Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,334
Miaka ya 90 hivi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya KAHAMA mkoani Shinyanga wakati huo Bi. Hawa Mchopa, ndiye aliyeonesha ujasiri wakati huo wakuwakomesha waliojiona ndio wababe wa mji. kulikuwa na TANK la mafuta jirani na eneo la kwa Ikombe amabalo kila mkuu wa wilaya aliyefika alishindwa kutoa maamuzi magumu yakulitoa ili barabara ipite, lakini mama huyu alifanikiwa kulitoa TANK hilo, nakumbuka lilikujaga bonge la whinchi likang'oa kama Magufuli kule Mwanza na sheli.
Nakumbuka mama huyu aliihamisha stendi ya mabasi madogo (wakati ule chai maharage) kutoka Stendi kuu na kuipeleka Uwanja wa mpira wa halmashauri na mafundi seremala wote walikusanywa na kuwekwa sehemu moja hukohuko uwanjani ambako tunapenda kuita uwanja wa Taifa, Nakumbuka barabara zilianza kufyekwa nakuonekana nzuri, nakumbuka yule mama Bagaire aliyekuwa Nesi pale hospitali ya wilaya ya kahama pale alipofukuzwa kazi na mama huyu baada ya huyu mkuu wa wilaya kufika hapo hospitalini akiwa na mgonjwa wake, kama kawaida ya manesi akaanza kurusha matusi bila kujua kama huyo anayemchamba ni bosi wake, aliposhituliwa kuwa huyo ni mkuu wa wilaya, tayari mama aliamuru awajibishwe na aliwajibishwa.Namkumbuka mbunge wa wakati ule Mzee Manyambonde na slogan yake ya manyambo...nde,,,,,wananchi tunamalizia......ndeeee, alikuwa na style nzuri ya kutufanya tujihadae bila kujua.
Na mkumbuka mbunge Marehemu Khaga alipoibiwaga gari lake baada tu ya kuwa mbunge, sikumbuki nini kilitokea mpaka kuondolewa ubunge na kesi yake ilikuwa moto sana naa sijui ilikuwa kesi yanini, kwasababu tulikuwa bado watoto kesi tuliyojua imemuondoa bungeni ni gari lake kuibiwa.
Namkumbuka zaidi Manyambonde aliyesema kuna siku kahama itakuwa mkoa, lakini sasa ni ndoto tena. kahama imegawanywa wilaya mbili bukombe na mbogwe na zikapelekwa mkoa mpya wa geita, kunatetesi Ushetu nayo itakuwa wilaya, tulicho ambulia ni kupata halmashauri ya mji wa kahama.
Pamoja na migodi maarufu tuliyonayo ya Buzwagi na Kakola(bulyankulu) lakini vumbi mpaka mlangoni kwa Lembeli na Maige wabunge wetu wa twiga na propaganda.Pamoja na kujaliwa kupata mawaziri kutoka wilaya hii bado hakuna tija kwa maisha Ya Vijana. Mgodi wa buzwagi upo mjini kabisa na ni maeneo tunayoishi binadamu, sisi wazawa na wakazi tunajiuliza hizo kemikali zinamazara au hazina mazara kwetu.KIDONDA KINAWASHA NAKIKUNA TU, jamaani natania tu.....KISANDU 2015