William Mganga Ngeleja anafaa urais 2015

William Mganga Ngeleja anafaa urais 2015

Nakumbuka aliingia ATM akaanza kuongea kwa simu, mlinzi kumuelewesha kwamba watu wengine wana subiri huduma, akamchapa mlinzi kibao...! haya....
 
MH.WILLIUM MGANGA NGELEJA SULUHISHO BORA MADINI

Itakumbukwa kuwa sekta ya nishati na madini ilishawah kukaliwa na nawazir wengi mno wakuwemo kina Mzee Msabaha,Mzee Daniel Yona na wengine wengi tuu,lakini hao wote walikuwa wanaishia kuwa katika wizara hiyo kwa muda wa miaka 2 na nusu na muda mwingine miwili kamili, ni mawazir watatu tuu akiwemo mh.Rais Kikwete pamoja na mh.Willium Mganga Ngeleja ndio waliokaa kwa muda mrefu kulingana na ugumu wa wizara hiyo,Mh.Kikwete alikaa miaka 6 na mh.Willium Mganga Ngeleja alikaaa miaka 5 na miez 8 kitu kinachoonyesha upambanaj mkubwa kwenye wizara hii na mh.Ngeleja, kwaukweli mambo aliyoyafanya yatabaki kuwa msaada mkubwa kwa Tanzania yetu,yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mh.Ngeleja aliyafanya alipokuwa ktk wizara ya Nishat na Madini ikiwa ni kwa muda wa miaka 5 na miez 8,:-

1.Itakumbukwa kuwa Ngeleja ndiye aliyepambana kwa hali na mali mpk kuhskikisha kunapatikana maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo.

2.Itaendelea kukumbukwa kuwa ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa mfuko maalum wa kuwasaidia wadogo nchini kitu ambacho kinazungumzwa na wachimbaji wadogo mpaka leo,na hata juzi nilipokuwa ziarani Geita nilipata kutembelea maeneo ya wachimbaji wadogo na walimtaja Ngeleja kama mkombozi wao,na daima wataendelea kumtukuza kwa anachokifanya kwani anafanya mambo mazur anapokabiziwa majukum ya kijamii.

3.Mwezi April 2010 mh.Ngeleja alipiga marufuku usafirishaji nje ya nchi wa madini ghafi ya Tanzanite yenye ukubwa unaozidi gramu1,kitu ambacho juzi nilivyokuwa nazungumza na baadhi ya mawazir na baadhi ya viongoz wa juu wa chama walikipenda na kusema Ngeleja anafaa kuingia wazir mkuu wa Tanzania au hata Raisi kama akiamua kugombea

4.Mh.Ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa kutoa hati ya uasili(certificate of origin) kwa wanaouza madini ya Tanzanite nje ya nchi ikiwa ni mkakati wa serikali kudhibiti uuzwaji haramu wa madini ya Tanzanite,kitu amabcho hata Prof.Muhongo anajivunia sasa na kipindi fulani hivi ktk ziara yake mererani yanapopatikana madini ya Tanzanite mh.Muhongo alimtaja Ngeleja kama msaada mkubwa katika hilo...

Mwisho
Watanzania tunapaswa kuwasemea watu kwa mabaya yao na mazuri yao yalio mengi kwani hakuna mwanadam aliye kamili,..Ngeleja kafanya mengi sana sekta ya madini na hayo hapo juu ni kwa uchache wake.
Ngeleja anataka kuwa rais wa nini? Maana Tanzania tuna marais wengi mara rais wa TFF, Rais wa Baraza la Michezo Tanzania, Rais wa Akudo,rais wa chama cha ngumi za kulipwa, rais wa riadha, Rais wa Bongo Movies hata Simba juzi wametoa cheo cha mwenyekiti wa club sasa ataitwa rais wa club.Swali langu je Ngeleja nae unataka kuwa rais wa kundi gani kati ya hayo?
 
WASIFU WA MHESHIMIWA WILLIUM MGANGA NGELEJA (THE CURRICULUM VITAE)

Particulars/ Husishi/Moja moja
Jina: WILLIUM
Jina la kati: MGANGA
Jina la mwisho/ukoo: NGELEJA
Tarehe kuzaliwa: 05/10/1967
Wasifu wa ndoa: AMEOA
Anuani: SLP 2000 DAR ES SALAAM
Simu ya kazi: 0754710070

Taaluma yake
2001-2002: CERTIFICATE YA SHERIA YA MAWASILIANO YA MITANDAO YA SIMU WITWATERSRAND UNIVERSITY SOUTH AFRICA
1996-1999: MASTERS IN LAW (LLM)UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
1991-1994: LLB UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
1987-1989: A-LEVEL IHUNGO HIGH SCHOOL
1983-1986: O-LEVEL MPWAPWA SECONDARY SCHOOL
1976-1982: PRIMARY EDUCATION(ELIMU YA MSINGI) BITOTO PRIMARY SCHOOL

Historia ya kazi
2005-2015: MBUNGE BUNGE LA TANZANIA (JIMBO LA SENGEREMA)
1/12/2007-08/02/2008: NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI
Feb 2008-May 2012: WAZIRI NISHATI NA MADINI
2000-2005: MWANASHERIA MKUU VODACOM TANZANIA
1995-2000: MWANASHERIA MKUU PRICE WATERHOUSE COOPERS COMPANY
1994-1995: OFISI YA MWANASHERIA MKUU KWA AJILI YA MAFUNZO YA SHERIA YA NCHI NA UTUMIZI SAMBAMBA NA USIMAMIZI WAKE

Wasifu kisiasa ndani ya chama (CCM)
1980-1981: MWENYEKITI WA VIJANA SHULE YA MSINGI BITOTO
2012-2017: MJUMBE HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

Na huo ndioo wasifu wa mheshimiwa Ngeleja...
 
Unaongelea ubunge au uraisi! Acha kuleta propoganda mfu! Kwa nini alitolewa kwenye baraza la mawaziri!? Amewafanyia nini wana Sengerema na baada ya kutolewa katika baraza la mawaziri ni mchango gani wa maana katoa kwa taifa hata tu kuchangia hoja mbalimbali bungeni?
Nenda kwanza jimboni kwake,ongea na wanasengerema ndo uje na hoja.
 
habari zingine bana, ngoja nipalilie mahindi yangu mie!!!

kenya-farmer-drought.jpg
 
Sasa hapo ndiyo umeonesha uwezo wa kiutendaji au ujuzi wa taaluma aliyosomea. Labda mtuma mada ungejaribu kutuelezea mafanikio na mapungufu yake katika utendaji kazi ingekuwa vizuri zaidi kwa sisi wananchi wa vijijini tuweze kumuelewa huyu Ngereja.
 
Kiutandaji Mbowe kamuacha mbali sana Ngeleja kufanya kazi kwenye chama cha upinzani sio mchezo wewe Gwanco, Ngeleja mpaka kapata uwaziri si kabebwa tu hivi kama nchi ingekua serious Ngeleja ni wa kumpa uwaziri?
 
Tanzania UMEME UTAKUWA NI HISTORIA. By Ngeleja
Kweli Urais Umekuwa Ni Urahisi.
UMELIPWA SH NGAPI KUMPIGIA DEBE?
 
Mbona haonekani kwenda 'school of law'!?
Academically yuko vizuri sana lakini morally inatia mashaka maana anaonekana kufanya kazi na taasisi kama mbili ambazo kipaumbele chake ni kufilisi nchi, japo alianzia PRICE WATERHOUSE COOPERS COMPANY ambako kimaadili wako juu kabla ya 'kujichafua'.
 
Kwa wabongo academic sio kipimo sahihi kwa Ngeleja tutampima kwa utendaji wake kwakuwa alishapata fursa ya kutuonyesha alichonacho kama mtendaji
 
Back
Top Bottom