Wilaya ya Kahama (Shinyanga) imebaki yatima

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,318
Miaka ya 90 hivi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya KAHAMA mkoani Shinyanga wakati huo Bi. Hawa Mchopa, ndiye aliyeonesha ujasiri wakati huo wakuwakomesha waliojiona ndio wababe wa mji. kulikuwa na TANK la mafuta jirani na eneo la kwa Ikombe amabalo kila mkuu wa wilaya aliyefika alishindwa kutoa maamuzi magumu yakulitoa ili barabara ipite, lakini mama huyu alifanikiwa kulitoa TANK hilo, nakumbuka lilikujaga bonge la whinchi likang'oa kama Magufuli kule Mwanza na sheli.

Nakumbuka mama huyu aliihamisha stendi ya mabasi madogo (wakati ule chai maharage) kutoka Stendi kuu na kuipeleka Uwanja wa mpira wa halmashauri na mafundi seremala wote walikusanywa na kuwekwa sehemu moja hukohuko uwanjani ambako tunapenda kuita uwanja wa Taifa, Nakumbuka barabara zilianza kufyekwa nakuonekana nzuri, nakumbuka yule mama Bagaire aliyekuwa Nesi pale hospitali ya wilaya ya kahama pale alipofukuzwa kazi na mama huyu baada ya huyu mkuu wa wilaya kufika hapo hospitalini akiwa na mgonjwa wake, kama kawaida ya manesi akaanza kurusha matusi bila kujua kama huyo anayemchamba ni bosi wake, aliposhituliwa kuwa huyo ni mkuu wa wilaya, tayari mama aliamuru awajibishwe na aliwajibishwa.Namkumbuka mbunge wa wakati ule Mzee Manyambonde na slogan yake ya manyambo...nde,,,,,wananchi tunamalizia......ndeeee, alikuwa na style nzuri ya kutufanya tujihadae bila kujua.

Na mkumbuka mbunge Marehemu Khaga alipoibiwaga gari lake baada tu ya kuwa mbunge, sikumbuki nini kilitokea mpaka kuondolewa ubunge na kesi yake ilikuwa moto sana naa sijui ilikuwa kesi yanini, kwasababu tulikuwa bado watoto kesi tuliyojua imemuondoa bungeni ni gari lake kuibiwa.

Namkumbuka zaidi Manyambonde aliyesema kuna siku kahama itakuwa mkoa, lakini sasa ni ndoto tena. kahama imegawanywa wilaya mbili bukombe na mbogwe na zikapelekwa mkoa mpya wa geita, kunatetesi Ushetu nayo itakuwa wilaya, tulicho ambulia ni kupata halmashauri ya mji wa kahama.

Pamoja na migodi maarufu tuliyonayo ya Buzwagi na Kakola(bulyankulu) lakini vumbi mpaka mlangoni kwa Lembeli na Maige wabunge wetu wa twiga na propaganda.Pamoja na kujaliwa kupata mawaziri kutoka wilaya hii bado hakuna tija kwa maisha Ya Vijana. Mgodi wa buzwagi upo mjini kabisa na ni maeneo tunayoishi binadamu, sisi wazawa na wakazi tunajiuliza hizo kemikali zinamazara au hazina mazara kwetu.KIDONDA KINAWASHA NAKIKUNA TU, jamaani natania tu.....KISANDU 2015
 
LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,640
512
Ndo kampeni mkubwa? Hivi uliamua kutoa historia ya Kahama kwa kumkumbuka Mama Hawa Mchopa. Huyu mama hata mimi namkubali kwani aliibadilisha Kahama.
 
PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,348
3,080
Nimeipenda hiyo slogan ya mbunge, it sounds good manyambo ..... ndeeee
 
Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,044
5,046
Ni mawazo potofu sana kuwaza Kahama kuwa mkoa! Maendeleo si mikoa, hata kama ingekuwa 8 kama ya Wakenya! By the way wasalimie wote huko Igomelo, Nyasubi, Nyahanga e.t.c. Ka supermarket ka Ndegesera kale ka vioo bado kapo?
 
Micro E coli

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
938
192

mkuu unaongelea haka ka mjini au kale ka Nyihogo alikokafunga kitambo.
 
Micro E coli

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
938
192
mji umekuwa na maisha magumu huo baada ya wachukua dhahabu bure kuingia hapo bora walipokuwepo wachimbaji wadogowadogo chungwa buku ni balaa wananchi wapo hoi kabisa hapo kahama barabara yao hasa hiyo Isaka road utacheka uzimie lami juu ya changalawe sijapata ona wizi mtupu halimashauli.
 
Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
19,827
15,035

Kamanda KISANDU!!

hamasisha makamanda kufungua matawi...kimya kimya.....likichomoza.....wakukute mlangoni!!!

bageshage makamanda bose mhongolo, maley
bawelage TOLIZA
 
St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,404
3,937
Tatizo kubwa la hiyo halmashauri ni rushwa iliyopitiliza,endapo tatizo hilo litapatiwa tiba basi kuna uwezekano wa kupata maendeleo.Ni aibu kwa Kahama kufikiria kuwa mkoa kwa sasa wakati hata makusanyo ya kodi za wananchi hayajulikani yanakwenda wapi.

Mzunguko wa pesa wa hapo ni mkubwa sana na zinafanyika biashara nyingi sana lakini miundombinu ni sifuri. Makusanyo ya Halmashauri yanaenda wapi..??

Mlioko huko jitahidini kuhakikisha mnachagua watu wenye upeo mkubwa ili wawe wawakilishi wazuri katika baraza la madiwani na sio hii ya sasa karibu robotatu ya madiwani ni darasa la saba..
 
Hebu orodhesheni hapa madiwani na elimu zao tuone. Hii itatusaidia kuona uwezo wao na elimu yao na kujipanga kwa 2015.
 
St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,404
3,937
Hebu orodhesheni hapa madiwani na elimu zao tuone. Hii itatusaidia kuona uwezo wao na elimu yao na kujipanga kwa 2015.

Mkuu kwa hilo nina imani kuwa wapo watakaokusaidia,ila mimi kwa sasa niko nje ya nchi na siwezi kukupa takwimu za uhakika....
 
NdasheneMbandu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
940
308
Mkuu wenu mpya wa wilaya Mhe. Benson Mpesya vipi siyo mzuri au ameanza kuleta usafasafa wake wa Mbeya?
 
Micro E coli

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
938
192
Mkuu kwa hilo nina imani kuwa wapo watakaokusaidia,ila mimi kwa sasa niko nje ya nchi na siwezi kukupa takwimu za uhakika....

Mkuu huu mji unavijana wazuri tu wasomi lakini sijui wanakimbilia wapi bwana hakuns hata mmoja namuona kwenye siasa za upinzani wanazidiwa na jirani zao kigoma maeneo ya kibondo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom