Mizengo Pinda: Natamani Katiba ya Tanzania ibadilishwe, ili Rais Magufuli aongezewe muda zaidi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema isingekuwa katiba ipo “tight” kidogo, basi angetamani kuona Rais Magufuli akiongeza miaka mingine mitano baada ya muda wake kuisha.

"Ni kwakuwa tu katiba zenyewe kidogo ziko taiti lakini kama si kwa sababu hiyo, Walahi ningesema mzee piga mingine mitano tu''

Pia Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu ameongeza kuwa:

“Ni matumaini yetu kwamba katika kipindi hiki hata kama utatugomea kabisa kuongeza kidogo, lakini utahakikisha basi umetupa kiongozi mwingine mzuri kwa kusaidiana na NEC, atakayeweza kusukuma mawazo haya na maamuzi haya magumu ambayo unayafanya”

Mzee Pinda ametoa kauli hiyo leo hii wakati wa Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyofunguliwa na Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, inayofanyika Jijini Mwanza.

 
Pamoja na kwamba sikipendi chama cha kijani, lakini huyu mzee Kayanda Peter Pinda ni mmoja ya wazee wachache wanao jielewa na kusimamia kile wanacho kiamini.

Mzee huwa namtazama akiongea hutoa kile ambacho yeye binafsi anakiamini, tena pasipo na tashwishwi husema jambo bila kushinikizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FB_IMG_1576146216334.jpg
 
Back
Top Bottom