Wimbo wa ''Tazama Ramani'' ulitungwa na nani?

Katika hili la kustaafu pamoja na kuwa wanasiasa wamelidandia na kulipotezea maana ila nadhani mfumo huu wa sasa wa kumlipa mstaafu kidogo kidogo ni mzuri sana!
Sabbu wengi walikuwa baada ya kumaliza pesa mkupuo ya kiinua mgongo walikuwa wanadharirika sana.! Unakuta yupo mtaani hana mbele wala Nyuma na umri umeshamtupa mkono.!
Hili la 25% huenda likasaidia kuwafanya bado waendelee kupata heshma kiasi kwenye jamii yao.
Watu wanataka hela zao wajenge vibanda vya kuwasitiri wewe unaongelea mambo ya kuadhirika?

Kwanini hao wabunge wasingeanza wao kwa kupewa hio hela polepole instead wanapewa lumpsum?

Unajua watumishi wanakua mpk hayo mafao yao wanakua wameshayakopea?Unapompa hio 25% unataka afanyaje?
 
Tanzania x2, nakupenda kwa moyo wotee
nchi yangu Tanzania nakupenda kwa moyo wote.
wimbo huu umenitoa machozi mara nyingi sana iniuimbapo
Tazama ramani utaona Nchi nzuri yenye mito, na mabonde mengi ya nafaka.!

Je wimbo huu ulitungwa na nani..? Mwaka gani? Na je mtunzi wa wimbo huu amepewa hadhi na heshima gani katika Taifa letu? Kwa Sasa yuko wapi?
Je ana hati miliki ya wimbo huo? Kama hana je wimbo huu unamilikiwa na nani?

Sambamba na wimbo huo pia ninatamani kufahamu mtunzi wa wimbo wa

Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, Nchi yangu Tanzania Jina lako ni tamu sana.!

Mwisho ninatoa wazo kwa wizara ya Utamaduni na michezo kubadili wimbo wa Taifa badala ya ule wa sasa ili wimbo rasmi wa Taifa uwe huu wa pili

"Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote"....!!

Sabbu kwa mtazamo wangu ni wimbo unaoamsha zaidi ari ya uzalendo kwa Nchi yetu kuliko ule wa awali.

Nawasilisha jukwaani kwa majibu na mjadala.
 
Ndugu sikutaka kujikita kwenye siasa nimeongea uzoefu wangu na maisha halisi ya watu ninao ishi nao na ninao wafahamu sio wawili wala mmoja. Na sio kwa mkoa mmoja watu hawa walilipwa ma milioni ya pesa. Leo hii ukiyaangalia maisha yao Mungu nisaidie hawana mbele wala nyuma.

Hebu fanya tathmini ya watu waliopewa pesa ya mkupuo kama mafao wangapi wanaishi vema baada ya kustaafu na wangapi wana maisha magumu.

Ikiwa umejielekeza kwenye siasa wala sitataka kubishana na wewe sabbu najua lengo la siasa lakini ikiwa unataka kujua ukweli usio wa kisiasa angalia wastaafu kutoka majeshi yetu wanavyoishi baada ya kustaafu.

Halafu leta tathmini wangapi wako vizuri na wangapi wanaadhirika mitaani wangapi wamejenga na wangapi wamekuwa maskini zaidi ya awali.
Watu wanataka hela zao wajenge vibanda vya kuwasitiri wewe unaongelea mambo ya kuadhirika?

Kwanini hao wabunge wasingeanza wao kwa kupewa hio hela polepole instead wanapewa lumpsum?

Unajua watumishi wanakua mpk hayo mafao yao wanakua wameshayakopea?Unapompa hio 25% unataka afanyaje?
 
Tanzania x2, nakupenda kwa moyo wotee
nchi yangu Tanzania nakupenda kwa moyo wote.
wimbo huu umenitoa machozi mara nyingi sana iniuimbapo
Ninatamani huu ungekuwa ndio wimbo wetu wa Taifa. Ni wimbo unao amsha Ari ya uzalendo kipekee.!
Kuliko hata huo Mungu ibariki Afrika.
 
Mm mwenyewe mpaka leo sijaelewa kila taifa lina nyimbo yake ya taifa iweje sisi tanzania katika wimbo wetu wa taifa tuingize africa tena
 
Ahsante Mkuu mtu huyu historia yake ilikuwaje? Familia yake iko wapi? Alikuwa anafanya kazi gani.? Na je ndie mtunzi wa nyimbo zote mbili?
Anaitwa Felician Albert Nyundo (RIP)
Huo wa Tanzania Tanzania...nakupenda kwa moyo wote nilisikia ulitungwa na Mzungu aliyeishi Tanzania...alikuwa mpiga kinanda.
 
Ndugu sikutaka kujikita kwenye siasa nimeongea uzoefu wangu na maisha halisi ya watu ninao ishi nao na ninao wafahamu sio wawili wala mmoja. Na sio kwa mkoa mmoja watu hawa walilipwa ma milioni ya pesa. Leo hii ukiyaangalia maisha yao Mungu nisaidie hawana mbele wala nyuma.

Hebu fanya tathmini ya watu waliopewa pesa ya mkupuo kama mafao wangapi wanaishi vema baada ya kustaafu na wangapi wana maisha magumu.

Ikiwa umejielekeza kwenye siasa wala sitataka kubishana na wewe sabbu najua lengo la siasa lakini ikiwa unataka kujua ukweli usio wa kisiasa angalia wastaafu kutoka majeshi yetu wanavyoishi baada ya kustaafu.

Halafu leta tathmini wangapi wako vizuri na wangapi wanaadhirika mitaani wangapi wamejenga na wangapi wamekuwa maskini zaidi ya awali.
Kwamba serikali ina huruma na watu wake sio?

Nimekuuliza swali rahisi,kwanini Wabunge nao wasingeanza kulipwa hio 25% instead wanalipwa hela yao yote zaidi ya mil 200 kwa kazi ya miaka 5 tu wkt mstaafu aliyefanya kazi kwa miaka 30 mwenye kiinua mgongo kisichozidi hata mil. 80 anyimwe pesa yake?
 
wimbo huo ulitugwa na mzee juma njemba mwaka 1969 huko mwanga kigoma then akapewa mwanafunzi msabaha kashora aliekuwa anasoma jitegemee dar
Mleta hoja ametaja nyimbo mbili ambazo ni Tazama Ramani na Tanzania Nakupenda kwa Moyo wote. Ni upi kati ya hizo mbili ulitungwa na huyo Juma Njemba? Kwa vyovyote vile kuna mambo makubwa mawili:

1. Kama umemtaja Juma Njemba yule sangoma tuliyesikia habari zake baadhi yetu wakati hausiki kwenye utunzi ni wazi unavuruga mijadala yenye tija kwa taifa.

2. Kuna waliokwisha wataja marehemu wawili Felician Albert Nyundo na Brig. Moses Nnauye kuwa watunzi wa hizo nyimbo mbili tofauti. Kwa kumtaja huyo J. Njemba (kama siyo utani tu) hiyo inaelekea kuleta mzozo utakaohusu mtunzi halisi wa moja ya nyimbo hizo.
 
Mimi ningependa kujua jina la mtunzi wa wimbo usemao Mabepari Walia Kukatiwa Mirija, Walipotangaziwa Azimio la Arusha.
 
Mungu ibariki siukubali kabisa,nikiwa Rais naufuta asubuhi na mapema.
 
Kiongozi uzi wako ulikuwa unataka kumjua mtunzi. Sikujua ulikuwa unataka kujua mengi hivyo.

Nakumbuka alikuwa mwajiriwa wa RTD kama fundi mitambo. Alikuwa ni mtunzi mahiri sana wa nyimbo nyingi sana zilizotamba kanisa Katoliki enzi hizo. Alifariki baada ya kupata ajali ya gari. Mtu huyu alikuwa mwenye asili ya mkoa wa Kigoma.
Umeitaja kigoma?,Du kigoma na mziki ni pipa na mfuniko.
 
Mm mwenyewe mpaka leo sijaelewa kila taifa lina nyimbo yake ya taifa iweje sisi tanzania katika wimbo wetu wa taifa tuingize africa tena
Nyerere na pan-africanism alikua damu damu.

Nyerere aliamini kama the rest of Africa itakua haina amani then hata Tanzania hali ingekua ni tete tu.

Ndio maana ya "Mungu ibariki Africa, wabariki viongozi wake".
 
Kwa wakati ule nadhani ilikuwa kutunga wimbo na ukapata.hadhi ya kitaifa ilikuwa na fahari na heshma tu ya mtu mwenyewe kama vile unavyoweza kucheza vizuri mbele ya Rais akakupa zawadi lakini
Kwa kizazi cha leo utunzi ni biashara nabkuna hati miliki pia
Ndio maana nikahoji ili wale ambao wanafahamu chochote basi kupitia jukwaa hili watupe majibu.
Sasahivi mambo yamebadilika kila mtu anajua sheria na haki za msingi.
 
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzani Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi za kuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa

Tanzania Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Hukimbizwa na walo wezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania
Mola awe na we daima.

Wow!! mpaka vinyweleo vimesimama, hakika huu wimbo ulistahili kua ni wimbo wa Taifa.
Huu ndio wimbo wangu bora kabisa, nikiusikia au kuuimba huwa ninakuwa nafeelings ambazo kwakweli najiona ni raia wa Tanzania na kwa vyovyote vile najukumu la kuifanyia kitu nchi yangu, wimbo unaamsha hisia zote za uzalendo, Huu kwakweli uwe wimbo wa taifa.
 
Ahsnte mkuu.!
Sabbu zama zimebadirika kipindi cha ukombozi wa Afrika kutoka kwa ukoloni wa kisiasa kimeisha tupo katika ukombozi wa kiuchumi ambao unahitaji sana uzalendo.
Kuliko silaha nyingine

Ninaona kama wimbo Tanzania Tanziania nakupenda kwa moyo wote unaleta hisia kali zaidi za kizalendo kuliko Mungu ibariki Afrika., natumai wahusika wapo humu wanaweza chukua hili wazo.
Wimbo wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo WOTE ulitungwa na Moses Nnauye
 
Huu ndio wimbo wangu bora kabisa, nikiusikia au kuuimba huwa ninakuwa nafeelings ambazo kwakweli najiona ni raia wa Tanzania na kwa vyovyote vile najukumu la kuifanyia kitu nchi yangu, wimbo unaamsha hisia zote za uzalendo, Huu kwakweli uwe wimbo wa taifa.
Upo sahihi kabisa.
 
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzani Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi za kuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa

Tanzania Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Hukimbizwa na walo wezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania
Mola awe na we daima.

Wow!! mpaka vinyweleo vimesimama, hakika huu wimbo ulistahili kua ni wimbo wa Taifa.
Hakika View attachment VID-20181210-WA0022.mp4
 
Nilichoelewa Wimbo wa Tazama Ramani ulitungwa na Felician Albert Nyundo,
wimbo wa Tanzania nakupenda ulitungwa na Brig. Moses Nnauye,

Je na huu Mungu ibariki katunga nani?
 
Back
Top Bottom