William Mganga Ngeleja anafaa urais 2015

Tukubali tukatae Ngeleja Ndie rais 2015
we jamaa kweli ni poyoyo wala hujatumwa lkn unajipendekeza ili huyo baba yenu akujue sasa kwa taarifa yako urais siyo shamba la bibi na kama mna njama zenu bas mmefeli mwambie huyo kibaraka mwenzio kua uraisi kwake utabaki story tu za jamii forum,ata juice na chai za Ikulu ataendelea kuzinywa kwa ofa.
 
MH.WILLIUM MGANGA NGELEJA SULUHISHO BORA MADINI

Itakumbukwa kuwa sekta ya nishati na madini ilishawah kukaliwa na nawazir wengi mno wakuwemo kina Mzee Msabaha,Mzee Daniel Yona na wengine wengi tuu,lakini hao wote walikuwa wanaishia kuwa katika wizara hiyo kwa muda wa miaka 2 na nusu na muda mwingine miwili kamili, ni mawazir watatu tuu akiwemo mh.Rais Kikwete pamoja na mh.Willium Mganga Ngeleja ndio waliokaa kwa muda mrefu kulingana na ugumu wa wizara hiyo,Mh.Kikwete alikaa miaka 6 na mh.Willium Mganga Ngeleja alikaaa miaka 5 na miez 8 kitu kinachoonyesha upambanaj mkubwa kwenye wizara hii na mh.Ngeleja, kwaukweli mambo aliyoyafanya yatabaki kuwa msaada mkubwa kwa Tanzania yetu,yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mh.Ngeleja aliyafanya alipokuwa ktk wizara ya Nishat na Madini ikiwa ni kwa muda wa miaka 5 na miez 8,:-

1.Itakumbukwa kuwa Ngeleja ndiye aliyepambana kwa hali na mali mpk kuhskikisha kunapatikana maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo.

2.Itaendelea kukumbukwa kuwa ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa mfuko maalum wa kuwasaidia wadogo nchini kitu ambacho kinazungumzwa na wachimbaji wadogo mpaka leo,na hata juzi nilipokuwa ziarani Geita nilipata kutembelea maeneo ya wachimbaji wadogo na walimtaja Ngeleja kama mkombozi wao,na daima wataendelea kumtukuza kwa anachokifanya kwani anafanya mambo mazur anapokabiziwa majukum ya kijamii.

3.Mwezi April 2010 mh.Ngeleja alipiga marufuku usafirishaji nje ya nchi wa madini ghafi ya Tanzanite yenye ukubwa unaozidi gramu1,kitu ambacho juzi nilivyokuwa nazungumza na baadhi ya mawazir na baadhi ya viongoz wa juu wa chama walikipenda na kusema Ngeleja anafaa kuingia wazir mkuu wa Tanzania au hata Raisi kama akiamua kugombea

4.Mh.Ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa kutoa hati ya uasili(certificate of origin) kwa wanaouza madini ya Tanzanite nje ya nchi ikiwa ni mkakati wa serikali kudhibiti uuzwaji haramu wa madini ya Tanzanite,kitu amabcho hata Prof.Muhongo anajivunia sasa na kipindi fulani hivi ktk ziara yake mererani yanapopatikana madini ya Tanzanite mh.Muhongo alimtaja Ngeleja kama msaada mkubwa katika hilo...

Mwisho
Watanzania tunapaswa kuwasemea watu kwa mabaya yao na mazuri yao yalio mengi kwani hakuna mwanadam aliye kamili,..Ngeleja kafanya mengi sana sekta ya madini na hayo hapo juu ni kwa uchache wake.


ATUELEZE KWANZA ZILE SEMI 100 ALIZONUNUA PESA ALITOA WAPI siku madereva wanafanya interview nilikuwepo ndo sababu ya mimi kujua kuwa ni mali zake, kwaiyo atueleze ilo kwanza alafu ndo mengine yafuate.
 
Vp kuhusu gamba lake la Nishati na Madini ana jipya gani au atarudisha pesa zetu ili zisaidie maendeleo ya Tanzania yetu?
Acheni kutuletea Mchwa jamani ....
 
Mheshimiwa alifanya mengi sana sekta ya nishati na madini, katika kujaribu kuuonesha umma wa watanzania mheshimiwa alifanya nini na ni kwa ninii alistahili kuwepo hapo, mheshimiwa ngeleja ni mtanzania halali na anayajua yanayowakumba watanzania wenzake kama changamoto,sidhan kama ataweza kuyafumbia macho matatizo ya ajira kwa sababu ni mtu mwenye mbinu na ni mbunifu sana kwa upeo wangu wakumjua japo nimekuwa nikizipata taarifa zake kwa media na kumsikia yy mwenyewe kwenye media.
Tukizungumzia nishati na madini ni sehem ya kwanza ya kuanza kumpima mheshimiwa kulingana na unyeti wa wizara hiyo, niseme kuwa sitegemei kama Ngeleja akigombea urais na akapata ridhaa ya kuisimamia Tanzania yetu anaweza kutusahau katika upande wa ajira,afya,elimu, kusimamia ugawanywaji wa rasilimali zetu na mambo mengine yanayofanana na hayo...Namjua kama mpambanaji.
 
Akamuombe kwanza msamaha yule Askari aliyemfukuzisha kazi pale JMALL...
 
habari zingine bana, ngoja nipalilie mahindi yangu mie!!!

kenya-farmer-drought.jpg
Hahahah mkuu umetisha.. Na huo ualaza
 
Na bado. . tutasikia mengi sana kuelekea 2015. Ngoja nami nikajipange nikirudi nashusha nondo za kumpigia kampeni Mh.John Komba. Lazima aende magogoni. . Komba for presidency!!
 
Ngeleja ni kibaraka wa Rostam,Rostam ndio alimuweka Voda kwenye company ambayo anashre,ndio aliyemuweka nishati na madini ili kulinda maslah yake ,watu kama Hawa tukiwapa nchi ni kuiweka reheani Tanzania kwa wafanya biashara kama akina Rostam
 
sasa wee jamaa ethcs unafikiri kupambana hadi kupambana hadi kupatikana kwa maeneo ya wachimbaji wadogo wadogo ni kitu kidogo? acha akiri fupi kasaidia watanzania wengi sana maskini..
 
KIKWETE, NGELEJA NDIO RAISI WA JAMHURI 2015


Bado Hali ni tete ndani ya CCM ,Ila Nani atakaye mrithi JK Ipo wazi na nafasi Hii imemwangukia mbunge kijana Mwenye ufanisi na
Haiba ya kuvutiaa mh William Mganga Ngeleja mmbunge wa sengerema kuendana na kasi iliyopo kwa kumteua mwanasiasa huyu kijana mtaalamu wa fani ya sheria .

Kwanini JK atamwachia Mikoba Hii ni kutokana na Kukubalika na wanachama wengi na watanzania wengi kwa ujumla wao ambao wamehaidi kumpigania Mh Ngelejah endapo atasimamishwa kugombea nafasi Hiyo ambayo inaonyesha wazi ndiye mrithi sahihi hivyo watu wa tanzania wajiandae kushirikiana na mh ngeleja katika mqpambano hayo yenye kuleta tija kwa watanzania kwa ujumla

Vilevile uchapakazi wa Mh Ngelejah Unafanya aaminike zaidi ndani ya chama na kwa wananchi kwa ujumla ,ngeleja anaamini katika kujenga uchumi imara Wenye nguvu utakaopambana na umaskini na Rushwa akijikita kwa kuwekeza zaidi kwenye nishati ya Umeme ambayo itachangia uzalishaji mali kwa kasi zaidi, Mifano iliyo wazi kupitia REA ambayo imechangia kusambaza umeme vijijini kwa upana mkubwa.

Kazi ya ujenzi wa barabara, Licha ya kuwa Jk amejitahidi kwa asilimia 65% na amefanya kwa kiwango cha juu na anastahili pongezi kwa barabara nzuri za kiwango cha Lami zenye kupitika, mh Ngelejah anatamani kuona asilimia 100% ya barabara zote zimekamilika miradi yote na barabara zijengwe imara zenye kudumu, hili linawezekana Kama tutakuwa na mfuatiliaji makini ambaye ni Mh Willium Mganga Ngeleja.

Kitu kinachompa nafasi mh Ngeleja ni uwezo wake mkubwa katika ujenzi wa siasa unganishi isiyo na makundi ndani ya wananchi na vyama vyao vya siasa, akiwa mwenye nia njema, mh.Ngeleja anapenda kuyaunganisha Makundi yote na wananchi waote licha ya utofauti wa rika zao katika jamii ili kujenga nchi na kuondoa ubaguzi.

Halikadhalika mh Ngeleja amejitosa kulipambania swala la kuondolewa kwa vikwazo kwa wafanyabiashara na wakulima wadogo wadogo kwa kuwatoza kodi kubwa ukilinganisha na gharama za uzalishaji hali inayopelekea kuwanyonya wakulima wa hali ya chini pamoja na wafanya biashara wadogo wadogo, wakishindwa kulipa ada ya watoto shuleni ,"Lazima tuyalinde masoko ya ndani ili kuweza kumnufaisha mkulima wa hali ya chini kufaidi jasho lake" mh Ngelejah aliyasema hayo wakati akizungumza na wakulima wa mananasi wilayani Sengerema kata ya Nyampulikano ...katika kuwanufaisha wakulima katika masoko ya ndani.

Kuboresha Afya, hili limekuwa changamoto kubwa kwa Kila kiongozi anayetoka madarakani,mh ndiye mtu pekee atakayewezesha kutumiaa rasilimali zetu kunufaisha wananchi wote kwa ujumla na sio Tu wawekezaji wanufaike na Rasilimali za nchi yao kwa kuwekeza kwenye sector ya Afya katika Hospital ,madawa na maabara yenye vifaa vya kisasa na vyakutosha Hilo linawezekana.

Eneo lingine analitazama kwa jicho la Karibu Ni katika sekta yenye kuchukuaa pesa nyingi kutoka serikalini japokuwa serikali bado haijafikiria kuzuia ulipaji wa ada kwenye sekta ya elimu, Mh ngeleja anajitahidi kuona Ni jinsi gani ELIMU itakavyoweza kutolewa bure na kwa ufanisi mkubwa hasa katika maeneo ya vijijini ambako kumekuwa na ushukaji wa kiwango cha uandikishwaji wa watoto kwa ajili ya Elimu ya Awali kwa kiwango kikubwa kutokana na umaskini.

Vipaumbele vya Taifa, Hapa Mh Ngeleja anatazama kwa umakini mkubwa, kwani anatambua kuwa ili tuendelee Lazima mahitaji yote yatolewe kwa usawa kuliko kuzidisha matumizi ya serikali kwa kununulia mashangingi ya wizara Huku wananchi wakiendelea kutaabika .

Mwisho,nafasi Hii kwa mh Ngeleja ni muhimu sana hasa tukizingatia uwezo wake mkubwa kifikra na kiutendaji. Tanzania Ni nchi yenye amani hivyo mh. Ngeleja anatumaini Kuiona zanzibar ikiendelea kuwa huru katika mipaka yake huru ndani ya Tanzania ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania Bara na visiwani kwani sote Ni ndugu wa asili kabisa ,tunategemeana kizazi hadi kizazi hakuna anayefurahi Leo tukivunjika, hivyo Ni Vyema kuzingatia taratibu za muungano wetu.


SHIME TANZANIA ,NGELEJA TISHIO NA ATOSHA 2015 TANZANIA....
 
Mhe. Ngeleja hafai hata kupewa kuongoza hata Kijiji. Mtu anapewa vijisenti Mhe. mzima na hana hata aibu. Kila kitu kwake ni DOHO TABU.
 
Mleta mada nafikiri Tanzania haiwezi kungozwa na mtu mwenye weledi mmoja tu kwemnye eneo moja tu la madini kamaulivyoeleza, tena kwenye madini ya vito ( Tanzanite) wakati unamwagia sifa kwa kutoa hati ya uasili, je? umejishughulisha kidogo kwa kujiuliza pamoja na hizo hati za uasili bado India na Kenya ndio zimeuza Tanzanite nyingi kwenye soko la kimatifa kwa mwaka 2012/2013?

Na kama umeamua kumpigia chapuo Bwna Ngeleja, Jeumeweza kujiuliaza kwa nini akiwa pale Wizarani alifumbia macho kinachoitwa garama za uendeshaji (capacity charge) za IPTL,pamojamojana bei ya mafuta mazito kuendesheamimbo hiyo wakati huo?

Jipan upya umlete huyu tu hapa kiwa na sababu zinazotosheleza, taasisi ya urais iataka mtu mwenye zaidi ya hicho ulichotaka kutuaminisha, Asante.
 
Back
Top Bottom