Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 19,147
- 43,081
Wasalaam Wakuu!
Pamoja na kuwa active sana humu kwenye mtandao wangu pendwa, nikichangia mada mbalimbali, lakini tangu jana Nilikuwa nasoma kitabu kinachoitwa The Road to Financial Freedom kilichoandikwa na Bodo Schäfer, mtaalam maarufu wa fedha kutoka Ujerumani:
Kitabu Kinafaa kila mtu:
-Vijan
-wafanyakazi
-Jobless
-wafanyabiashara, na mtu yeyote anayehangaika kifedha au kuishi kwa mshahara hadi mshahara (Mtu aliyeajiriwa). Na wale watu wanaotafuta msukumo wa kuchukua hatua ya kifedha.
Kinafundisha kuhusu aina za Maendeleo ya kifedha, motisha na kujifunza kujitegemea kifedha
Bodo Schäfer anatoa mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi mtu anaweza kufikia uhuru wa kifedha ndani ya miaka 7, kwa kutumia nidhamu, maarifa sahihi na mtazamo chanya kuhusu fedha.
Mambo Muhimu niliyojifunza:
1. Kuweka Malengo ya Kifedha
Kutambua unahitaji pesa kiasi gani ili kuwa huru kifedha.
Kutengeneza malengo ya muda mfupi na muda mrefu.
2. Kujilipa Kwanza Mimi Mwenyewe
Kila unapopata kipato, weka asilimia 10 hadi 30 ya mapato yako kwenye akiba kabla ya kutumia.
3. Kutengeneza Vyanzo Vingi vya Mapato
Usitegemee kazi moja tu. Jifunze kuwekeza, kufungua biashara ndogo, au kupata mapato ya mzunguko kama kodi, gawio, au mirabaha.
4. Jinsi ya kuhibiti Matumizi Yako
Kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.
Usikopesheke kwa vitu visivyo na tija (mfano: mikopo ya simu, mavazi ya bei).
5. Kuwekeza kwa Busara
Tumia nguvu ya riba iliyounganishwa (compound interest).
Anza mapema hata kama ni kidogo — kadri muda unavyosonga, akiba inaongezeka.
Jifunze kuhusu soko la hisa, mali isiyohamishika, na mifuko ya uwekezaji.
6. Kubadilisha Mtazamo Kuhusu Fedha
Namna ya kuondoa imani potofu kama "pesa ni mbaya" au "sitaweza kuwa tajiri".
Jiamini kuwa unastahili kuwa na utajiri na unaweza kuufikia.
7. Nidhamu ni Muhimu
Uhuru wa kifedha unahitaji uvumilivu na ufuatiliaji wa mpango wa fedha.
Endelea kuweka akiba na kuwekeza hata kama unakutana na changamoto.
8. Kutafuta Mshauri wa Fedha
Kushauriwa na mtu mwenye mafanikio hukusaidia kuepuka makosa makubwa na huongeza kasi ya mafanikio.
Kauli Maarufu Kutoka Kwenye Kitabu:
“Si kiasi unachopata ndicho kinachokufanya uwe tajiri, bali ni kiasi unachohifadhi.”
“Utajiri huanza akilini kabla haujaonekana mfukoni.”
Mpango wa Miaka 7:
Bodo Schäfer anapendekeza mpango wa:
Kutengeneza bajeti ya binafsi
Kuweka akiba kwa bidii
Kuongeza kipato
Kuwekeza kwa maarifa
Kuishi maisha yasiyo na matumizi yasiyo ya lazima.
Wikiend yako imeishaje? 😃