William Lukuvi kumrithi Mizengo Pinda

William Lukuvi kumrithi Mizengo Pinda

Abel 2015

Senior Member
Joined
Sep 5, 2015
Posts
112
Reaction score
55
Mnakumbuka kipindi Magufuli alipopita top 3 kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea urais CCM? William Lukuvi alikua mpambe wake kipindi Magufuli akiasalimiana na wajumbe na hakutaka kumuacha kwani walikua bega kwa bega.

Katika watu walio karibu na Magufuli na ambao Magufuli anaowakubali Lukuvi ni mmoja wapo, na kuna kila dalili JP Magufuli akishinda atamteua yeye kuwa PM.

By Abel sere from Moshi.
 
MNAKUMBUKA KIPINDI MAGUFULI ALIPOPITA TOP 3 KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA KUMTAFUTA MGOMBEA URAIS CCM? WILLIAM LUKUVI ALIKUA MPAMBE WAKE KIPINDI MAGUFULI AKIASALIMIANA NA WAJUMBE NA HAKUTAKA KUMUACHA KWANI WALIKUA BEGA KWA BEGA.KATIKA WATU WALIO KARIBU NA MAGUFULI NA ANBAO MAGUFULI ANAOWAKUBALI LUKUVI NI MMOJA WAPO. NA KUNA KILA DALILI JP MAGUFULI AKISHINDA ATAMTEUA YEYE KUA PM.
By Abel sere from Moshi

Thubutuuu kwa uchaguzi upi? labda wa 2025 siyo huu dogo ,2015 ni LOWASSA tu na UKAWA upo hapo
 
Wabunge gani ambao watampigia kura bungeni kuidhinisha uwaziri mkuu wake?? Forget that!!
 
Lukuvi ni JEMBE. Ni mtu wa kazi. Magufuli ni mtu wa kazi. Ukijumulisha hapo unapata mchaka mchaka wa maendeleo
 
Yaani Lukuvi awe PM...!!!

Kama JK aliweza kuwa Rais atashindwa Lukuvi? kama mtu kama Magufuli ambaye thinking yake inaonekana ni hafifu sana amepewa agombee Urais atashindwa Lukuvi?

Ndo maana nilikubaliana na kauli ya Sumaye kuwa TZ inahitaji kuwa na vyama vikubwa mbadala hii ya CCM tuu inaleta madhara kama hayo...
 
Sio siri CCM imejisahau mkuu...

Kama JK aliweza kuwa Rais atashindwa Lukuvi? kama mtu kama Magufuli ambaye thinking yake inaonekana ni hafifu sana amepewa agombee Urais atashindwa Lukuvi?

Ndo maana nilikubaliana na kauli ya Sumaye kuwa TZ inahitaji kuwa na vyama vikubwa mbadala hii ya CCM tuu inaleta madhara kama hayo...
 
Uko isimani jimboni hali tete

Wala Lukuvi ata ahangaiki na kampeni ndio maana unamuona yupo busy na migogoro ya ardhi mikoa mbalimbali, kwenye ubunge Ismani Lukuvi hana upinzani, ni suala la kukamilisha ratiba tu.
 
MNAKUMBUKA KIPINDI MAGUFULI ALIPOPITA TOP 3 KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA KUMTAFUTA MGOMBEA URAIS CCM? WILLIAM LUKUVI ALIKUA MPAMBE WAKE KIPINDI MAGUFULI AKIASALIMIANA NA WAJUMBE NA HAKUTAKA KUMUACHA KWANI WALIKUA BEGA KWA BEGA.KATIKA WATU WALIO KARIBU NA MAGUFULI NA ANBAO MAGUFULI ANAOWAKUBALI LUKUVI NI MMOJA WAPO. NA KUNA KILA DALILI JP MAGUFULI AKISHINDA ATAMTEUA YEYE KUA PM.
By Abel sere from Moshi

Wapi tena? Libya au Kuwait?

Hawana nafasi tena Tanzania hao!.

Ccm out!
 
Kiukweli Lukuvi anastahili kuwa waziri mkuu. Nchi itaendeshwa kwa uadilifu na uwajibikaji mkubwa sana. Pia anauzoefu.
Lowassa HAWEZI mteua mtu wa darasa la 7 awe PM,kikubwa zaidi Lukuvi SIO UKAWA
Pia Lukuvi kumshinda kijana Sosopi kule Isimani asali sana maana ana hali mbaya
 
Wala Lukuvi ata ahangaiki na kampeni ndio maana unamuona yupo busy na migogoro ya ardhi mikoa mbalimbali, kwenye ubunge Ismani Lukuvi hana upinzani, ni suala la kukamilisha ratiba tu.
Nenda Isimani kabla hujatoa hitimisho!Lukuvi ana hali mbaya zaidi y uchaguzi wowote alio wahi kushiriki!Kupanga na MAMA Abwao kama ajiondoe Isimani ili wasigawane kura CCM A na CCM B(ACT-Wazalendo)hakujawasaidia
 
Kama JK aliweza kuwa Rais atashindwa Lukuvi? kama mtu kama Magufuli ambaye thinking yake inaonekana ni hafifu sana amepewa agombee Urais atashindwa Lukuvi?

Ndo maana nilikubaliana na kauli ya Sumaye kuwa TZ inahitaji kuwa na vyama vikubwa mbadala hii ya CCM tuu inaleta madhara kama hayo...

Huyo suma mwenyewe elimu yake unaijua lakini?
 
Kama JK aliweza kuwa Rais atashindwa Lukuvi? kama mtu kama Magufuli ambaye thinking yake inaonekana ni hafifu sana amepewa agombee Urais atashindwa Lukuvi?

Ndo maana nilikubaliana na kauli ya Sumaye kuwa TZ inahitaji kuwa na vyama vikubwa mbadala hii ya CCM tuu inaleta madhara kama hayo...

Hakuna mwana MAHESABU na mwana SAYANSI mwenye low thinking capacity.Wewe utakuwa wale wa Qt au form four Arts Pure,mara zote akilı zenu zınawaza NAHAU na miaka ya vifo vya machıfu.
 
Back
Top Bottom