Wife kanuna kisa nimepata shavu Uganda

WA KISHUA

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
365
130
Habari wadau wa jukwaa pendwa, jukwaa nalolipenda kushinda mengine hasa kutokana na kuwa na vioja vingi kila kukicha.

Muda mrefu umepita tangu kutia maguu kwenye jukwaa hili, hiyo ni kutokana na shughuli zangu za kijasiriamali ambazo zimekuwa zikini-keep busy 24/7 365.
Baada ya kuamua kufanya maamuzi magumu ya kujiajiri, hatimaye nimeanza kuona mafanikio japo kwa mbali.

Sasa ishu inakuja ni kwamba, wiki moja iliyopita, rafiki yangu wa kitambo sana ndg. Jack Pemba a.k.a The Money Bag kama anavyojulikana Uganda kwa sasa, aliweza kunipa mwaliko wa kuhudhuria kwenye birthday yake ambapo mgeni rasmi alikuwa Koffi Olomide.

Kasheshe likaanzia home, wife akawa amenuna na haku-bless kabisa ile safari yangu, sema hakuwa na jinsi maana huwezi kuzuia mvua kunyesha, ikabidi nikwee pipa mpaka kwenye ardhi ya Museveni.

Kwa ujumla nili-enjoy sana bata la Uganda hasa ile Hospitality niliyoipata kutoka kwa mwenyeji wangu, hotel yenye hadhi ya nyota tano (5) ambayo ndiyo nilifikia hapo, kipindi chote hicho nilikuwa namu-update wife kinachoendelea.

Sasa ishu ikaja ni kwamba nimepata mchongo wa nguvu Uganda hasa kutokana na Network niliyoipata siku ile, maana ilikuwa ni birthday moja classic, kama nyie mtakuwa watembeleaji wa mitandao hasa ya UG bila shaka mtaweza kuona.

Baada ya kurudi nyumbani na kumuelezea mama watoto akawa amenuna mara mbili ya nilivyomuacha, ameanza kunitolea kashfa za ajabu ajabu, kama hiyo haitoshi nimerudi home na dola zaidi ya elfu 15 na package ya iPhone 7 na takataka nyingine.

Nikaona nimpatie maana mimi sio mpenzi sana wa bidhaa za Apple, lakini wife aliipokea kishingo upande, hata haki zangu za msingi za usiku kanipa kwa masharti kama vile ndio tunaanza U-boyfriend na U-girlfriend.

Jamani waungwana, huyu mwanamke nimfanyie nini? maana naona tunapoelekea nitaanza kumchoka mapema kabisa, ndoa kila siku visa na mikasa.. Arghhhhhhhhhh I'm Fed Up...
 
Bikuhabari wadau wa jukwaa pendwa, jukwaa nalolipenda kushinda mengine hasa kutokana na kuwa na vioja vingi kila kukicha.

Muda mrefu umepita tangu kutia maguu kwenye jukwaa hili, hiyo ni kutokana na shughuli zangu za kijasiriamali ambazo zimekuwa zikini-keep busy 24/7 365.

Baada ya kuamua kufanya maamuzi magumu ya kujiajiri, hatimaye nimeanza kuona mafanikio japo kwa mbali.

Sasa ishu inakuja ni kwamba, wiki moja iliyopita, rafiki yangu wa kitambo sana ndg. Jack Pemba a.k.a The Money Bag kama anavyojulikana Uganda kwa sasa, aliweza kunipa mwaliko wa kuhudhuria kwenye birthday yake ambapo mgeni rasmi alikuwa Koffi Olomide.

Kasheshe likaanzia home, wife akawa amenuna na haku-bless kabisa ile safari yangu, sema hakuwa na jinsi maana huwezi kuzuia mvua kunyesha, ikabidi nikwee pipa mpaka kwenye ardhi ya Museveni.

Kwa ujumla nili-enjoy sana bata la Uganda hasa ile Hospitality niliyoipata kutoka kwa mwenyeji wangu, hotel yenye hadhi ya nyota tano (5) ambayo ndiyo nilifikia hapo, kipindi chote hicho nilikuwa namu-update wife kinachoendelea.

Sasa ishu ikaja ni kwamba nimepata mchongo wa nguvu Uganda hasa kutokana na Network niliyoipata siku ile, maana ilikuwa ni birthday moja classic, kama nyie mtakuwa watembeleaji wa mitandao hasa ya UG bila shaka mtaweza kuona.

Baada ya kurudi nyumbani na kumuelezea mama watoto akawa amenuna mara mbili ya nilivyomuacha, ameanza kunitolea kashfa za ajabu ajabu, kama hiyo haitoshi nimerudi home na dola zaidi ya elfu 15 na package ya iPhone 7 na takataka nyingine.

Nikaona nimpatie maana mimi sio mpenzi sana wa bidhaa za Apple, lakini wife aliipokea kishingo upande, hata haki zangu za msingi za usiku kanipa kwa masharti kama vile ndio tunaanza U-boifriend na U-girlfriend.

Jamani waungwana, huyu mwanamke nimfanyie nini? maana naona tunapoelekea nitaanza kumchoka mapema kabisa, ndoa kila siku visa na mikasa.. Arghhhhhhhhhh I'm Fed Up...
Hana kwao??ulimkuta juu miti??inaonesha unatafuta sababu tu ila umemchoka cku nying!ukisusa wenZio wanakula kalagabaho!
 
Hata angekuwa Nani angenuna tu, urudi na dola elfu 15 na iPhone 7 juu na mazaga zaga mengine kibao Bure Bure tu? Mmmmh lazima wife ashtuke asee. Ulipewa bure? Bado ulipewa hospitality ya hali ya juu na Jack Pemba? 5 star hotel ukafikia! Mmmh mashaka kwa kweli

Kama kweli wife anakupenda kwa dhati lazima ashtuke na kughadhabika sana aisee
 
Ahaaaa wa kishua tena? Nilimiss sana stori zako karibu jukwaani.

Waifu wako mwache anune tu akileta za kuleta mletee toto la kinyankore ( abahima ba lakai, mtungamo) banangeee lazima anyooke.
 
Hata angekuwa Nani angenuna tu, urudi na dola elfu 15 na iPhone 7 juu na mazaga zaga mengine kibao Bure Bure tu? Mmmmh lazima wife ashtuke asee. Ulipewa bure? Bado ulipewa hospitality ya hali ya juu na Jack Pemba? 5 star hotel ukafikia! Mmmh mashaka kwa kweli

Kama kweli wife anakupenda kwa dhati lazima ashtuke na kughadhabika sana aisee
Nadhani Unazungumzia Ile Philosophy Ya SUGU.
 
Hana lolote ni wivu tu huo unaomsumbua jitahid ktk hzo safar zako umkusanye uende nae akajionee unachoenda kufanya kwa macho yake sio kila siku unamsimulia tu...
Naamin inaweza ikasaidia kias flan akapoa
 
15876259_1809870292586791_6536703172382031872_n.jpg
 
MPE namba ya jack Pemba.atatulia.we hadi mange kimambi anajitongozesha kwa jamaa.unafikiri mchezo.
 
Hata mm ningenuna tuu,.kwann uwende pekeako wakati sisi tushakuwa mwili mmoja!?tena umeenda kuenjoy eti sherehe Bora ingekuwa kikazi.....kuna hatihati ulimsaliti pia mkeo ww..
 
Kwa ujumla nili-enjoy sana bata la Uganda hasa ile Hospitality niliyoipata kutoka kwa mwenyeji wangu, hotel yenye hadhi ya nyota tano (5) ambayo ndiyo nilifikia hapo.

Ameanza kunitolea kashfa za ajabu ajabu, kama hiyo haitoshi nimerudi home na dola zaidi ya elfu 15 na package ya iPhone 7 na takataka nyingine.

Wife anajua hakuna cha bure, ndani ya siku mbili tu umepata USD 15K na iphone?

Anahisi soon utashindwa kumpa haki yake ya ndoa.
 
Back
Top Bottom