Why "Vita vya Ufisadi" failed and will never win election..

There is no such a thing called solution at this point......The solution was to adhere to the rule of law in which they took an oath to keep and protect it,.. but that is not the case now...

They know what to do since then they assumed the highest office of the land!!We could have not trusted them if at all they knew nothing!! JK shy away from taking the difficult path,but wananchi,if they a keen enough will do it come 2010...Just keep hope alive!!

Cheers to you Comrade TD,

The hopes are still alive, but focusing simply towards 2010 is a short term goal which results into short term Solution.

Our focus should transition into long term goals that will offer long term solution.

So far the short term goal strategy that was started by NCCR in 1992 at creation of Multipartism, has not yet worked!

Just to show you what posibilities are there for Tanzania to be a developing country, read this article; It shows how Tanzania can be self sufficient and get away from being dependent, the problem that lies ahead of us to tap these resources carefully and progressivelly is what I have just addressed to Serpent General above.

2008-08-31 09:07:51
By Staff Writer

As massive poverty continues to rock the majority of Tanzanians, the latest data reveal that Tanzania`s wealth in terms of the top five metals out of eleven provable mineral deposits amounting to millions of tonnes.

It is hard to believe it, but that is the reality in a country where 38million plus population lives in abject poverty, below a dollar per day, while 89percent of the total population survive on a single meal per day.

According to a geological survey conducted last year by the ministry of energy and minerals, Tanzania has huge reserves in eleven key minerals which include gold, Nickel, Tanzanite, Diamonds, copper, Iron ore, coal, Limestone, soda ash, gypsum and phosphate.

The five key minerals and their provable amounts in brackets is Gold (2,222tones), Nickel (209million tones), Diamonds (Carat 50.9million), Copper (13.65million tones), and Iron ore (103million tones).

However since this was just a geological survey undertaken by experts last year, its actual result is approximated to be accurate by up to 70 percent.

So far, only three types of minerals - gold, diamonds, Tanzanite - are being fully mined by multinational companies which at the end of the day take 97percent, leaving only peanut to the original Tanzanian owners.

If well managed through sound, people-centered mining policies, the mining sector can catapult Tanzanians to the proverbial promised land in decades and generations to come.

Comparing these huge deposits and the actual situation of poverty in the country, the message that comes across one`s mind is that Tanzania is in what experts describe as `resource curse`.

The term `resource curse` refers to the observation that nations with rich endowments of natural resources (oil, metals, timber) often dramatically under-perform economically relative to what one would expect.

Common sense and simple economics suggest that countries blessed with an abundance of natural resources should live long and prosper.

Yet over many years, it has been observed that nations rich in oil, gas, or mineral resources have been disadvantaged in the drive for economic progress.

Why are we poor?

Perhaps the biggest question that begs an urgent answer is; why are we so poor despite having all these huge minerals deposits?

It is a question that policy makers and politicians have been avoiding to seek answers for.

Tanzania like many other African countries is highly blessed with rich natural resources, but its people are swimming in the deep sea of massive poverty.

But the appalling truth is that instead of financing people`s development, Africa\\'s huge mineral resources were used to fund the brutal civil wars that ravaged millions of people during the past four decades.

Today in Africa only a few countries like Botswana, Ghana and South Africa have managed to use their natural resources, especially minerals, to facilitate development and welfare to their people.

This example is vividly manifested in the Democratic Republic of Congo, Sierra Leone, Ivory Coast, Nigeria, Sudan and Angola whereby masters of the wars used natural resources to finance their deadly power struggle.

However in Tanzania, there wasn`t any civil war apart from the role played by the founding President, (the late) Dr Julius Nyerere, in liberating Southern African countries during the nationalist struggle.

While it is an undeniable truth that the move to allow the private sector to participate in the mining industry was brilliant one, the truth is that due to poor policies introduced by the third phase government, the whole idea has become a disaster to Tanzanians.

This is well echoed in the lucrative mining industry which has been mainly benefiting multinational companies, while paying the government a small slice of the cake.

Last year, for instance, the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, told the parliament that during the period between 2001 and 2006, Tanzania produced gold worth $2.6 billion (Tshs3.38 trillion), but the government earned only $78 million.

In simple arithmetic, this is just 3 percent of the total revenues generated from thousands of tonnes of gold produced in the Lake Victoria gold belt. It also shows that the government earned an average of $13 million annually during that period from the multibillion industry whose real investments currently is valued at $2.5 billion.

According to the available statistics from the mining industry, from June 2000 to December 2006, the two biggest gold mines in the country produced a total of 5,686,710 ounces of gold, which at the current gold price of $600 per ounce is valued at Tshs 4.3 trillion ($ 3.3 billion), but what the nation earned is frightening and a shame.

While mineral production has increased in Tanzania in the past few years with export per year estimated to be nearly $900 million (Tshs1.17 trillion), the contribution of the mining sector to the Gross Domestic Product (GDP) remains very minimal, accounting to 3 percent.

According to the National Economic Survey report released in 2006, the growth rate of mining and quarrying sector increased from 15.4 percent in 2004 to 15.7 percent in 2005, whereby the increment was attributed to new investments in Tulawaka gold mines in Biharamulo District, Kagera Region.

The report further states that, the contribution of the sector to GDP, which is the total value of goods and services produced in a country during a year, increased from 3.2 percent in 2004 to 3.5 percent in 2007.
 
Nadhani lazima tuanze na kuweka term limits katika nafasi zote za kisiasa kuanzia udiwani, ubunge, uwaziri, ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa na kadhalika kama ilivyo kwa rais. Mtu ataweza kuniuliza kuwa hizo term limits zitasaidia nini, lakini ukweli ni kuwa zitasaidia kuwafanywa viongozi wajue kuwa madaraka yao yana mwisho, na endapo watashindwa kutekeleza majukumu yao sawasawa wataweza kuchukuliwa hatua za kisheria na uongozi utakaofuata.
 
Jamani, kama hali ndio hii ya kuonenana aibu wakati wa kufanya maamuzi dhidi ya Mafisadi na walarushwa, je tutafika wapi? Hebu angalia Kauli ya Katibu mkuu Kiogozi anayoanza kujichanganya kuhusu hatma ya Hosea na Mwanyika...! Kwa hali hii kweli rushwa na Ufisadi hautakaa uishe Tanzania...!


Na Timu ya Majira Jumapili
Said Mwishehe na Reuben Kagaruki.

SIKU chache baada ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kuwasilisha Bungeni taarifa ya Serikali juu ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kufuatia kashfa ya kampuni tata ya Richmond na kubainisha kuwa vigogo kadhaa Serikali waliohusishwa na kashfa hiyo hatIma yao iko ngazi za juu, Ikulu imetoa tamko rasmi.

Ikulu jana imetoa msimamo wake kwa mara ya kwanza juu ya kinachoendelea baada ya kuachiwa dhamana ya uamuzi juu ya vigogo hao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bw. Luhanjo alisema Serikali haitaki kukurupuka juu ya hatima ya akina Hosea, Mwanyika na Mwakapugi akisema ni suala zito linalogusa maisha ya watu na familia zao.

"Suala hili tunalishughulikia, unaposhughulikia maisha ya mtu haustahili kutoa uamuzi wa kukurupuka...tunashughulikia, hatukurupuki," alisema na kuashiria kuwa kwa sasa kazi iliyoko mbele yao ni kupima uzito na athari za kila uamuzi utakaofanyika.


"Kabla ya kutoa uamuzi lazima upime kwanza na sio kukurupuka...Hebu fikiria ungekuwa wewe mtu anakuhukumu kufungwa kwa kukurupuka, familia yako na wewe mwenyewe mtaathirika kwa kiasi gani? alihoji.

Bw. Luhanjo hata hivyo alikwepa swali lililomtaka athibitishe iwapo ofisi yake imekwishapokea maelezo ya utetezi kutoka kwa maofisa hao wote na hatua ambazo itazichukua.

"Kwani Waziri (Waziri Mkuu) alisemaje? Alisema wamewasilisha maelezo yao kwa kamati ya nidhamu."

Akiwasilisha ripoti hiyo Bungeni Alhamisi wiki hii, Bw. Pinda akizungumzia suala vigogo hao kwa nyakati tofauti katika ripoti yake alisema: "Ili kutekeleza Azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.

"...Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa Watendaji Wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu.

"Bwana Mwakapugi amekwishawasilisha maelezo yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ndiye Mamlaka yake ya nidhamu katika muda uliotakiwa."

Bw. Luhanjo hakutaka kuingia kwa undani kuhusu muda ambao Ikulu itachukua kabla ya kutoa uamuzi wake juu ya vigogo hao.
 
Nadhani lazima tuanze na kuweka term limits katika nafasi zote za kisiasa kuanzia udiwani, ubunge, uwaziri, ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa na kadhalika kama ilivyo kwa rais. Mtu atawea kuniuliza kuwa hizo term limits zitasaidia nini, lakini ukweli ni kuwa zitasaidia kuwafanywa viongozi wajua kuwa madaraka yao yana mwisho, na endapo watahsindwa kutekeleza majukumu yao wataweza kuchukuliwa hatua na uongozi utakaofuata.

Mwalimu,

You have said it well, may be tukiachana na Ubunge wa kudumu, watu wataanza kuamka na kufanya kazi!
 
Hivi jamani, pamoja na ushaidi wote uliotolewa na Ripoti ya Richmond bado leo hii tunaanza kuja na excuses za kuanza kuwaonea hawa watu huruma?

Kweli Tanzania yetu hii ni nchi ya kipekee, hii ndio inafanya watu wakose imani na serikali ya kikwete kwa kumbatia hawa mafisadi na wala rushwa kwa kuanza kujenga hoja zisizoeleweka hata kwa mwananchi wa kawaida...!
 
Kama kweli ufisadi hautakwisha Tanzania basi wakulaumiwa ni Watanzania na si mwingine yeyote.
 
Well,

Watu wengi wamezungumza mambo mazuri lakini issue inabakia ni jinsi gani tunaweza kuwafikia mamilioni ya watanzania na kuwapa elimu ya kufungua akili zao na kuanza kufikiri kama watu na sio kukupelekwa pelekwa na mbinu na hadaa za CCM.


Mwanakijiji nadhani ameonyesha mfano kwa kuanzisha kijarida cha cheche, ila nadhani kuna mambo mengine muhimu ili nia na sababu ya kuanzisha ifanikiwe

1. Circulation inabidi iwe kubwa sana kwa kila tolea ina maanisha watu zaidi wakujitolea kuchapa/print and kuvisambaza

2. Mwelekeo wa content inabidi uwe ni wa kuamsha fikra zaidi kwa level ya wazee wetu wa vijijini rather than kuendelea kulisti mambo ya ufisadi ingawa sio vibaya kuendelea kuyaongelea.

3. Nikiongelea zaidi kuhusu content, mara nyingine ni vizuri kujua hali halisi ya mahali kama ni wilaya, kata, kijiji na kuangalia hali ya shule, zahanati na huduma nyingine zikoje kwa sasa.......na kuwaeleza kinagaubaga wananchi kiuhalisia hali ilitakiwa iweje even kwa kulinganisha na sehemu nyingine humu humu Tanzania. Mfano ...tunajua kama wakati CCM iliyoogonza karibu miaka 40 walikuwa na shida kubwa ya maji lakini baada ya Dr. Slaa kuchukua jimbo amejitahidi sana kuondoa hiyo shida zaidi kwa juhudi binafsi kama mbunge anayewajibika kwa watu wake.


