Wimbo wa Taifa ubadilishwe

Wimbo wa Taifa ubadilishwe

Mkuu wimbo huu ukibadilishwa hivi sasa, wimbo mpya utajaa vituko virupu, na kwa jinsi nchi hii hivi sasa ilivyojaa machawa wengi, wimbo huo utaharibiwa na kujaa sifa na kuaabudu, na hata utasikia vionjo vya maneno mengi yakujipendekeza kama vile kutajwa kabisa kwa jina la Dkt. Samia Suluhu ndani yake.

Kwanza kwa kadiri ninavyoijua serikali ya CCM jinsi ilivyo, jukumu la utunzi wa wimbo huo watamkabidhi mtu kama Mrisho Mpoto ili kwa makusudi ya kuweka vionjo vya kichawa ndani yake. Hapo tegemea kupata maboko matupu tu.
Halafu utaambiwa uandaaji wa wa wimbo umegharimu bilioni 300.
 
Mimi nadhani wimbo wetu tukufu wa taifa unafaa kubadilishwa hasa pale panaposema WABARIKI VIO-NGOZI WETU maana haiwezekani tukawa tunawaombea baraka viongozi matapeli, wanyanyasaji na wakandamizaji Kama baadhi ya hawa tulio nao.

Na huwenda haya tunayopitia na kutosikiwa na Mungu huwenda ni sababu ya midomo yetu na baraka tunazowaombea katika wimbo ule.

Huenda Mungu anatushangaa kwamba "aah hawa ni machizi nini mbona wanalia wanaonewa na hao viongozi afu hapohapo wanawaombea baraka kwangu au wanadanganya hawaonewi chochote" Kiufupi matendo ya viongozi wetu yameunajisi wimbo wetu wa taifa.

Yani huenda unakuata kiongozi anawekesha watu chupa za makalio, mwizi, mmakaji, mzurumati, tapeli, jambazi, anua watu huko migodini, anaibia nchi mafuta bandarini, anakwiba fedha za umma, muuwaji, anaibia masikini wake zao, anatia mimba watoto wa shule, jizi la ardhi za watu afu eti unapoimba wimbo wa taifa umuombee baraka. Hiyo no, wimbo ubadirike hapo tufute
Kwanza hauna maana yoyote maana nchi imejaa majangili tupu
 
Mimi nadhani wimbo wetu tukufu wa taifa unafaa kubadilishwa hasa pale panaposema WABARIKI VIO-NGOZI WETU maana haiwezekani tukawa tunawaombea baraka viongozi matapeli, wanyanyasaji na wakandamizaji Kama baadhi ya hawa tulio nao.
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wimbo wa Taifa hauna kosa wala hakuna haja ya kuubadili.

Uongozi una misingi yake na kila kiongozi anatakiwa kuifuata kwa maslahi ya anaowaongoza. Hivyo hata wimbo ulitungwa kwa misingi hiyo.

Ni kukengeuka tu kwa viongozi wetu.
 
Mimi nadhani wimbo wetu tukufu wa taifa unafaa kubadilishwa hasa pale panaposema WABARIKI VIO-NGOZI WETU maana haiwezekani tukawa tunawaombea baraka viongozi matapeli, wanyanyasaji na wakandamizaji Kama baadhi ya hawa tulio nao.

Na huwenda haya tunayopitia na kutosikiwa na Mungu huwenda ni sababu ya midomo yetu na baraka tunazowaombea katika wimbo ule.

Huenda Mungu anatushangaa kwamba "aah hawa ni machizi nini mbona wanalia wanaonewa na hao viongozi afu hapohapo wanawaombea baraka kwangu au wanadanganya hawaonewi chochote" Kiufupi matendo ya viongozi wetu yameunajisi wimbo wetu wa taifa.

Yani huenda unakuata kiongozi anawekesha watu chupa za makalio, mwizi, mmakaji, mzurumati, tapeli, jambazi, anua watu huko migodini, anaibia nchi mafuta bandarini, anakwiba fedha za umma, muuwaji, anaibia masikini wake zao, anatia mimba watoto wa shule, jizi la ardhi za watu afu eti unapoimba wimbo wa taifa umuombee baraka. Hiyo no, wimbo ubadirike hapo tufute
Naunga mkono hoja.
Hatuwezi kuombea Baraka vibaka
 
Ndio maana unapopigwa wimbo wa taifa huwa siimbi kabisa, hasa nikiangalia viongozi wenyewe wanaoombewa baraka.

Bora niinjoy tu! 😡
 
Mkinichagua kuwa Rais, ndani ya siku 100 za uongozi wangu uliotukuka; nitawaita magwiji wa nota za muziki nchini ili wayaboreshe mashairi ya ule wimbo wa Tazama ramani ili uwe ndiyo wimbo wa Taifa. Wimbo wa kibabe sana ule.

Huu wa sasa kwanza umepooza! Halafu tulidesa kutoka kwa mtunzi wa Afrika ya Kusini. Hivyo sioni kama una tija kwenye dunia ya sasa. Kwanza hauna chembe chembe za uzalendo. Zaidi ya kuleta hizo stori za kubariki watu, sijui viongozi, na bla bla nyingine.
Nyerere ameukomeshaa...
Karume ameukomeshaaa..
Tanu imeukomeshaa.....
Napata shida kidogo hapo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom