu, ni mamlaka ya rais katika uteuzi za zile nafasi za uteuzi at presidents pleasure, rais hatakiwa kutoa sababu kwa yoyote kwa nini anamteua fulani, na vivyo hivyo kwa hizo nafasi za uteuzi at presidents pleasures, rais akiamua kutumbua, pia anaweza kutumbua, kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote na hatakiwi kuhojiwa na yeyote, hivyo wale wote wanaohoji kwa nini rais amemteua fulani kuwa Balozi, RC, DC, RAS, DED or DAS, na wenyeviti wa Bodi, ni nafasi za uteuzi at presidents pleasures, ana uhuru wa kumteua yoyote kwa sababu yoyote, au bila sababu yoyote na harusuhusiwi kuhojiwa na yeyote.

Zamani enzi za Mwalimu, pia kulikuwa na sheria iliyoitwa Presidential Preventive Detention Order, ambayo rais wa JMT, alikuwa ana mamlaka ya kumsweka lupango mtu yoyote ndani ya JMT, kwa kipindi chochote, bila kumfikisha kwenye mahakama yoyote, wala kumjulisha sababu zozote!. Sasa unapokutana na rais Mzee wa totoz, mkagombea naniliu, ukamshinda rais, ndugu yangu unaweza kuishia pabaya kama yule DAS wa naniliu!, Thanks God, kupitia japo la wanasheria nguli wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, wa enzi hizo, wakiongozwa na Prof. Issa Gulamhusein Shivji, Prof. Gamalieli Mgongo Fimbo na Prof. Chris Peter Maina, waliichallenge hii sheria, na mahakama kuu, ikairekebisha na kumlazimisha rais akimtia mtu ndani kwa kutumia mamlaka hayo, lazima atoe sababu na ziwe za mashiko, na sio mnagombana na mtu kwenye ulevi, kugombea bibi, kisha mtu unaozea lupango.

Mamlaka hayo ya mtu kutoulizwa kitu, bado yako kwa DPP, katika uendeshaji wa kesi zote za jinai, ni DPP ndio huanzisha mashitaka. DPP ana mamlaka ya kuingilia kesi yoyote ikiwa hatua yoyote kabla ya hukumu, kuibadili, kuifuta, kupunguza washitakiwa na hata kuifuta kesi kwa Nolle, na DPP hapaswi kutoa sababu yoyote wala kuulizwa na yoyote hata rais wa JMT hana mamlaka ya kuulizwa chochote kwa DPP!. Mtu mwingine mwenye mamlaka ambayo rais hana uwezo wa kuuliza ni CAG kwenye kuwasilisha ripoti ya CAG Bungeni, Ripoti hiyo inawasilishwa Bungeni na rais, ikitokea rais asipoiwasilisha, then CAG amepewa mamlaka ya kuachana na rais, na kuiwasilisha mwenyewe ripoti hiyo, hilo likitokea, Bunge baada ya kuipokea, linamshughulikia rais kwa mujibu wa kufungu 46. Na Bunge likigoma kupokea ripoti ya CAG, linavunjiliwa mbali!.

Sote tumemsikia rais Samia alichosema kuhusu kuhusu ofisi ya DPP na kilio cha haki. Rais Samia ameonyesha nia ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki kwa kauli na matendo, ikiwemo kumuondoa DPP aliyekuwepo na kumteua DPP mpya ili tuanze upya. Jee DPP mpya ataweza kuanza upya kutenda haki, huku amezongwa na lundo la uchafu wa uvundo mkali uliotokana na machozi, jasho na damu, au aanze kwanza na usafi wa kusafisha uozo aliokuta?, au kwa vile DPP hatakiwi kuingiliwa hivyo tumuache tuu?. N mwisho jee kumshauri DPP kama nifanyavyo kwenye makala hiyo, ni kumuingilia?

Wasalaam
Jumapili Njema.
Rejea za Mwandishi Kuhusu DPP.
1. https://www.jamiiforums.com/threads/kagoda-kamwe-haitafikishwa-mahakamani.169015/
2. Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.
3. Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o!
4. Wito kwa DPP: Japo ni Ushauri wa Rais kuwasamehe, Tafadhali tumia Nolle kufuta kesi zao, Makubaliano yawe siri ili wapokelewe na Jamii kama Watu Wema
5. ‪DPP atumie madaraka yake kisheria ipasavyo, asisubiri maelekezo ya wanasiasa ili afanye kazi‬
6. Utabiri wa Good News kwa CHADEMA: DPP Ataifuta Kwa Nolle, Ile Kesi ya Ugaidi ya Lwakatare!
7. DPP wa Tanzania: Ni Kihiyo wa Sheria, Msanii au Mbabaishaji?
8. Baada ya kukamilika siku 14 za msamaha kwa wahujumu, Je Rais Magufuli atumie busara za Harun El Rashid kuwasamehe ambao hawakuandika barua? Au...!.
Paskali.
Update
Hatimaye usaidizi huu, unakwenda kufanyika, kupitia kipindi cha TV kwenye kituo cha Channel Ten, kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku na marudio kila Jumatano saa 9:30 Alasiri.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZn
Usikose kuangalia!.
P
 
Msimseme vibaya Pascal, aliponea chupu chupu utawala uliopita, alitingisha mihimili miwili, serikali na bunge! Kwa vyovyote vile alitishwa akaufyata.

Ilikuwa lazima kujifanya mjinga uishi au uendelelee kuwa kiherehere ukufe! HATA ingekuwa mimi Pascal ningejifanya tu mnafiki niishi ingawa roho inauma hivyo hivyo,
 
kwahiyo anaandika kwa kutumia tumbo?
 
View attachment 1802098
Wanabodi, kama kawaida yangu, kila nipatapo nafasi, huwa nawaletea zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huandikwa kwa swali, na kukuachia wewe msomaji uhuru wa kuchangia na kutoa jibu lolote. Makala hizi zitakuwa zinatoka kwenye Gazeti la Nipashe, kila siku za Jumapili.

Makala ya Jumapili ya leo, ni ya pongezi kwa DPP wetu mpya, kwa vile DPP huyu ameipokea ofisi ya DPP, ikiwa imechafuka kwa kesi za kubambikia na mlolongo wa kesi zinazo suasua, wanabodi mnaonaje, jee tumshauri DPP wetu, kama ataona itampendeza, anze kazi akiwa mahali pasafi, hivyo kwa kutumia mamlaka yake ya Nolle, kazi yake ya kwanza iwe ni usafi, kusafisha malundo ya uchafu wote wa mtangulizi wake aliokuta mezani kwake, ili apate fursa ya kuanza upya kwa usafi, au, kwa vile kwa mujibu wa sheria iliyounda ofisi ya DPP, DPP, anatakiwa kufanya kazi yake independently bila kuulizwa, kuingiliwa au kushinikizwa na yeyote, na kwa faida ya wengi, ni DPP na Rais wa JMT, ndio watu wawili pekee, wenye mamlaka ya kufanya chochote bila kuulizwa au kutakiwa kutoa sababu kwa yoyote.

Mamlaka ya Rais kufanya chochote bila kuuliziwa au kutoa sababu, ni mamlaka ya rais katika uteuzi za zile nafasi za uteuzi at presidents pleasure, rais hatakiwa kutoa sababu kwa yoyote kwa nini anamteua fulani, na vivyo hivyo kwa hizo nafasi za uteuzi at presidents pleasures, rais akiamua kutumbua, pia anaweza kutumbua, kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote na hatakiwi kuhojiwa na yeyote, hivyo wale wote wanaohoji kwa nini rais amemteua fulani kuwa Balozi, RC, DC, RAS, DED or DAS, na wenyeviti wa Bodi, ni nafasi za uteuzi at presidents pleasures, ana uhuru wa kumteua yoyote kwa sababu yoyote, au bila sababu yoyote na harusuhusiwi kuhojiwa na yeyote.

Zamani enzi za Mwalimu, pia kulikuwa na sheria iliyoitwa Presidential Preventive Detention Order, ambayo rais wa JMT, alikuwa ana mamlaka ya kumsweka lupango mtu yoyote ndani ya JMT, kwa kipindi chochote, bila kumfikisha kwenye mahakama yoyote, wala kumjulisha sababu zozote!. Sasa unapokutana na rais Mzee wa totoz, mkagombea naniliu, ukamshinda rais, ndugu yangu unaweza kuishia pabaya kama yule DAS wa naniliu!, Thanks God, kupitia japo la wanasheria nguli wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, wa enzi hizo, wakiongozwa na Prof. Issa Gulamhusein Shivji, Prof. Gamalieli Mgongo Fimbo na Prof. Chris Peter Maina, waliichallenge hii sheria, na mahakama kuu, ikairekebisha na kumlazimisha rais akimtia mtu ndani kwa kutumia mamlaka hayo, lazima atoe sababu na ziwe za mashiko, na sio mnagombana na mtu kwenye ulevi, kugombea bibi, kisha mtu unaozea lupango.

Mamlaka hayo ya mtu kutoulizwa kitu, bado yako kwa DPP, katika uendeshaji wa kesi zote za jinai, ni DPP ndio huanzisha mashitaka. DPP ana mamlaka ya kuingilia kesi yoyote ikiwa hatua yoyote kabla ya hukumu, kuibadili, kuifuta, kupunguza washitakiwa na hata kuifuta kesi kwa Nolle, na DPP hapaswi kutoa sababu yoyote wala kuulizwa na yoyote hata rais wa JMT hana mamlaka ya kuulizwa chochote kwa DPP!. Mtu mwingine mwenye mamlaka ambayo rais hana uwezo wa kuuliza ni CAG kwenye kuwasilisha ripoti ya CAG Bungeni, Ripoti hiyo inawasilishwa Bungeni na rais, ikitokea rais asipoiwasilisha, then CAG amepewa mamlaka ya kuachana na rais, na kuiwasilisha mwenyewe ripoti hiyo, hilo likitokea, Bunge baada ya kuipokea, linamshughulikia rais kwa mujibu wa kufungu 46. Na Bunge likigoma kupokea ripoti ya CAG, linavunjiliwa mbali!.

Sote tumemsikia rais Samia alichosema kuhusu kuhusu ofisi ya DPP na kilio cha haki. Rais Samia ameonyesha nia ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki kwa kauli na matendo, ikiwemo kumuondoa DPP aliyekuwepo na kumteua DPP mpya ili tuanze upya. Jee DPP mpya ataweza kuanza upya kutenda haki, huku amezongwa na lundo la uchafu wa uvundo mkali uliotokana na machozi, jasho na damu, au aanze kwanza na usafi wa kusafisha uozo aliokuta?, au kwa vile DPP hatakiwi kuingiliwa hivyo tumuache tuu?. N mwisho jee kumshauri DPP kama nifanyavyo kwenye makala hiyo, ni kumuingilia?

Wasalaam
Jumapili Njema.
Rejea za Mwandishi Kuhusu DPP.
Paskali.
Huyo alikua kwenye ofisi hiyo akiwabambikizia watu kesi,jumong ni mweupe anateua watu waliokosa ueledi kuongoza...hakuna jipya chini ya macho kumchuzi
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom