Wimbi la Wazayuni wanaoikimbia Tel Aviv kukwepa makombora ya Hamas lazidi kuwa kubwa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,840
17,438
Wimbi la Wazayuni wanaoikimbia Tel Aviv kukwepa makombora ya muqawama lazidi kuwa kubwa

May 19, 2021 03:14 UTC

Vyombo vya habari vimetangaza kuwa, wimbi la Wazayuni wanaokimbia mji mkuu wa Israel Tel Aviv kutokana na mashambulizi ya wanamapambano wa Palestina linazidi kuwa kubwa, siku baada ya siku.

Jana Jumanne, televisheni ya al Alam imetangaza kuwa, duru za kuaminika zimeiambia tovuti ya Arabi 21 kwamba, wakazi wa Tel Aviv wamekuwa wakikimbia kwa wingi kuelekea upande wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kutokana na kuongezeka mashambulio ya wanamapambano wa Palestina katika mji mkuu huo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi kubwa ya Wazayuni wamekimbia nyumba zao mjini Tel Aviv na kuelekea katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko kwenye Ukingo wa Maghari wa Mto Jordan.

Makundi ya muqawama ya Palestina jana Jumatatu pia yaliendelea kujibu jinai za utawala wa Kizayuni kwa kuyatwangwa kwa makombora na maroketi maeneo mbalimbali ya walowezi wa Kizayuni kama vile al Asqakalan (Ashkelon) na kambi ya kijeshi ya Wazayuni ya Kissufim.

Televisheni ya al Mayadeen iliripoti kuwa, wanamapambano wa Palestina wanaendelea kujibu jinai za utawala wa Kizayuni unazozifanya mfululizo dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Leo Brigedi za al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS limeyatwanga kwa makombora na maroketi maeneo ya kiistratijia ya kitongoji cha Asqalan (Ashkelon) na pia kambi ya jeshi la utawala wa Kizayuni ya Kissufim.

Vile vile wanamapambano wa Palestina waliipiga kwa makombora kambi ya kijeshi ya Wazayuni ya Mars na kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Erez kaskazini mwa Sderot.

Kambi ya Hatzerim ya jeshi la anga la Israel la utawala wa Kizayuni huko Be'er Sheva nayo imetwangwa kwa makombora ya WaPalestina ikiwa ni kulipiza kisasi jinai zisizo na kifani za Wazayuni dhidi ya raia wa kawaida wa Palestina.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom