William Malecela: Watoto wa viongozi na uongozi wa taifa letu!

Mkuu kutetea ni pamoja na kusema kauli tata ya katibu wa ccm sio issue bali mkulu! Hizi ni propaganda mkuu,ulipaswa kushangaa na kuuliza hilo gamba basi ni nini? Lakini hujakosoa huo mkanganyiko wazi bali ukaamua kuwaaminisha watu pale unapoamini! Je chama ni mwenyekiti? Kama sio what is going on there? Wewe ni kizazi tena damu yetu usifungwe na mbinu hizi zinazoshindwa za ccm.ukitaka ueleweke kuwa muwazi na mkweli tu.werevu wengi wanapita humu usipindishe mambo kwa personal benefit mkuu.
 

- Zed mambo mengine ni facts of life kwamba hata wewe ukiwa waziri siamini kwamba utataka watoto wako wasome bongo, wakati unao uwezo wa kuwasomesha nje kwenye elimu bora zaidi. Kosa kubwa Tanzania tunashindwa kuelewa ni kwamba majuu wana system ambazo zinampa kila mwanandamu ku-explore potential zake kielimu, hakuna binadam ameumbwa bila talent hata moja, kwa hiyo mtoto ambaye baba yake ni kiongozi anafanya vibaya shule za chini hapa bongo, akienda majuu kule anatihaniwa na kuangaliwa wapi anafaaa na kuepelkwa huko, sasa talent yake ikiwa full explored automatically anaanza ku-perform kuliko hata his imaginations, sasa akirudi bongo tunashangaa aaghhh huyu darasani alikuwa zero, hapana ndio tofauti yetu bongo na majuu!

- Kuhusu Makongoro wengi inaelekea hamumjui vizuri, mimi ninakumbuka Marehemu baba yake akimcheka kwamba he would never raise to anything in politics na yeye akimjibu kwamba ni kwa sababu ya kuwa mtoto wake ndio maana atakapata sana shida ku-raise above his name, lakini aliposhinda ubunge wa upinzani, Mwalimu was the first one kumpa pongezi tena nakumbuka sana akumuita "Mheshimiwa Mbunge", na Makongoro kwenye kampeni alimshambulia sana Mwalimu kwamba amemrithisha urais mkapa, kwa hiyo kampeni za uchaguzi zilikuwa ni waste of time and money za taifa.

- Lakini then came the political charges kwamba wapinzani wanamtumia tu Makongoro, soon watamtupa which they did, sasa unaona matatizo ya mtoto wa kiongozi anapoamua kuwa kiongozi upinzani, sasa amerudi CCM he seems to make a lot of sense, lakini bado kuna mtoto wa baba wa taifa kutoka mostly wapinzani, let the man be himself as he is badala ya hizi title zisizo na faida kwake as a man na mwananchi,

- Watoto wa viongozi waruhusiwe kuwa wananchi, wanapofanya mazuri na wanapofanya mabaya pia!


William @ NYC, USA.
 
Kwamba wana haki ya kushiriki hilo ni kweli.Lakini hilo haliondoi ukweli kwamba kuna upendendeleo.Haki ni haki lakini haipatikani bure mara pengi hupiganiwa.Ninaamini kwenye process ya watoto hao na viongozi kuipigania ama kuipreserve haki hiyo,basi nepotism hutokea.
 

- Mkuu Mushi iweke hii kikatiba ya Jamhuri yetu, itasomeka vipi mkuu wangu?

William @ NYC, USA.
 

Nakuunga mkono kwenye red if you mean what you mean....nimesoma baadhi ya post wako wanaokuzungumzia vizuri kama fighter, no more to add kwa kuwa sikufahamu.....hatuna uwezo wa kupima nia ila utakuwa kapu moja na wengine kama utakuwa uko-driven na factors zinazowa-drive watoto wengine wa vigogo "kushiriki keki tuliyoizoea"

By the way, what is your opinion in a more general term kwa kuwaangalia watoto wenzako wa viongozi wengine? Are they like you? Maana hapa hatuzungumzii Willy tu, ila general as a system kwa watoto wa vigogo
 
Kwa mtizamo wangu tatizo ni kubwa zaidi kuliko maelezo; katika miaka ya hivi karibu uongozi wa juu umechukuliwa na watu ambao maisha yao yote ya utumishi wa umma yamekua kwenye siasa.

Inavyoelekea watu aina hiyo wanachukulia siasa kuwa ni ulaghai, kwa maana kwamba wanachukulia siasa kuwa ni tathmilia inayolenga kuchota akili za umma bila ya kuwa na mahudhui yeyote. Na hivyo unaweza ukaanzisha mjadala wa chama kujivua gamba, ukawaacha wananchi waogelea, kila mtu anajaribu kuwa bigwa wa kutoa tafsiri ya nini hasa maana halisi ya kujivua gamba.

Kwa kuwa hawa watoto wa wakubwa wamekulia kwenye utamaduni huo, itakuwa ni balaa kwa nchi yetu kuendelkeza mfumo wa kuridhishana madaraka.
 

William hongera sana kwa kujisomesha mwenyewe angalau umeweza kuokoa pesa za wakulima, lakini hilo pekee halikufanyi wewe uwe tofauti na watoto wa viongozi wengine wanaofuja mali za Taifa. Nitakubaliana na wewe iwapo utasema hadharani kukana matendo machafu ya viongozi wa CCM akiwamo Raisi, kukana maovu aliyoyafanya Mzee Malecele (hatuna haja ya kuyadili). Siku zote unaleta pointi lakini unakwepa ukweli.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Ni mara chache sana watu waliokuwa na priveledge kama hizo i.e kuwa watoto wa viongozi, kuwa na uelewa wa matatizo halisi ya mtanzania.Kama baba zao wenyewe hawajui kwanini sisi ni masikini,unategemea watoto waje na jibu gani?Sana sana ni kujijenga na kujiimarisha kuyalinda madaraka na hizo priveledges by any means neccessary.Vibaraka wenye kunufaika wanao kibao pia.
 

Kweli mkuuu umetusaidia kupanua huu mjadala...Yaani hali hii inazidisha simanzi tukiwaona wale watoto wa wakubwa waliokuwa vilaza, wakiambulia makarai (C), make ups, supplimentary exams na vitu kama hivyo kwamba leo ndio watunga sera wa nchi hii au wale wanaosimamia uchumi wa nchi yetu pale BOT.


Inakera sana!
 
nyie mnaojiita watoto wa viongozi mna dhambi ya dhuluma, mmelelewa na hela za dhuluma, mmebeba dhambi ya dhuluma!!

Baba zenu waliiba hela zetu kuwasomesha,tatizo letu tunaogopa mtaileta ile dhambi kwenye utawala ambao tunataka kuusimamia!
 


Kaka mimi hawa waupinzani naweza kuwasamehe kwa kuwa siasa za upinzani ningumu sana na zinaitaji muamko na kujitolea kwa nguvu zoite, tumeshuhudia watu wengi wakiogopa kuingia upinzani kwa kuwa wanaogopa CCM itawafanya mbaya kwenye biashara zao na maisha yao ya kila siku,
Ila ukweli ni kwamba ni rahisi kwa watu waliojitolea na kujenga majinakwenye upinzani kushawishi ndugu zao na watu wakaribu kuliko watu wasio wajua, Atleat sikuhizi kuna muamko!

kwahiyo kuwalaumu UPINZANI kwa hili ni kuwaonea kwani mazingira ndio yansababisha haya yote!

Ila kwa CCM hilo halisameheki tunaona watu wasio na uwezo wanavyobebwa na kuachwa vijana wenye huwezo mkubwa sana tena kupita hata WAZAZI hao wano wabeba watoto wao!

Ni kwa nini nyerere hakufanya hivi?
Ni kwanini Sokoine hakufanay hivi?
Ni kwa nini .......... hakufanay hivi? Hope tunamkumbuka alifariki hukokusini kwa ajali ya helikopter!
 
willy rudi bongo uone watu wa ngara n.k wanavyoishi! Nafikiri utajua kwanini tuna machungu na watu wanaofanya mizaha na shida zetu kwa maslahi yao
 
Hili ni jambo tata sana na si rahisi tu kusema kuna upendeleo au hakuna, tutumie busara tu kujadiliana bila kutoa hukumu.
Mkuu William kuna mambo ambayo ni magumu kuyatolea ushahidi wa moja kwa moja lakini ushahidi wa kumazingira unaonyoshe ingawa haujitoshelezi kama ushahidi kamili. Nakubaliana nawe kuwa watoto wa viongozi wana haki sawa kama wengine, na wanstahili fursa sawa.

Nafasi hasa za kisiasa zinatia shaka kwani wazazi viongozi huwa na 'influency na network nzuri' kwahiyo ni rahisi kwao ku- manipulate system in favor of their interest. Mtoto wa kiongozi akiwa mbunge wa kuchaguliwa haina shida, lakini kama kwa mfano wapo watoto 10 au 15 wa nafasi za kuteuliwa inatia shaka.

Mkuu hivi inakuwaaje kwa mfano mahali kama BoT kuwe na watoto wa viongozi tupu!
Inawezekana kabisa watoto hao wana sifa nzuri sana kutokana na ubora wa elimu na maarifa yao. Wasi wasi unaletwa na baba zao (viongozi) ambao wamekuwa si wa wazi. Kelele za BoT ziliposikika wakatafutwa watoto wawili watatu na kutolewa kafara. Gavana akaunda tume kuchunguza hao waliobaki, jambo la kushangaza ni kuwa hakuna taarifa yoyote ya kuwatuhumu au kuwasafisha iliyotolewa. Hapa ndipo watu wanabaki wakijuiuliza kuna nini kinafichwa? na ni kwa sababu hizo wanaendelea kuamini kuwa ipo namna.

Kwa vile utaratibu wa kupata viongozi wa nyanja zote si wa wazi, inakuwa ngumu sana kwa baadhi ya watu kuamini haki inatendeka.
Mfano mzuri upo ndani ya Chama chako cha CCM, mara tunaambiwa Bashe si raia anaenguliwa kugombea ubunge, waziri anajitokeza na kusema ni raia baada ya mchujo,je huu si ushahidi wa kimazingira kuwa hila zilitumika? Ukiangalia issue nzima unaona ina influency ya viongozi, sasa katika mazingira haya utawezaje kukataa kuwa ushawishi wa viongozi wazazi au walezi si sehemu muhimu kwa mafanikio ya watoto wao?

Nasema haki itendeke lakini si tu itendeke bali ionekane inatendeka kwa watoto wa viongozi na watoto wengine, kwa mfumo wetu usio na uwazi na uliojaa rushwa dhana hii itabaki vichwani mwa watu, na wala asidhani mtu kuwa ni suala la wivu na husuda.
 
Ridhiwani wakati wa kampeni 2010 alipita Jimboni kwangu! Alimwahidi kijana mmoja ukuu wa Wilaya......nilicheka sana nilipoipata hiyo. Yule dogo alikuwa anapewa Hadi ripoti za maendeleo ya Wilaya as if naye ni kiongozi wa nchi.....sababu ya Jina Kikwete....
 
Hivi hizo ndiyo nini? Manake nimekuwa nikizisoma soma tu humu bila hata kuelewa ni vitu gani.

Pole mkuu na pia hongera..Inaonekana hukuwahi kukutana na vitisho vya Ma-Prof wa bongo..

Hiyo ni mitihani ambayo wanapewa watu walioshindwa mtihani wa kwanza (first sitting) katika vyuo vikuu vya hapa Bongo. Pia inaweza kuchukuliwa kama special exam endapo mtu huyo atakuwa hakuwahi kufanya mtihani wa kwanza kwa sababu za msingi zilizomfanya auhairishe. Mara nyingi watu wanaoenda kwa kuchechemea (vilaza) walikuwa wanaokoka kwa kufanya hiyo mitihani ingawa kama ni Sup exam huwezi kupewa pass mark zaidi ya C!!!

Karibu Bongo Dar mkuu!!
 

Ndiye Rais wenu huyo baada ya Hussein Mwinyi
 
Mbona kwenye awamu ya kwanza watoto wa wakubwa hawakuwa wengi kwenye siasa kama sasa?. Inakera sana...ial yana mwisho!!
Dark City, Enzi za Mwalimu, uongozi ulikuwa ni kwa vito tena kwa kujitolea. Sasa uongozi wa kisiasa ni professional ambayo ni ajira rasmi tena ndio the top most paying job motive ikiwa not to lead but to gain, reap and sometimes rob!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…