johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,968
- 141,976
Karibu ufuatilie matangazo hayo mubashara kupitia luninga ya ITV! Kwa hotuba ya leo kuna kila dalili ya mtu fulani kutumbuliwa soon!
=====
UPDATES
JAJI MKUU
Wananchi wa Tanzania, watarajie huduma bora za uendeshaji wa kesi, uwazi na huona hukumu kwani Tehama itarahisisha yote haya na sisi majaji, mahakimu na watendaji wa Mahakama tubadili fikiri zetu na kuijua Tehama kwani karne hii inahitaji kwenda na wakati
Utaratibu unafanyika ili kukamilisha mfumo wa menejimenti za kesi ambayo itatumika kulipa ada, uendeshaji wa kesi kwa masafa ya mbali.
Idadi ya majaji waliopo hayaendani na majalada wanayopewa kuyasikiliza kwani majaji waliopo ni 62 pekee na kila mwaka wanabeba majalada 535 badala ya 225 wanayopaswa kuyasikiliza.
Huu ni mzigo mkubwa sana na iko nje ya makubaliano kwamba kila jaji amalize majalada 225 lakini kwa idadi hii ni mzigo mkubwa sana
Mpaka sasa ni mikoa 14 kati 26 pekee ndizo zenye Mahakama Kuu ambapo malengo ni kuwa na Mahakama Kuu katika mikoa 22 ifikapo mwaka 2020. Malengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 wilaya zote 139 za Tanzania bara zinakuwa na Mahakama za wilaya.
Hatutamwonea mtumishi lakini hatutamvumilia mtu anayetupaka matope sisi kama Mahakama
MAKAMU WA RAIS TLS
Matarajio yake (Rais Magufuli) hayafiki kwetu sisi na kwa maoni yangu matarajio ya kiongozi wangu huyu yanaakisi matarajio ya wananchi
Mahakama inafaa kuwa mahali iliyotukuka kwani ni mahali pekee tunapokuwa na migogoro, pale tunapoililia sheria tunakwenda mahamakani na hii haijalishi aina ya mtu.
Tusiitumie Mahakama kama majaribio, maabara au jumba la kamari. Majaji msiitumie hata Mara moja kwani mnalindwa kisheria na msimamie hilo ili Mahakama isionekane ya ajabu ajabu
RAIS MAGUFULI
Kwa kuadhimisha siku hii ya sheria maana yake ni kwamba nchi yetu inatambua umuhimu wa sheria katika kusimamia haki, kudumisha amani na kuleta maendeleo ya nchi
Maadhimisho haya ya siku ya sheria ni muhimu kwa vile yanatoa fursa kwa vyombo vinavyohusika na masuala ya sheria na utoaji haki, yani Mahakama, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jeshi la polisi, Magereza, TAKUKURU, Mwendesha Mashtaka wa Serikali na Mawakili.
Napenda kutumia fursa hii kuvipongeza vyombo vyote vinavyohusika na masuala ya sheria na haki nchini, kwa kazi kubwa ya kusimamia sheria na kutoa haki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita
Naipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanya ya kutoa haki, lakini katika hotuba yangu mbele huko nitatoa changamoto lakini nimeanza kuipongeza kwanza, kwahiyo yale yatakayokuja ni changamoto tu
Ucheleweshaji wa kesi umefanya baadhi ya makampuni zikiwemo benki kufirisika hii ni moja ya sababu zinazofanya riba za benki zetu kuwa juu.
Pamoja na pongezi nilizozitoa kwenu hivi punde, jambo moja lipo dhahiri kwamba usimamizi wa sheria na mfumo wa utoaji haki nchini bado unakabiliwa na matatizo mengi, na moja ya matatizo hayo ni kupungua kwa uadilifu kwa watumishi wachache wa vyombo vyetu
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Twaweza hivi karibuni umeonesha kiwango cha rushwa kimepungua kwa 85%, ikilinganishwa na miaka 5 iliyopita huku Polisi na Mahakama zikiongoza kupokea rushwa, tunaweza tukawa hatuutaki utafiti, lakini hatuwezi kupuuzia.
Kwa vile nafahamu kuwa watumishi wengi wa vyombo hivi ni wazuri na waadilifu lakini hawa wachache hatupaswi kuwaacha kwa vile matendo yao yanavichafua sana vyombo vyetu, hawa ndio wanaodai rushwa, kuwabambikiza kesi wananchi, wanachelewesha upelelezi
Mimi nina uwezo wa kusema hadharani sababu nilipewa jukumu hilo na watanzania,mimi nimeumbwa kusema ukweli na hiyo ndio tabia yangu na sitaibadilisha unipige ,uniweke kwenye shimo, univuruge nikitoka nitasema ukweli.
Kinachoshangaza pamoja na hatua nzuri ya Serikali kupeleka 'Legal Aid Act' ya mwaka 2017 na mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini 'regulation' mpaka saizi hazijaletwa ila Waziri yupo tena Mwanasheria, tena ni Profesa, AG yupo, Deputy AG yupo
Jamani mtanisamehe sana mimi ndivyo nilivyo nawasema hapa hapa kwa hiyo wewe Profesa Juma na majaji na mahakimu hamna 'Instrument' za kuweza kutoa uamuzi. Wabunge wao wamepitisha sheria, mimi nikaletewa nikasaini lakini regulations mpaka leo miezi tisa imepita
Watu wapo wanakula tu mishahara, magari wanayo na viyoyozi vipo ila wananchi wanapata shida na muda mwingine mtasingiziwa mahakama kwamba hamtoi haki kumbe ni Serikali watendaji wake hawatoi haki kwa Watanzania,
Ndiyo maana nawaambia changamoto zingine zipo ndani ya Serikali lazima na mimi nijitathimini ninachaguaje hawa watu ambao wanachelewesha chelewesha, hiyo ndiyo tathimini ambayo ninaanza kujifanyia kuanzia leo.
