Wilfred Lwakatare arejea CUF baada ya kufutwa uanachama CHADEMA. Kutumika kuiangamiza CHADEMA

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Shamrashamra zimeshaanza hapa Manzese tawi la Kosovo. Inasemekana Mh Lwakatare yuko maeneo ya Kibaha kwa sasa.

Watu wako kwenye ari kubwa sana.

===


CUF yaeleza itakavyomtumia Lwakatare kuiangamiza Chadema


CHAMA cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania kimesema, kitamtumia Wilfred Lwakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini, kuvimaliza vyama vya upinzani, hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.

Hayo amesema Maftah Nachuma, Makamu Mwenyekiti wa CUF Bara, leo Jumamosi tarehe 30 Mei 2020, wakati anamkaribisha Lwakatare, katika Ofisi za chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Lwakatare mbunge kupitia Chadema amerejea CUF, baada ya kuvuliwa uanachama wa Chadema hivi karibuni, kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Chadema iliamua kumfukuza Lwakatare, baada ya mbunge huyo kukaidi maagizo ya kutohudhuria vikao vya bunge kwa muda wa siku 14, kuanzia Mei 3 hadi 17, 2020.

Chadema ilitoa agizo hilo, ili wabunge wake wajiweke karantini, ikiwa ni tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19).

Pamoja na Lwakatare, wengine waliovuliwa uanachama ni David Silinde (Momba), Joseph Selasini (Rombo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini).

Hata hivyo, wabunge hao wote, wamekata rufaa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa wakipinga uamuzi huo wa chama chao.

Katika hafla ya kumpokea Lwakatare, Nachuma amesema aliimaliza CUF katika Kanda ya Ziwa alipohamia Chadema, na kwamba chama chake kitamtumia tena Lwakatare kujiimarisha tena katika kanda hiyo.

“Alipohamia Chadema, Lwakatare alitumaliza kanda ya ziwa. Tunakuomba utakaporudi uvae njuga, kama ulivyosema unaenda kufanya mkutano mkubwa wa kuimaliza Chadema kanda ya ziwa,” amesema Nachuma.

Amesema chama hicho kimezaliwa upya, baada ya kumpokea Lwakatare, ambaye ni mwiba kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), Chadema na ACT-Wazalendo.

“Tulipitia magumu, lakini tulihakikisha waliotaka kukiharibu wanakimbilia vichochoroni. Wadhamini walifanya kazi kubwa kuhakikisha CUF inabaki salama. Lakini leo hii CUF inazaliwa upya baada ya kumpokea Lwakatare ambaye ni mwiba wa CCM, Chadema na ACT-Wazalendo,” amesema

Nachuma ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Mjini amesema, Lwakatare hajarudi CUF kwa ajili ya kupata cheo, bali ameamua kurudi nyumbani kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo.

“Hakuna anayetaka vyeo hapa. Mwenyekiti yupo, viongozi wengine wapo. Cheo gani tena mtu anataka kuchukua hapa? Mpaka wakati ufike mtu anahaki ya kutaka cheo chochote. Hawa wamekuja kufuata itikadi ya vyama. Kupambana na vyama manyang’au, kuondoa CCM madaralani na Chadema kwenye majimbo yote, na ACT-Wazalendo wasipate kabisa,” amesema Nachuma.


Nachuma amesema kuwa, mkakati wa CUF kwa sasa ni kuhakikisha vyama vya upinzani vinashinda uchaguzi huo, hasa wa majimbo katika jiji la Dar es Salaam.

Awali, Mohamed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari CUF, ameeleza namna chama hicho kilivyomshawishi Lwakatare, kurejea nyumbani.

Amesema, CUF kupitia Rukia Kassim, Katibu wa wabunge wa chama hicho, kiliunda kamati maalumu ya kumshawishi mwanasiasa huyo arudi nyumbani.

“Katibu wa wabunge, Rukia Kassim aliunda kamati maalumu ya watu wanne kuandaa mapokezi. Nao kwa pamoja walishirikiana kuhakikisha kila siku wanamkabili kurudi nyumbani na kuacha adha zinazomkabili alikotoka,” amesema Ngulangwa.

Credit: Regina Mkonde

ZAIDI SOMA:
- Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

- Mbunge wa viti maalumu CHADEMA, Sabriana Sungura ahamia CUF
 
Back
Top Bottom