Wimbi la Wazayuni wanaoikimbia Tel Aviv kukwepa makombora ya Hamas lazidi kuwa kubwa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,991
2,000
Wimbi la Wazayuni wanaoikimbia Tel Aviv kukwepa makombora ya muqawama lazidi kuwa kubwa

May 19, 2021 03:14 UTC

Vyombo vya habari vimetangaza kuwa, wimbi la Wazayuni wanaokimbia mji mkuu wa Israel Tel Aviv kutokana na mashambulizi ya wanamapambano wa Palestina linazidi kuwa kubwa, siku baada ya siku.

Jana Jumanne, televisheni ya al Alam imetangaza kuwa, duru za kuaminika zimeiambia tovuti ya Arabi 21 kwamba, wakazi wa Tel Aviv wamekuwa wakikimbia kwa wingi kuelekea upande wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kutokana na kuongezeka mashambulio ya wanamapambano wa Palestina katika mji mkuu huo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi kubwa ya Wazayuni wamekimbia nyumba zao mjini Tel Aviv na kuelekea katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko kwenye Ukingo wa Maghari wa Mto Jordan.

Makundi ya muqawama ya Palestina jana Jumatatu pia yaliendelea kujibu jinai za utawala wa Kizayuni kwa kuyatwangwa kwa makombora na maroketi maeneo mbalimbali ya walowezi wa Kizayuni kama vile al Asqakalan (Ashkelon) na kambi ya kijeshi ya Wazayuni ya Kissufim.

Televisheni ya al Mayadeen iliripoti kuwa, wanamapambano wa Palestina wanaendelea kujibu jinai za utawala wa Kizayuni unazozifanya mfululizo dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Leo Brigedi za al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS limeyatwanga kwa makombora na maroketi maeneo ya kiistratijia ya kitongoji cha Asqalan (Ashkelon) na pia kambi ya jeshi la utawala wa Kizayuni ya Kissufim.

Vile vile wanamapambano wa Palestina waliipiga kwa makombora kambi ya kijeshi ya Wazayuni ya Mars na kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Erez kaskazini mwa Sderot.

Kambi ya Hatzerim ya jeshi la anga la Israel la utawala wa Kizayuni huko Be'er Sheva nayo imetwangwa kwa makombora ya WaPalestina ikiwa ni kulipiza kisasi jinai zisizo na kifani za Wazayuni dhidi ya raia wa kawaida wa Palestina.
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
7,825
2,000
Acha ushabiki wa kingese wewe punga mpaka sasa uharibifu waliofanya hao waisrael hapo Gaza hautasahaulika.
Hao Hamas wamejibu na vikombora vyao vya kuulia kuku
ndio wanatwangwa sasa.
Na Waisrael wameenda kunywa maji tu walichofanya usiku wanakijua wao
wakirudi kazi inaendelea.
Na ni chimbo kwa chimbo, hao Hamas safari hii watakiona.
Hawa victim wengine wanakutwa tu in the middle of action and battle.
Hao wangese wenzio Hamas anaweza akakutwa kwenye kibano kakimbia wanaenda beba watoto,anabeba mtoto akaanza allah Akbaru×2
hao unaita wa zayoni hapo wanamaliza wote ila target ni huyo jamaa aliyembeba mtoto wanakua na info zake zote.
Huo ndio upuuzi unaofanya watoto wanakufa na vizee nadra na wamama nadra.
Ni hao wanamgambo na wanawashikilia watoto kama protection.
Kwa taarifa yako wanavuaga magwanda hao Hamas na kukimbilia majumbani na ndio kule jamaa akija anabwaga jengo zima hajali nani yumo nani hayumo.
We unatueleza nani anakimbia Jerusalem.?
Una akili wewe shelter zipo kila mahali kukiwa na vita.
Swala watu wameambiwa kakaeni mahali. Kwanza ngoja tumalizane na hawa malofa.
Tena wanapelekwa kwa gari za kijeshi ikifika hali hiyo.
Hamna hata hiyo hali Jerusalem wala Tel Aviv
Usalama upo
Na raia Wanapiga mishe zao tu mtaani maana biashara
Kivita inapigwa pale Palestina Gaza kwa hao Hamas wakiachiwa kidogo Ndio wanarusha vikombora vyao mjini Jerusalem. Na vinadakwa juu kwa juu
Na wenzio hizo zote technic.
Kesho mbali utakuta wote wamejaa balozi zote za Ulaya wanaomba ukimbizi.
Wanapewa wanahamishwa wakienda huko
wanapiga hela wanarudi makwao kujenga

Hapo bongo shelter mkiambiwa zameni mapangoni ndo kwanza mtakimbilia kuangalia na kupiga selfie.🤣
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom