Wimbo upi? Kumbukumbu ipi?

shareef95nes

Senior Member
Jan 16, 2013
108
16
Habari,

Nyimbo hutukumbusha matukio mbalimbali yaliyopata kututokea hapo nyuma.Matukio haya yanawezakuwa ya furaha au huzuni katika swala zima la mahusiano.

Binafsi nikisikia wimbo wa "Missing you" by Busy Signal nakumbuka miaka miwili nyuma nilipokuwa na mpenzi wangu wa zamani katika fukwe moja jijini Dar tukipunga upepo huku wimbo huu ukituburudisha.

Je,wimbo upi ambao ukiusikia unakufanya ukumbuke tukio fulani?

Kumbukumbu hiyo ni ipi?

Ahsanteni!
 
Wimbo wa If I culd turn back the hand of clock " wa RKelly hunikumbusha watu wangu wa karibu waliotangulia kwa Mungu
 
daaah! paper lovin by chris martins, nikiiskiaga nakumbuka nilivyokuwa na piga mtongozo siku ya mwaka mpya three yrs back mitaa flani hivi yenye utulivu wa hali ya juu,mtoto hakuchomoa na mpaka leo nnae.
 
hongera kwa kumbukumbu nzuri yenye kuvutia
 
Wimbo Wa 'nikusaidieje' Wa Pr Jay,. 'Nampenda Yeye' Wa Mh. Temba, 'dhahabu' Wa Dully Sykes,. Zinanikumbusha Utamu Wa Bongoflava Za Zamani, Zilikuwa Zimetulia Sana, Uache Za Sasa Wanakurupuka,. Nyimbo Zima Inapigwa Hupati Ladha Wala Maana., Kwa Upande Wangu Wananikera Sana.
 
Wimbo wa my love is your love wa Whitney Houston unanikumbusha 2001 nilipopanda tax stend ya ipogolo Iringa, dereva tax aliweka kanda yake wakati naenda kuanza kidato cha tano Mkwawa high school.
 
Cindelelaaa wa ally kiba..unanikumbusha 2007/8 for the first time naanza kuja dar....ulikuwa ndio wimbo maarufu
 
Habari,

Nyimbo hutukumbusha matukio mbalimbali yaliyopata kututokea hapo nyuma.Matukio haya yanawezakuwa ya furaha au huzuni katika swala zima la mahusiano.

Binafsi nikisikia wimbo wa "Missing you" by Busy Signal nakumbuka miaka miwili nyuma nilipokuwa na mpenzi wangu wa zamani katika fukwe moja jijini Dar tukipunga upepo huku wimbo huu ukituburudisha.

Je,wimbo upi ambao ukiusikia unakufanya ukumbuke tukio fulani?

Kumbukumbu hiyo ni ipi?

Ahsanteni!
Manungayembe.
 
Fally Ipupa-Sweet life, nakumbuka ilikuwa morogoro kikazi nikapata one night stand moja na mtoto nuru, dah! life is beautiful kwakweli!
 
Wimbo Wa 'nikusaidieje' Wa Pr Jay,. 'Nampenda Yeye' Wa Mh. Temba, 'dhahabu' Wa Dully Sykes,. Zinanikumbusha Utamu Wa Bongoflava Za Zamani, Zilikuwa Zimetulia Sana, Uache Za Sasa Wanakurupuka,. Nyimbo Zima Inapigwa Hupati Ladha Wala Maana., Kwa Upande Wangu Wananikera Sana.
kweli kabisa
 
Fally Ipupa-Sweet life, nakumbuka ilikuwa morogoro kikazi nikapata one night stand moja na mtoto nuru, dah! life is beautiful kwakweli!
these are the unforgettable moments am talking about...hutasahau kamwe as long as hiyo "sweet life" ya fally ipupa ipo hai....kweli life with music is sweet
 
Wimbo wa mzee wa busara unanikumbusha siku ya kwanza unatoka niliusikiliza radio free africa masafa ya kati mitabendi 1600 kipindi kinaitwa showtime, nakumbuka nilikuwa nachunga ng'ombe zetu takriban 64 mbuzi 40, na kondoo 26 peke yangu, nakumbuka marisho yalikuwa takribani kilomita 8-13 toka nyumbani, #Sitosahau
 
Nakumbuka 'my love' wa west life dedication ya kwanza kabisa kupewa iliandikwa kwenye barua ndeefu ya maua maua na Perfume juu.
 
it's all coming back to me now wa celin dion........... unanikumbusha Joseph Wang after his death maana ndo ulikuwa unanifariji

go the distance by Michael Bolton unanikumbusha
siku nahitimu form four phwezi girls mkoani Rumphi nchini Malawi

thats why you go away wa Lionel Rich..... nilipo achwa na first man whom I loved ever
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka 'my love' wa west life dedication ya kwanza kabisa kupewa iliandikwa kwenye barua ndeefu ya maua maua na Perfume juu.
Hahahaaaaa umenikumbusha mambo ya kuandika barua kwenye zile karatasi zenye maua na kupulizia perfume. ..
Dahhh!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom