Gang Chomba
Platinum Member
- Feb 29, 2008
- 20,734
- 4,871
Wapenzi wa Muziki,
Nyimbo gani Imewakaa kichwani leo, na kwanini?
Mimi leo tangu niamke, nausikilizia, "A Rose By Any Other Name, by Teena Marie feat. Gerald Levert (RIP)....
Ndugu Kisura salama lekum. Sina lengo la kukosoa umahiri wako katika ujuvi wa lugha ya Kiswahili bali naomba kuangalia kwa pamoja usahihi wa matumizi ya Neno NYIMBO.
Niliposoma heading yako kwa haraka nilidhani kuwa unamaanisha nyimbo zilizowakaa watu vichwani lakini baadaye nikabaini kuwa ulimaanisha WIMBO mmoja na sio nyingi na ulipotumia neno "Imewakaa "
"Nyimbo gani Imewakaa kichwani leo, na kwanini?"
Katika siku za karibuni kumetokea matumizi ya neno NYIMBO badala ya WIMBO kitendo ambacho ni ukiukaji mkubwa wa kanuni za sarufi. Na bahati mbaya sana kwa Watanzania ambao hupenda kutumia maneno bila kufanya utafiti. Nimekuwa nikipata shida sana ninapofikiri kuwa ipo siku, kutokana na changamoto za utandawazi, huenda watanzania tukanyimwa AJIRA kwa kutojua Kiswahili, kwa sababu tu ya kupenda kudandia matumizi ya maneno yanayokwenda kinyume na kanuni za sarufi ya lugha husika.
Lugha ya Kiswahili inaonekana kuwa Mhanga wa tatizo la ukiukaji wa kanuni aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Lakini sababu ya bahati mbaya, mimi binafsi naweza kuona haipo bali ni makusudi yanayotokana na mkakati wa Wasomi wa Tanzania katika kuiwa Lugha ya Kiswahili kwa manufaa ya Lugha ya Kiingereza.
Kwa matumizi ya neno NYIMBO badala ya WIMBO ni kielelezo cha mkakati wa huo japokuwa ni vigumu sana kushinda. Hata ndugu Kisura ameshindwa kuivunjilia mbali kanuni ya matumizi neno Wimbo alipojikuta akitumia neno "nausikilizia"
Hata hivyo kwa kuwa sikuwa na lengo la kuandika makala kuhusu matumizi ya neno wimbo, naomba nimalize kwa kutoa angalizo katika msamiati wa lugha ya Kiswahili hakuna neno "NYIMBO"linalomaanisha WIMBO bali neno NYIMBO ni wingi wa neno WIMBO ambalo lipo katika NGELI ya U-ZI yaani WIMBO UPI na NYIMBO ZIPI.
ChiefMtz,Ndugu Kisura salama lekum. Sina lengo la kukosoa umahiri wako katika ujuvi wa lugha ya Kiswahili bali naomba kuangalia kwa pamoja usahihi wa matumizi ya Neno NYIMBO.
Niliposoma heading yako kwa haraka nilidhani kuwa unamaanisha nyimbo zilizowakaa watu vichwani lakini baadaye nikabaini kuwa ulimaanisha WIMBO mmoja na sio nyingi na ulipotumia neno "Imewakaa "
"Nyimbo gani Imewakaa kichwani leo, na kwanini?"
Katika siku za karibuni kumetokea matumizi ya neno NYIMBO badala ya WIMBO kitendo ambacho ni ukiukaji mkubwa wa kanuni za sarufi. Na bahati mbaya sana kwa Watanzania ambao hupenda kutumia maneno bila kufanya utafiti. Nimekuwa nikipata shida sana ninapofikiri kuwa ipo siku, kutokana na changamoto za utandawazi, huenda watanzania tukanyimwa AJIRA kwa kutojua Kiswahili, kwa sababu tu ya kupenda kudandia matumizi ya maneno yanayokwenda kinyume na kanuni za sarufi ya lugha husika.
Lugha ya Kiswahili inaonekana kuwa Mhanga wa tatizo la ukiukaji wa kanuni aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Lakini sababu ya bahati mbaya, mimi binafsi naweza kuona haipo bali ni makusudi yanayotokana na mkakati wa Wasomi wa Tanzania katika kuiwa Lugha ya Kiswahili kwa manufaa ya Lugha ya Kiingereza.
Kwa matumizi ya neno NYIMBO badala ya WIMBO ni kielelezo cha mkakati wa huo japokuwa ni vigumu sana kushinda. Hata ndugu Kisura ameshindwa kuivunjilia mbali kanuni ya matumizi neno Wimbo alipojikuta akitumia neno "nausikilizia"
Hata hivyo kwa kuwa sikuwa na lengo la kuandika makala kuhusu matumizi ya neno wimbo, naomba nimalize kwa kutoa angalizo katika msamiati wa lugha ya Kiswahili hakuna neno "NYIMBO"linalomaanisha WIMBO bali neno NYIMBO ni wingi wa neno WIMBO ambalo lipo katika NGELI ya U-ZI yaani WIMBO UPI na NYIMBO ZIPI.
Wimbo uliyonikaa kichwani kwa siku ya leo ni ANITA wa Matonya. Binti Kisura nashukuru kwa shukrani zako.