William Mganga Ngeleja anafaa urais 2015

William Mganga Ngeleja anafaa urais 2015

Joined
Oct 9, 2014
Posts
95
Reaction score
13
MH.WILLIUM MGANGA NGELEJA SULUHISHO BORA MADINI

Itakumbukwa kuwa sekta ya nishati na madini ilishawah kukaliwa na nawazir wengi mno wakuwemo kina Mzee Msabaha,Mzee Daniel Yona na wengine wengi tuu,lakini hao wote walikuwa wanaishia kuwa katika wizara hiyo kwa muda wa miaka 2 na nusu na muda mwingine miwili kamili, ni mawazir watatu tuu akiwemo mh.Rais Kikwete pamoja na mh.Willium Mganga Ngeleja ndio waliokaa kwa muda mrefu kulingana na ugumu wa wizara hiyo,Mh.Kikwete alikaa miaka 6 na mh.Willium Mganga Ngeleja alikaaa miaka 5 na miez 8 kitu kinachoonyesha upambanaj mkubwa kwenye wizara hii na mh.Ngeleja, kwaukweli mambo aliyoyafanya yatabaki kuwa msaada mkubwa kwa Tanzania yetu,yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mh.Ngeleja aliyafanya alipokuwa ktk wizara ya Nishat na Madini ikiwa ni kwa muda wa miaka 5 na miez 8,:-

1.Itakumbukwa kuwa Ngeleja ndiye aliyepambana kwa hali na mali mpk kuhskikisha kunapatikana maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo.

2.Itaendelea kukumbukwa kuwa ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa mfuko maalum wa kuwasaidia wadogo nchini kitu ambacho kinazungumzwa na wachimbaji wadogo mpaka leo,na hata juzi nilipokuwa ziarani Geita nilipata kutembelea maeneo ya wachimbaji wadogo na walimtaja Ngeleja kama mkombozi wao,na daima wataendelea kumtukuza kwa anachokifanya kwani anafanya mambo mazur anapokabiziwa majukum ya kijamii.

3.Mwezi April 2010 mh.Ngeleja alipiga marufuku usafirishaji nje ya nchi wa madini ghafi ya Tanzanite yenye ukubwa unaozidi gramu1,kitu ambacho juzi nilivyokuwa nazungumza na baadhi ya mawazir na baadhi ya viongoz wa juu wa chama walikipenda na kusema Ngeleja anafaa kuingia wazir mkuu wa Tanzania au hata Raisi kama akiamua kugombea

4.Mh.Ngeleja ndie muasisi wa utaratibu wa kutoa hati ya uasili(certificate of origin) kwa wanaouza madini ya Tanzanite nje ya nchi ikiwa ni mkakati wa serikali kudhibiti uuzwaji haramu wa madini ya Tanzanite,kitu amabcho hata Prof.Muhongo anajivunia sasa na kipindi fulani hivi ktk ziara yake mererani yanapopatikana madini ya Tanzanite mh.Muhongo alimtaja Ngeleja kama msaada mkubwa katika hilo...

Mwisho
Watanzania tunapaswa kuwasemea watu kwa mabaya yao na mazuri yao yalio mengi kwani hakuna mwanadam aliye kamili,..Ngeleja kafanya mengi sana sekta ya madini na hayo hapo juu ni kwa uchache wake.
 
Ni mapema sana kutabiri, CCM wako smart sana katika hilo na huwezi kuwatabiria hilo
 
Unanikumbusha umeme wa Ngeleja ulivyo mwaibisha Kikwete wakati akihutubia uwanja wataifa umeme ukakatika gafla, naona magamba baada ya gamba kukatalia kiunoni mmehamua kulivaa tena. CCM chama cha mapuuzi ni janga.
 
Sijui unatumia ninii kinachokufanya uuite umeme wa Ngeleja,lakini itakumbukwa awamu ya Ngeleja tabu ya umeme kukatika ndipo ilipoanza kupungua,huyu Jamaa ni mzuri sana tukianzia taaluma yake na namna anavyoendesha mambo yake kwa fikra pevu, mi nakubaliana na CCM kumuandaa kuwa raisi 2015
 
Mkuu kajipange upya, hamna point yamaana hapo, yani kupambana na kupata maeneo zaidi kwaajili ya wachimbaji wadogo ndio jambo kubwa katika wizara? Inamaana mikataba mibovu hakuiona ambayo inaliingizia taifa hasara. 5 years wizarani ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake!!!
 
Kwani hakuwa analipwa mishahara? Umeandika kana kwamba alikuwa anajitolea kutusaidia watanzania kumbe aliajiriwa na ufisadi mwingi kaufanya. Hebu tueleze alipata wapi hela za kununua yale Malori 200 yameandikwa Sengerema pamoja kujenga hoteli ya ghorofa kumi Mtaa wa Rufiji Mwanza kwa jina la Pigeon Hotel aka Njiwa Pori
 

Naona jamaa umeingia na mzuka wa hatari maana huu uzi wa pili sasa wenye issue ileile.

Any ways kama ana mtandao butu usiokuwa na mikakati mathubuti then he has a long way to go no matter ni mchapakazi ama mwadilifu wa kiwango kipi.

Hiyo ndo CCM.
 
Vipi kuhusu UMEME, alifanya nini? Aliingia mgao ulikuwa masaa nane akaondoka mgao masaa 16. Leo sasa ndio nimeelewa kumbe anaweza vitu rahisi rahisi kama hivyo vilivyotajwa lakini issues ngumu kama umeme hakuna kitu. Aliishia kutaja megawati tu.
 
Back
Top Bottom