Wimbo wa ''Tazama Ramani'' ulitungwa na nani?

Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzani Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi za kuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa

Tanzania Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Hukimbizwa na walo wezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania
Mola awe na we daima.

Wow!! mpaka vinyweleo vimesimama, hakika huu wimbo ulistahili kua ni wimbo wa Taifa.
Sahihi kabisaa R I.P BRIGEDIA M. NNAUYE katuachia wimbo ulio TUFUNZA UZALENDO TUKIWA BADO WADOGO
 
wimbo huo ulitugwa na mzee juma njemba mwaka 1969 huko mwanga kigoma then akapewa mwanafunzi msabaha kashora aliekuwa anasoma jitegemee dar
 
Hahah kwani mkuu ulitaka waishije?

Mkuu wa Majeshi mstaafu ndg. Sarakikya mwenyewe analalamika kulipwa pensheni ya elfu 50 kwa mwezi,je hao waimbaji watakua na hali gani?hahah
Miye nawashangaaga watumishi wengine wauma wanakomaaga na mambo mpaka unawaza hivi hawa wanaijua serikali ya Tanzania, kituko huwa namuona kwa mastari wastaafu yani mtu anastaafu leo hii ila wiki ijayo wenzake hao hao wanaanza mnyanyasa utasikia nini wewe una nini wewe yani kama bar alikuwa akifika anakutana na bia za offer mfulilizo zote zinakata gafla akienda maeneo hata maji ya jero hapati offer, ukita katika utawala yani ndio wanamsahau kabisa mpaka unajiuliza hivi uyu si anasiri za serikali mbona yupo wamemsahau hivi
 
Ni watanzania wote tu hatuna hulka ya kupendana na kuthaminiana, nenda hata kwenye nyumba za ibada ni hayohayo uliyosema hapo juu, nenda hata kwenye koo zetu nako ni sawa tu.
 
Maisha yangu huwa nakomaa sana kujua tamaduni za kabila langu la kihehe hasa lugha na ngoma zetu. Na kwa kuwa ni mtoto wa mjini wakati wa utoto wangu kila likizo nilienda kwa g.parents maana ndo walikuwa wananiongelesha kilugha na kusimuliwa hadithi kwa lugha mama ya kabila letu.

Na hata nikipata mtoto Mungu akijalia basi nitahakikisha watoto wangu wajue lugha ya kabila lao na sehemu ya tamaduni za kihehe
Heko kwako Mr. Region.... ni jambo jema sana kupenda asili yako na kuithamini hiyo ndio hazina ya vizazi vyako.
 
Katika hili la kustaafu pamoja na kuwa wanasiasa wamelidandia na kulipotezea maana ila nadhani mfumo huu wa sasa wa kumlipa mstaafu kidogo kidogo ni mzuri sana!
Sabbu wengi walikuwa baada ya kumaliza pesa mkupuo ya kiinua mgongo walikuwa wanadharirika sana.! Unakuta yupo mtaani hana mbele wala Nyuma na umri umeshamtupa mkono.!
Hili la 25% huenda likasaidia kuwafanya bado waendelee kupata heshma kiasi kwenye jamii yao.
Miye nawashangaaga watumishi wengine wauma wanakomaaga na mambo mpaka unawaza hivi hawa wanaijua serikali ya Tanzania, kituko huwa namuona kwa mastari wastaafu yani mtu anastaafu leo hii ila wiki ijayo wenzake hao hao wanaanza mnyanyasa utasikia nini wewe una nini wewe yani kama bar alikuwa akifika anakutana na bia za offer mfulilizo zote zinakata gafla akienda maeneo hata maji ya jero hapati offer, ukita katika utawala yani ndio wanamsahau kabisa mpaka unajiuliza hivi uyu si anasiri za serikali mbona yupo wamemsahau hivi
 
Ulitungwa na hayati brigedia mnauye..alipata pia kuwa mshauri wa raisi mkapa..ndiye baba mzazi wa nape mnauye..so nape anavyowaambia kuwa ana mizizi muwe mnamuelewa..mzee mnauye si jina la kutafuta Tanzania.. Ana historia yake
 
Ok nyimbo gani nyingine alizotubga Moses Nnauye.? Je waweza kutupa historia yake kama unayo.?
Ulitungwa na hayati brigedia mnauye..alipata pia kuwa mshauri wa raisi mkapa..ndiye baba mzazi wa nape mnauye..so nape anavyowaambia kuwa ana mizizi muwe mnamuelewa..mzee mnauye si jina la kutafuta Tanzania.. Ana historia yake
 
TRUE SHULE ZA ENGLISH MEDIA HAKIKA HAZIWAJENGI VIJANA KUIJUA NCHI YAO. WENGI HAWAJUI HATA GEOGRAFIA VIZURI YA NCHI. MUULIZE TANZANIA INA WILAYA NGAPI, HALMASHAURI ZA WILAYA NGAPI UTASHANGAA MAJIBU ATAKAYOKUPA.
 
Appreciation ya kikubwa ulichokifanya upaswi kuishi kwenye dhiki, hivi mtunzi wa wimbo mmoja wapo awepo alafu kula yake kwa siku haieleweki unadhani inaleta picha gani kwa jamii inayomzunguka kuhusu serikali?
Appreciation si pesa pekee, rudi darasani
 
Wana jamvi lazima mujuwe utofauti wa wimbo wa taifa Yani mungu ibariki Africa /mungu ibariki Tanzania hiyo ni dua/ maombi maalum ya kuliombea taifa ndiomaa anatajwa Mungu.ingqwa serikali haiamini mungu lakini wanao ongoza na wanao ongozwa na hiyo serikali wanaamini mungu ,na ndiomaa mwisho wa winbo wa taifa tunasema tubariki watto wa Africa / Tanzania ,so lazima utabakia Kuwa wimbo wa taifa na hizo zingine 2 pia ni nyimbo maalum mzuri za kitaifa ,nakumbuka mtunzi wa Tanzania nakupenda ni Mzee Mussa Mnauye baba yake mhe Nape ,ila huu tazama kwenye ramani sijui ulitungwa na Nani ? Na kwanni hauimbwi Sana hata shule za msingi sijui kma unaimbwa ,mm kwa Mara ya kwanza niliujulia nikiwa advance secondary kidato Cha 5
 
Duuh pole sana Tazama ramani mimi nimefundishwa nikiwa darasa la tatu shule ya msingi Ihanda mbozi. Miaka ya hiyo.. !
Na bado tukiwa kwenye mchakamchaka tuliimba nyimbo nyingine za kizalendo.
Leo hizo sijui st.. nini zenu sijui hata kama wana Bendi ya shule au Ukaguzi, au Mchakamchaka.! Au elimu ya kujitegemea shamba la shule.au hata Sayansi kimu siku ya kupika shuleni..
Sijui kama hayo huko kwenu kwenye elimu ya kisasa yapo.
 
Huu wimbo uliwekwa Maneno tu ila tune ilikopiwa toka tune za kivita huko Russia au ulaya mashariki. 2010 wakati star times imeanza kuna channel ya muvie za kizanani inaitwa TCM (Kama cjakosea) ilikuwa inaonesha muvi za kivita za kizamani sana za wanajeshi wanatumia farasi zinazokokota magari ya kizamani sana (black and White), cku moja usiku Sana niliamka nikawasha TV nikaweka TCM (2010) nikakutana na muvi wanajeshi wanapiga matarumbeta wabaimba hiyo tune. Kwa kweli najilaumu sana kushindwa kurekodi hiyo muvi. Hapo ndio niligundua kuwa huu wimbo tulikopi tukaweka Maneno tu. Lakini ni ubunifu vile vile kwa aliyeweka Maneno. Mm niliskia kuwa ni moses nnauye cjui kama ni kweli
 
Ulitungwa na hayati brigedia mnauye..alipata pia kuwa mshauri wa raisi mkapa..ndiye baba mzazi wa nape mnauye..so nape anavyowaambia kuwa ana mizizi muwe mnamuelewa..mzee mnauye si jina la kutafuta Tanzania.. Ana historia yake
Mleta hoja ametaja nyimbo mbili ambazo ni Tazama Ramani na Tanzania Nakupenda kwa Moyo wote. Kati ya hizo Brig. Nnauye katunga upi?
 
Huu wimbo uliwekwa Maneno tu ila tune ilikopiwa toka tune za kivita huko Russia au ulaya mashariki. 2010 wakati star times imeanza kuna channel ya muvie za kizanani inaitwa TCM (Kama cjakosea) ilikuwa inaonesha muvi za kivita za kizamani sana za wanajeshi wanatumia farasi zinazokokota magari ya kizamani sana (black and White), cku moja usiku Sana niliamka nikawasha TV nikaweka TCM (2010) nikakutana na muvi wanajeshi wanapiga matarumbeta wabaimba hiyo tune. Kwa kweli najilaumu sana kushindwa kurekodi hiyo muvi. Hapo ndio niligundua kuwa huu wimbo tulikopi tukaweka Maneno tu. Lakini ni ubunifu vile vile kwa aliyeweka Maneno. Mm niliskia kuwa ni moses nnauye cjui kama ni kweli
Ahsante. Kumbuka mleta hoja ametaja nyimbo mbili ambazo ni Tazama Ramani na Tanzania Nakupenda kwa Moyo wote. Kati ya hizo nyimbo mbili ni upi unaorandana na huo ulioona wanajeshi wakiimba kwenye TV?
 
Back
Top Bottom