Wife kanuna kisa nimepata shavu Uganda

Wife kanuna kisa nimepata shavu Uganda

Hata angekuwa Nani angenuna tu, urudi na dola elfu 15 na iPhone 7 juu na mazaga zaga mengine kibao Bure Bure tu? Mmmmh lazima wife ashtuke asee. Ulipewa bure? Bado ulipewa hospitality ya hali ya juu na Jack Pemba? 5 star hotel ukafikia! Mmmh mashaka kwa kweli

Kama kweli wife anakupenda kwa dhati lazima ashtuke na kughadhabika sana aisee
Kwahiyo unata kumaanisha nini?
 
Ana hofu na jack pemba hizo zawadi na urafiki wenu maana inasemekana eti uwa ana tabia ya kuea cameroon watu.
Sasa anahisi baada ya ile bday jack kanogewa anataka akuhamishe kabisa uwe karibu naye
 
why hujaenda nae? usimlinganishe mke wako na kitu chochote, hata hiyo sherehe haikuwa muhimu sanaa kwenda kuliko kumsikiliza mkeo!
 
Hata angekuwa Nani angenuna tu, urudi na dola elfu 15 na iPhone 7 juu na mazaga zaga mengine kibao Bure Bure tu? Mmmmh lazima wife ashtuke asee. Ulipewa bure? Bado ulipewa hospitality ya hali ya juu na Jack Pemba? 5 star hotel ukafikia! Mmmh mashaka kwa kweli

Kama kweli wife anakupenda kwa dhati lazima ashtuke na kughadhabika sana aisee
Hahaha , nadhani akisoma vizuri hapa atakuelewa.
 
Hawa wanawake hawana cha kupoteza...mwanaume ndio anayepoteza. Jichange kichwani na ufanye jambo sahihi.
 
Analinda haki yake ya ndoa maana hizo treatent za jack sio hivihivi!!
 
At the first place ingewezekana kwenda nae ungeenda nae.
And now kama inawezekana nendanae.
Si mwili mmoja nyie. Au haukuahidi kumpenda na kua nae adi mtenganushwe na kifo?

Tafakari i i i inaonekana anakupenda. So ww kama mwanaume na mmewe fanya uamuzi sahihi usifikirie kumuacha nisahihi wakati hapo hamna kosa kwake zaid ya kuonyesha concern yake
 
a1a235736c43b881faef67a630e4e514.jpg


Hii kitu inapokelewa kwa shingo upande...
 
Hana kwao??ulimkuta juu miti??inaonesha unatafuta sababu tu ila umemchoka cku nying!ukisusa wenZio wanakula kalagabaho![emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57]
Lakini humu watu wana ushauri. Unaweza ukawa umebanwa na mawazo ukasoma ushauri ikabidi ucheke mwenyewe tena kwa sauti. Ha ha ha
 
Wakishua unapewaje pesa kirahisi rahisi hivyo wakati watu tunahaso hatuzioni. Wife lazima anune. Nlitegemea wewe ndo umpe mwenye sherehe zawadi lakini cha kustaajabisha wewe ndo umepewa zawadi. Duh. Kizungumkuti
 
Habari wadau wa jukwaa pendwa, jukwaa nalolipenda kushinda mengine hasa kutokana na kuwa na vioja vingi kila kukicha.

Muda mrefu umepita tangu kutia maguu kwenye jukwaa hili, hiyo ni kutokana na shughuli zangu za kijasiriamali ambazo zimekuwa zikini-keep busy 24/7 365.
Baada ya kuamua kufanya maamuzi magumu ya kujiajiri, hatimaye nimeanza kuona mafanikio japo kwa mbali.

Sasa ishu inakuja ni kwamba, wiki moja iliyopita, rafiki yangu wa kitambo sana ndg. Jack Pemba a.k.a The Money Bag kama anavyojulikana Uganda kwa sasa, aliweza kunipa mwaliko wa kuhudhuria kwenye birthday yake ambapo mgeni rasmi alikuwa Koffi Olomide.

Kasheshe likaanzia home, wife akawa amenuna na haku-bless kabisa ile safari yangu, sema hakuwa na jinsi maana huwezi kuzuia mvua kunyesha, ikabidi nikwee pipa mpaka kwenye ardhi ya Museveni.

Kwa ujumla nili-enjoy sana bata la Uganda hasa ile Hospitality niliyoipata kutoka kwa mwenyeji wangu, hotel yenye hadhi ya nyota tano (5) ambayo ndiyo nilifikia hapo, kipindi chote hicho nilikuwa namu-update wife kinachoendelea.

Sasa ishu ikaja ni kwamba nimepata mchongo wa nguvu Uganda hasa kutokana na Network niliyoipata siku ile, maana ilikuwa ni birthday moja classic, kama nyie mtakuwa watembeleaji wa mitandao hasa ya UG bila shaka mtaweza kuona.

Baada ya kurudi nyumbani na kumuelezea mama watoto akawa amenuna mara mbili ya nilivyomuacha, ameanza kunitolea kashfa za ajabu ajabu, kama hiyo haitoshi nimerudi home na dola zaidi ya elfu 15 na package ya iPhone 7 na takataka nyingine.

Nikaona nimpatie maana mimi sio mpenzi sana wa bidhaa za Apple, lakini wife aliipokea kishingo upande, hata haki zangu za msingi za usiku kanipa kwa masharti kama vile ndio tunaanza U-boyfriend na U-girlfriend.

Jamani waungwana, huyu mwanamke nimfanyie nini? maana naona tunapoelekea nitaanza kumchoka mapema kabisa, ndoa kila siku visa na mikasa.. Arghhhhhhhhhh I'm Fed Up...
Asante sana Rutashobya kwa tangazo lako japo ujalipia vat. Usijali utapata wateja wa hizo iphone 7 japo nia yako hapa ilikuwa nikujisifia sio kuhusu mke wako kununa nadhani wenye akili watakuwa wameelewa
 
Ulienda kufanya biashara gani? Au ulienda kusafishwa njia. Ualikwe kwenye birthday halafu upewe na zawadi juu. Au yai lilishapasuliwa na ndiyo hiyo biashara unayosema umejiajiri. Nawaza tu kwa ukimya
 
Back
Top Bottom