Wiki ya Sheria: Rais Magufuli awabadilikia Waziri Kabudi, AG Masaju na DPP kwa kukwamisha haki kutendeka

huo ndo ukweli houpe Rais wao atakanusha hukohuko aliko maana yeye ni mkali kwanza wa kupinga kila jambo.
 
Makamu mwenyekiti wa chama cha mawakili (TLS) Godwin Ngwilimi leo kwenye maadhimisho ya 22 ya wiki ya sheria amesema wanampongeza rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya wananchi kwa kutatua kero mbalimbali zinazowakumba wananchi.

Maadhimisho hayo yanafanyika leo tarehe 1/02/2018

Source .Mwananchi .

My take . Pongeze hizi za TLS kwa rais Magufuli ni kinyume kabisa na matarajio ya chadema , ambao walitarajia Rais Magufuli achukiwe na wanasheria baada ya Tundu Lisu kupata matatizo ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma.
Safi,chadomo watambue tundu lissu wao anasura mbili ya ucdm na uTLC,kwenye ucdm atapiga burabura zake ilo apate mkate wa kila siku kwenye uTLS ni hapa kazi tu hakuna rongorongo
 
Uteuzi huo ufanyike kwa haki bila upendeleo wa aina yoyote ili mradi wawe na sifa za uadilifu wa kuwatumikia wananchi, kuna mahakimu wengi waadilifu wanaweza kufanya Kazi za ujaji kwa weledi mkubwa na kupunguza changamoto za mlundikano wa kesi, tubadilike tusifanye Kazi kwa mazoea.
 
Boniphace Kichonge naona leo thread zako zote ni kuhusu ufunguzi wa hiyo shughuli ya sheria. Hongera. Huu sasa ni kama uzi wa saba tangu Rais atoe hotuba. Endelea kuleta na zingine na zingine na zingine
 
Prof kabudi anatengenezewa namna ya kuchomolewa, inaonekana issue ya makinikia imekaa vibaya. Ndio maana sikuhizi kabudi yuko kimya sana.
 
Hili la makonda kutengeneza mahakama bubu mnazi mmoja ni wazi mpira anao midfilder ikitolewa pass goli ninaingia.

Ningekuwa mie kabudi ningejifanya visiting lacturer kama dr.david msuya.
 
Mkuu huo ni unafiki tena mkubwa sana. Anachukizwaje na rushwa wakati yeye mwenyewe ndiyo mtoa rushwa mkubwa nchini? Kumbuka milioni 10 kila mbunge wa CCM ili wapitishe muswaada uchwara na mabilioni ya kununua wachumia tumbo toka upinzani na vyeo pia. Wanafiki ndivyo WALIVYO!!!!

Angalao leo ameonyesha kuchukizwa na rushwa, chuki hii sasa ihamie kwenye kuhonga upinzani
 
Hakuna sababu ya msingi yakuacha kuteua majaji wa kutosha wa kusikiliza kesi wakati nchi yetu ina wasomi wengi weledi ambao wana sifa za kuwa majaji, kuna mahakimu waadifu na wajuzi wana uwezo wa kufanya Kazi.
Hongre JPM kwa kuliliona hilo, sasa naamini mhimili huu chini ya Jaji MKUU utanyooka.
 
Hakuna sababu ya msingi yakuacha kuteua majaji wa kutosha wa kusikiliza kesi wakati nchi yetu ina wasomi wengi weledi ambao wana sifa za kuwa majaji, kuna mahakimu waadifu na wajuzi wana uwezo wa kufanya Kazi.
Hongre JPM kwa kuliliona hilo, sasa naamini mhimili huu chini ya Jaji MKUU utanyooka.
Sema utaimarika!i
 
Back
Top Bottom