William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
by William Malecela on Saturday, May 14, 2011
Ni lazima tukubaliane kwanza kwamba watoto wa viongozi wa Tanzania ambao wengi wameanza kuingia kwenye siasa na kushika nafasi mbalimbali wana haki kabisa ya kushika nafasi yoyote ya uongozi wa taifa kama Watanzania wengine. Haki yao ya Kikatiba kuchaguliwa au kushiriki nafasi yoyote ya kisiasa kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo haifutwi au kuondolewa kwa sababu ya nafasi za baba zao kwa taifa letu, sasa au huko nyuma.
-Tatizo kubwa ambalo lipo au niseme mawili ni kwamba kuna hisia kuwa watoto hao wanapewa nafasi hizo si kwa sababu ya kustahili wao wenyewe bali kwa sababu ya kubebwa au kutengenezewa mazingira ya kushika nafasi mbali mbali kwa sababu ya wazazi wao. Hili tumejionea likitokea kwa vyama vyote vya siasa nchini, yaani watoto na ndugu wa viongozi wakishiriki kwenye uongozi pia!
- Na pili, endapo wanashika nafasi ambazo zinahusiana na masuala ya utawala na sheria itakuwa vigumu sana kwa watoto hao kutengua au kuchukua hatu ambazo zitawaonesha kuwa wanafumua mambo yaliyoyofanywa na wazazi wao au hata kushindwa kuchukua hatua mbalimbali kwa sababu ya wazazi wao.
- Hivyo, hisia za haya mawili zinawafanya wananchi wengi kuona kuwa katika nafasi kadha wa kadha hasa za kisiasa ni vigumu sana kwa watoto kuwawajibisha wazazi wao - aidha kwa kusahihisha makosa yao au kuwachukulia hatua kama inapasa. Jambo la msingi ni kuweka msingi na utaratibu kuwa kila Mtanzania anapata nafasi ya kulitumikia taifa lake kwa kustahili kwake yeye mwenyewe na si upendeleo (uwe wa kidugu, kidini, kikabila, rangi au ushawishi).
- Na pale inapotokea kuwepo ushahidi wa upendeleo kutokana na nafasi za baba zao basi wananchi tujitokeze na kusema wazi palipopindishwa sheria, lakini sio kulalama tu bila sababu za msingi na hasa wivu, maana ni haki yao pia kushiriki taifa bila kuvunja sheria.
Ahsanteni.
William Malecela.