Espy_
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 91,950
- 183,442
Sasa tunaenda sawa, sifa ya kwanza ya mwanaume ni kuwa "provider". Then mambo mengine yanafuata, hivyo si kwamba ukiwa na kazi basi umemaliza bali kuna mengine ya muhimu yanaambatana na hilo.Adam aliumbiwa Hawa kama msaidizi wa kufanana naye na hii haimanishi kwamba Adam alitakiwa kufanya kila kitu kwasababu tu Hawa ni msaidizi.
Unataka kusema kuwa “mume” ni kuwa na kazi/pesa? Kwamba yeyote mwenye kazi/pesa tayari ana sifa za kuwa “ mume”? Kama hii ndio sifa ya kuwa mume babu/baba zetu wasingeoa hakika na pengine tusingekuwepo duniani.
Mke akinihudumia kwa kila kitu sio mbaya ndiyo maana halisi ya ndoa inapojidhihirisha (kwenye shida na raha). Au mwenzangu unaitafsiri vipi ndoa? Kwamba ni mwanaume tu ndiye anayetakiwa kumhudumia mke kwa kila kitu?
Kuhusu mahari haina shida mwanaume yeyote anayeamua “kuoa” mahari atapambana kwa namna yeyote aipate regardless ni jobless.
Nashukuru kwa kukubali mafanikio ya mwanaume yeyote yule huchagizwa na mama yake.
Babu zetu hawakuoa ilimradi wanaoa, walioa kwasababu walikuwa wapo "tayari" kuoa. Huo utayari ni jambo pana sana ndio na hiyo "kazi" inaingia hapo.
Kama ambavyo unapambana kwa hali na mali ili uweze kupata mahari basi upambane pia uwe na kazi ndio uoe. Maana mahari ni part ndogo mno ya responsibility ya mume katika ndoa.