Bado kuna tatizo kubwa ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG (Mwanasheria Mkuu), panakuwa na ushahidi na nyie Majaji mnaona lakini hakuna wa kuutetea. Mwaka jana nililamika, mwaka huu nitalishughulikia, tena kabla ya Februari hii kuisha
Naipongeza sana tume ya utumishi wa Mahakama ambayo ipo chini ya Jaji Mkuu kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwafukuza watumishi wa Mahakama wapatao 112 ambao walibainika kuhusika na vitendo vya rushwa
Hivi majuzi nilitoa msamaha kwa wafungwa, lakini nimesikitika kusikia baadhi yao tayari wamekamatwa kwa uhalifu tena,ipo haja kuangalia upya mafunzo ya magerezani.
Wanatoa hukumu zinazopendelea watu, kuchelewesha hukumu au kesi na kati ya 112 waliofukizwa au kustaafishwa 27 walikuwa Mahakimu na wote walipokwenda Mahakamani walishinda
Walikuwa Mahakimu 14 walifukuzwa kazi, 67 watumishi wa kawaida walifukuzwa kazi. Wito wangu kwa vyombo vingine IGP, Mkuu wa Magereza, Takukuru muige mfano wa Profesa Juma (Ibrahim Juma-Jaji Mkuu.
Habari zaidi....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali inaunga mkono utekelezaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Mahakama ili kuongeza ufanisi wa majukumu yake.
Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo tarehe 01 Februari, 2018 wakati akihutubia katika siku ya sheria, maadhimisho ambayo yamefanyika katika Mtaa wa Chimala, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, yakiwa na kauli mbiu “Matumizi ya Tehama katika utoaji wa haki kwa wakati na kuzingatia maadili”.
Pamoja na kuunga mkono matumizi ya TEHAMA kwa Mahakama, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Mahakama kwa kazi inayoifanya ikiwemo kupunguza mrundikano wa kesi na ameahidi kuwa Serikali ipo tayari kusikiliza ushauri wa Mahakama juu ya maslahi ya wafanyakazi utakaotolewa mwezi huu na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.
Pia Mhe. Rais Magufuli amesema yupo tayari kufanya uteuzi wa Majaji wengine kadiri atakavyoshauriwa na Mahakama ili kukabiliana na changamoto ya upungufu mkubwa wa Majaji iliyosababisha ongezeko kubwa la mrundikano wa mashauri katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.
Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kuendelea kurekebisha dosari ambazo zimekuwa zikiuchafua mhimili huo wa Dola ikiwemo Majaji na Mahakimu kujihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa na ucheleweshaji wa kesi ambavyo vinasababisha hasara kubwa kwa Taifa.
“Nilikuuliza Mhe. Jaji Mkuu na mimi nasema kwa uwazi kabisa, katika vibali vingi vya kusafiri nje ya nchi ninavyoombwa na Majaji na ambavyo vyote huwa ninaruhusu, na vimenisaidia kufanya utafiti wangu, wengi huwa wanaomba kwenda likizo nje ya nchi, Afrika Kusini, Uingereza, nakadhalika, na wanaenda na familia zao, wanakaa huko kwa siku 28, na pale chini wanaandika kuwa watajigharamia, hili huwa ni swali ninalojiuliza sana, maana mshahara wa Jaji ninaujua.
“Na ukweli huwa nafuatilia anapokwenda kule anakaa hotel na nani amehusika kulipa hotel hiyo yenye gharama za juu, na kwa nini ni fulani fulani tu, Mhe. Jaji Mkuu majibu hujayapata na mimi sijayapata, sasa Mhe. Jaji Mkuu fuatilia hili” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Jaji Mkuu kwa hatua alizochukuwa kuwafukuza kazi watumishi 112 wa Mahakama wakiwemo Mahakimu 17 waliojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili na amevishangaa vyombo vingine ambavyo hushirikiana na Mahakama kama vile Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Magereza na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa kutowawajibisha watumishi wake wanaokiuka maadili.
“Mwaka jana nililalamika, sasa mwaka huu sitalalamika, nitachukua hatua, tena mwezi huu wa pili hautaisha, pale ofisini kwangu napokea barua nyingi za malalamiko ya ucheleweshaji wa kesi, kila kesi upelelezi haujakamilika, ni lazima kuwe na utatuzi wa jambo hili, hivi sasa kuna kesi za Shilingi Bilioni 169.1 na Dola za Marekani Milioni 38.2 zinasubiri tu na nchi inakosa mapato” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, kukamilisha kanuni za sheria ya msaada wa kisheria (Legal Aid Act, No.1 of 2017) ambayo imepitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais tangu miezi 9 iliyopita, ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa.
Mapema kabla ya hotuba ya Mhe. Rais Magufuli Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema Mahakama imedhamiria kuanza matumizi ya TEHAMA katika shughuli zake na ametaka watumishi hasa Majaji na Mahakimu wajiandae kutumia teknolojia hiyo, na pia ameahidi kuwa Mahakama itaendelea kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kusimamia uwajibikaji.
Nae Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Mhe. Godwin Simba Ngwilimi amesema TLS inaunga mkono dhamira ya kutumia TEHAMA katika shughuli za Mahakama na amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake unaoakisi nia na matarajio ya Watanzania.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam