Wikiend yangu leo imemalizika hivi 😊

Wikiend yangu leo imemalizika hivi 😊

View attachment 3404856

Wasalaam Wakuu!
Pamoja na kuwa active sana humu kwenye mtandao wangu pendwa, nikichangia mada mbalimbali, lakini tangu jana Nilikuwa nasoma kitabu kinachoitwa The Road to Financial Freedom kilichoandikwa na Bodo Schäfer, mtaalam maarufu wa fedha kutoka Ujerumani:

Kitabu Kinafaa kila mtu:
-Vijan
-wafanyakazi
-Jobless
-wafanyabiashara, na mtu yeyote anayehangaika kifedha au kuishi kwa mshahara hadi mshahara (Mtu aliyeajiriwa). Na wale watu wanaotafuta msukumo wa kuchukua hatua ya kifedha.

Kinafundisha kuhusu aina za Maendeleo ya kifedha, motisha na kujifunza kujitegemea kifedha

Bodo Schäfer anatoa mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi mtu anaweza kufikia uhuru wa kifedha ndani ya miaka 7, kwa kutumia nidhamu, maarifa sahihi na mtazamo chanya kuhusu fedha.

Mambo Muhimu niliyojifunza:

1. Kuweka Malengo ya Kifedha

Kutambua unahitaji pesa kiasi gani ili kuwa huru kifedha.

Kutengeneza malengo ya muda mfupi na muda mrefu.

2. Kujilipa Kwanza Mimi Mwenyewe

Kila unapopata kipato, weka asilimia 10 hadi 30 ya mapato yako kwenye akiba kabla ya kutumia.

3. Kutengeneza Vyanzo Vingi vya Mapato

Usitegemee kazi moja tu. Jifunze kuwekeza, kufungua biashara ndogo, au kupata mapato ya mzunguko kama kodi, gawio, au mirabaha.

4. Jinsi ya kuhibiti Matumizi Yako

Kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

Usikopesheke kwa vitu visivyo na tija (mfano: mikopo ya simu, mavazi ya bei).

5. Kuwekeza kwa Busara

Tumia nguvu ya riba iliyounganishwa (compound interest).

Anza mapema hata kama ni kidogo — kadri muda unavyosonga, akiba inaongezeka.

Jifunze kuhusu soko la hisa, mali isiyohamishika, na mifuko ya uwekezaji.

6. Kubadilisha Mtazamo Kuhusu Fedha

Namna ya kuondoa imani potofu kama "pesa ni mbaya" au "sitaweza kuwa tajiri".

Jiamini kuwa unastahili kuwa na utajiri na unaweza kuufikia.

7. Nidhamu ni Muhimu

Uhuru wa kifedha unahitaji uvumilivu na ufuatiliaji wa mpango wa fedha.

Endelea kuweka akiba na kuwekeza hata kama unakutana na changamoto.

8. Kutafuta Mshauri wa Fedha

Kushauriwa na mtu mwenye mafanikio hukusaidia kuepuka makosa makubwa na huongeza kasi ya mafanikio.

Kauli Maarufu Kutoka Kwenye Kitabu:

“Si kiasi unachopata ndicho kinachokufanya uwe tajiri, bali ni kiasi unachohifadhi.”

“Utajiri huanza akilini kabla haujaonekana mfukoni.”

Mpango wa Miaka 7:

Bodo Schäfer anapendekeza mpango wa:
Kutengeneza bajeti ya binafsi
Kuweka akiba kwa bidii
Kuongeza kipato
Kuwekeza kwa maarifa
Kuishi maisha yasiyo na matumizi yasiyo ya lazima.

Wikiend yako imeishaje? 😃
Nimejifunza Siri iliyojificha kwenye Uumbaji
 
Pacha mbona una penda vurugu 😂🦅
Mtu swali dogo anaacha kujibu analeta maneno ya shombo feri..!! 😹😹😹

Huyu manyanza nimemuuliza ana utajiri wa kiasi gani mpk sasa kutokana na bandiko lake na anavyojimwambafai. Ajabu anajiuma uma anasema yeye anaelezea weekend yake ilivyoisha. Hivi hapo umemuelewa?

Muoga wa challenge ndogondogo sasa sijui km hizo pesa ataweza kumiliki..!! 🤣
 
Lakini si ana haki ya faragha?, au utajiri lazima usemwe kwa kila mtu .

sema acha niwa achie mtanange wenu, hili ni jiwe gizani 😂🦅
 
Lakini si ana haki ya faragha?, au utajiri lazima usemwe kwa kila mtu .

sema acha niwa achie mtanange wenu, hili ni jiwe gizani 😂🦅
Sasa tajiri gani hasemi hata anamiliki nini, tutamuamini vipi?? 😹😹

Haya basi atuambie chanzo cha utajiri wake?
Mi ninachojua Manyanza hili bandiko kaiba katuletea hapa ili aonekane genius 🤣
 
Sasa tajiri gani hasemi hata anamiliki nini, tutamuamini vipi?? 😹😹

Haya basi atuambie chanzo cha utajiri wake?
Mi ninachojua Manyanza hili bandiko kaiba katuletea hapa ili aonekane genius 🤣
Ila pacha uki muamulia mtu, huwa haumpi nafasi ya kupumua.

sijui ali zingua wapi, ila usi kanyagie sana 😂 🦅
 
Na yeye ndio moja katika jamii😂
Aahh si unajua kuna mambo ambayo mtu huwa anayafanya kwa sababu
1. Ujasiri wa “kuwa nyuma ya keyboard
2.Upungufu wa adabu au malezi ya mtandaoni kushindwa kuonyesha ule uasili
3. Wivu au chuki ya ndani, mtu anaandika maneno ya kejeli kwa lengo la kupunguza chuki na presha yake
4. Kutafuta likes na attention ambazo hazina maana
5. Mtu ana matatizo yake binafsi na anamwaga kejeli na maneno ya kejeli kwa wengine.

Ni hayo tu Mkuu
 
Swali, una utajiri kiasi gani?
Mbona maelezo mengi Manyanza 😹😹
 
Back
Top Bottom