Kwa leo yangu ni hao
 
Rev. Kishoka,
Wewe ni mmoja katika ya wana-JF ambao ninaushawishi nao mkubwa katika ujengaji wa hoja na ufikishaji wa fikra zako kwa wengine. Katika postings zako nimekuelewa kuwa wewe siyo shabiki wa kutoa hoja zaidi ya kuamini kile ambacho unakielewa kutoka katika mawazo yako, in short wewe ni mtu wa mfano katika nyanja ya majadiliano.
Napenda kukiri kuwa japo ninakukubali katika upande huo lakini kama binadamu wa kawaida huwa pia ninatofautiana nawe kwenye masuala mengine, japo si lazima niwe nimechangia moja kwa moja.

Katika hoja yako iliyopo mbele yetu hapa ninapenda kusema kuwa baadhi yetu sisi watanzania hatuna mikakati endelevu katika kukabiliana na issues tofauti. Tuna hulka ya kutaka 'short cut' kwa kila jambo na hii imekuwa ni tabia iliyojijenga ndani ya mioyo yetu. Kwa mfano

-Tunapomaliza chuo, tunataka tupate kazi ambayo 'tutatengeneza' pesa ya haraka, matokeo yake ufanisi haupatikani na zaidi ya hapo ni wizi na rushwa.

-Tunapopatiwa coach katika vilabu vyetu vya mipira au hata timu ya taifa, tunataka tupate ushindi kwa hali yeyote bila ya kujali kama tunahitaji kupata vipaji na kuvifundisha (kwa maana ya kuwekeza).

-Tunahitaji siasa za ushindani, tunahitaji chama/vyama vya ushindani vya kubalance power/kuiondoa CCM madaraka. Badala ya kuwekeza katika base ambayo italeta ufanisi wa kufikia malengo, tunaona viongozi wa kisiasa hasa vyama vya upinzani wanatumia resources nyingi kutafuta njia ya kwenda Ikulu. Huko Ikulu kuna nini?

Mimi ninashauri vyama shindani vya siasa vichukue mawazo ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime hayati Wangwe na kuyatumia kama dira ya kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa katika nchi hii. Vyama havina budi kutumia resources zao nyingi katika kujengea uwezo wananchi wa chini kabisa waelewe mfumo halisi wa demokrasi nchini. Hii itawawesha wao kufanya maamuzi yaliyosahihi inapofika katika masuala ya kupiga kura na uendeshaji wa mamlaka zao.
Katu mimi sitaunga mkono kiongozi yeyote sasa hivi wa upinzani anayetaka tumbebe aende Ikulu ilhali huku chini hajaweka mambo sawa.

Tujenge na kuimarisha msingi wa demokrasia, Ikulu baadae.
 
Pundamilia,

Kwa ulichoandika kama ndivyo unadai tunapingana mawazo mbona umekosea sana?

Maana ulichoandika ni njia fupi na ya namna ingine ya kuwasilisha ujumbe ambao nimekuwa naupigia kelele siku zote.

Umelenga sawa kwa kusema kuwa tunapenda short cut, ndio hizo short term goals for short tems solution. Mtu anapata shahada Chuo Kikuu, anajiona kuwa sasa anastahili mshahara mkubwa baada ya kusota miaka minne UDASA, anajiona yeye ni mtaalamu, kwa kuwa ana elimu ya nadharia.

Kaja Maximo, tunafikiri tutashinda kombe la dunia kesho na tunalazimisha ushindi upatikane mara moja.

Lakini pamoja na mifano hiyo ya kuonyesha tunavyotaka matokeo ya haraka, linapokuja suala la Uongozi na hasa katika tija na ufanisi katika kuleta maendeleo ya watu, jamii na Taifa, hilo halina msamaha wa kusema ngoja nijifunze au tujipe muda kuleta yanayotegemewa hasa ukizingatia kuwa ni Chama kimoja na watu wale wale wamekuwa katika duru za uongozi.

Leo hii kuna watu wanaamini tumpe Kikwete muda zaidi. Sasa angefaa apewe muda zaidi kama japo angeonyesha umakini katika kazi yake. Sasa tujiulize, tutampaje muda zaidi ikiwa yeye amekuwa katika Serikali kwa miaka 25 kabla ya kuwa Rais wa Jamhuri? Je miaka yote hakujifunza Uongozi na kuangalia wenzake waliotangulia?

Wengine mtasema yeye ni mgeni kama MWenyekiti wa CCM. Lakini Kikwete si alianza kazi kama kada wa chama, akiwa katibu wa chama Singida, je alishindwa kujua jinsi ya kuongoza chama cha siasatangui ngazi ndogo kama wilaya?

Hata tukimgeukia Pinda, Karume, Lowassa na wengine, wamekulia katika mfumo mmoja, ambao una sera, falsafa na itikadi moja. Iweje washindwe mpaka leo kupiga vita Ujinga, Umasikini na Maradhi na badala yake kukimbilia shot cuts na kuziona ndio tiba na kinga ya matatizo ya Tanzania?

Mimi na wewe hatupingani kimawazo katika hili, bali ni uwasilishaji wetu umekuwa na tofauti kidogo tu.

Nafurahi kuwa unachukua muda kusoma na hata kunipa wasifu kama uliousema.
 
Rev. Kishoka,

Mkuu hoja yako nzito sana na ina mwamko mzuri sana isipokuwa tu mkuu wangu kuna kitu kimoja ambacho nitakufahamisha hapa.Kumbuka maneno yangu kwamba kila unapofikiria jambo linalohusu mustakabali wa nchi yoyote ile ni muhimu kutazama vitu hivi viwili... WATU na MAZINGIRA yao...

Tatizo la Tanzania sio viongozi peke yake ni pamoja na raia wake kwani sisi na hao viongozi hatuna tofauti yoyote zaidi ya kwamba wao wamekalia viti na kulia mezani wakati sisi tumetandikia janvi na kusukumiwa sahani la Pilau..Hapo mikono mingi kila mmoja wetu anawahi pande la nyama lililofukiwa ndani ya pilau..Jaribu kujiuliza kwa nini ktk mapishi ya pilau nyama hufukiwa badala ya kukwa juu ama kando ili kila mmoja wetu apate kipande chake...

haya ndiyo makuzi yetu sisi tumekuwa tukiishi maisha ya kimaskini hivyo hata mbinu zetu hutazama kile kilichopikwa kuweza kuupumbaza umma...
Tatizo moja kubwa mabalo hadi sasa hivi naliona ni kwamba sio kweli Umma haufahamu bmabaya ya Uongozi wetu isipokuwa wananchi wamebanwa na Umaskini wa hali na mali..hivyo resoning yao inakuwa mbali sana kwanza shibe na CCM wanafahamu vizuri kwamba sisi tuna jaa...
Tactic ni ile ile kuuweka mpunga wa pilau (jina kubwa) kama vile madini sote mioyo yetu itapendekeza kuona madini yetu yakichimbwa hali ndani ya madini hayo hakuna nyama isipokuwa vipande vichache sana ambavyo haviwezi kutosheleza. Huko ktk meza yao ndio kuna nundu, vitu vya ndani na nyama zimewekwa ktk sahani ya pekee wakila huku wakipiga soga. Sisi midomo imejaa mpunga mkono mmoja una pande la nyama mwingine unaenelea kufukua pilau.. by the time pilau limekwisha hakuna aliyeshiba..Kwa upande wao viongozi hakuna anayetaka kuondoka juu ya meza hiyo kurudi ktk janvi lisilo kuwa na mwaliko, hivyo ni lazima uonyeshe umuhimu wake kubakia hapo mezani..hakuna mtu anayetaka kwenda kupigania pilau janvini mkuu wangu.

Sasa waangalie vizuri kundi la watu waliowekwa janvini?.. ni wale wasiokuwa na matumaini ya kesho majumbani mwao, hawana mbele wala nyuma yaani maisha yao yanaendeshwa kwa kudra za Mungu na ndio asilimia 80 ya Watanzania - hao wakulima na wafanyakazi.

Mimi nina hakika kabisa kwamba wananchi kufikia leo hii wanafahamu fika kwamba CCM mazishi lakini ndiye pekee huandaa pilau la Hitma la uhakika...
Kama umekwisha hudhuria mazishi Bongo utaamini maneno yangu kwamba kila mazishi ya mtu maarufu ambaye sio tu anapendwa kwa mapenzi ila wananchi wanafahamu mpunga wa nguvu utakuwepo ndiye atapata mazishi makubwa sana pamoja hata kama alikuwa jambazi, mtovu wa adabu ama mtu mwema sana...Majonzi yao hubadilika kuwa furaha na naweza kusema ni wakati mdogo sana Watanzania tumekuwa na majonzi ya kweli kuondokewa na viongozi ambao uzuri wao umekuja onekana baada ya wao kuondoka..

Ni hulka yetu kushabikia matumbo yetu kwanza kabla ya reasoning na ndicho kinaendelea hadi kesho. Wapo watu humu ndani ya JF wanaoshabikia sana baadhi ya viongozi kwa sababu tu ndio wanaowapa kula yao. Wapo wanaoshabikia CCM kwa sababu tu ndio kula yao au pengine kuna matumaini ya pilau bila kuwepo kilio. Ni hulka utaikuta misikitini, makanisa, majukwaa ya miziki (Papa pedejee)na hata magari yanapoegeshwa. Hawa watu hubabaikiwa sana hata kama wana sura mbovu kama ukuta.
Kikwete binafsi nilikuwa na tumaini naye japo kuwa nilikuwa na mashaka hasa baada ya kusikia kundi lake toka kwa Field Marshall Es...na ajabu sio kwamba sikufahamu kuna kundi baya la watu kina Mkapa ambaye amesifika sana nchini hali ktk taarifa yako hapo juu imeonyesha wazi ndiye chanzo cha mikataba mibovu..
Siwezi kusema sikuwa na mwamko wa kifikra kuweza kujua kwamba CCM haifai kabisa isipokuwa nilidhani ndani ya CCM wapo viongozi ambao wanapiga vita uongozi wa Mkapa na sera zake...Kikwete akiwa mmoja wao na kama unakumbuka lipongezwa sana kwa hutuba yake ya kwanza Bungeni..Lakini ndio kama hivyo Kikwete ndio kaondoa kabisa zile life support za maisha ya mama yetu Tanzania...

Kwa hiyo kuu wangu ni kazi nzito sana kuwafahamisha Watanzania wenye njaa hasa kama hakuna sahani la Pilau...watu kusubiri hadi kifo cha CCM inatakiwa kuwepo mwanga wa kuhitmisha kiasi kwamba hawa WATU wananchi ambao leo hii wapo ktk MAZINGIRA magumu wapate kuona mpunga utakuwepo...Na hii sio kazi itakayo fanywa kwa mdomo tu ila ni vitendo vidogo vidogo ambavyo vitaweza kujenga jina la chama ama jumuiya inayotaka mageuzi. Watu kama Castrol wameonyesha uwezo wao wa kuongoza kwa vitendo ttoka chini wakiwa hawana madaraka. Vyombo kama Hezbullah kule Lebanon vimepata sauti na nguvu kubwa kutokana na misaada yao midogo midogo ktk jumuiya zao na pengine wanayafanya makubwa kwa masikini kuliko hata serikali yenyewe...Kumbuka pia hadithi za mitume wetu walifanya maajabu kwanza kuwavuta waumini wao kabla ya kuwapa neno la Mungu...Yesu aliweza kugawa samaki na mvinyo kwa wavuvi waliokwisha kata tamaa...from there alivuta watu.

Sasa basi ili ushindi upatikane dhidi ya mafisadi sii rahisi kutumia maneno matupu, pale hawa mafisadi wamepasahau (huko vijijini) sisi wanamapinduzi tunatakiwa tuziweke nguvu zetu kwa vitendo. Pasipokuwa na shule au Hospital sisi tuwafikie watu hao..hakuna pembejeo za ukulima sisi tufikishe pembejeo hizo hata kama itabidi sisi tuingie mashambani na kulima.
Ni kwa mifano kama hii ndipo wananchi wanaweza akuona tofauti kati ya sisi na huyo fisadi akipima uwezo wako mdogo umeweza kuwaondolea hata kiu cha maji... Ni katika hatua kama hizo maskini mwenye njaa anaweza kuona ama kupima uwezo wako laa sivyo mkuu tutasema hadi kiyama hakuna mtu atakaye pokea mkono mtupu ambao waswahili wanasema haulambwi.
Nina hakika hasa kwa sisi watu tunaoishi nchi hizi kuna vifaa vya mahospital ambavyo kama utaenda kuomba ktk hospital kubwa utapatiwa kwa sababu wao hubadilisha kila mara..Ujenzi wa zahanati ndogo ndogo vijijini sio kazi kubwa ikiwa NGOs zinasajiliwa kila siku..Dawa itatoka ktk misaada yetu hii..nakumbuka sana ndugu yangu Taasisi alikuwa akisisitiza sana kuona vyama vya Upinzani wakifanya vitu kama hivi lakini hadi leo naona kama vile the main plan ya mafanikio ya vyama hivi ni kukipaka tope tu CCM, hali wao mikono mitupu...haiwezi kusaidia kitu...

Kwa hiyo mkuu wangu sio kwamba napinga kuwaelemisha wananchi lakini nadhani elimu hiyo itanguliwe na kuwapa shibe hawa maskini ili wapate nguvu ya hata kusikiliza hizo hotuba laa sivyo watakuwa wanalala usingizi na kuitikia kama vile wanakuelewa kumbe mawazo yao yote yapo ktk kuweka kipande cha mkate mezani kwa familia zao. Waswahili husema mazungumzo huja baada ya shibe!
 
Pundamilia,

Kwa ulichoandika kama ndivyo unadai tunapingana mawazo mbona umekosea sana?

Maana ulichoandika ni njia fupi na ya namna ingine ya kuwasilisha ujumbe ambao nimekuwa naupigia kelele siku zote.

Umelenga sawa kwa kusema kuwa tunapenda short cut, ndio hizo short term goals for short tems solution. Mtu anapata shahada Chuo Kikuu, anajiona kuwa sasa anastahili mshahara mkubwa baada ya kusota miaka minne UDASA, anajiona yeye ni mtaalamu, kwa kuwa ana elimu ya nadharia.

Kaja Maximo, tunafikiri tutashinda kombe la dunia kesho na tunalazimisha ushindi upatikane mara moja.

Lakini pamoja na mifano hiyo ya kuonyesha tunavyotaka matokeo ya haraka, linapokuja suala la Uongozi na hasa katika tija na ufanisi katika kuleta maendeleo ya watu, jamii na Taifa, hilo halina msamaha wa kusema ngoja nijifunze au tujipe muda kuleta yanayotegemewa hasa ukizingatia kuwa ni Chama kimoja na watu wale wale wamekuwa katika duru za uongozi.

Leo hii kuna watu wanaamini tumpe Kikwete muda zaidi. Sasa angefaa apewe muda zaidi kama japo angeonyesha umakini katika kazi yake. Sasa tujiulize, tutampaje muda zaidi ikiwa yeye amekuwa katika Serikali kwa miaka 25 kabla ya kuwa Rais wa Jamhuri? Je miaka yote hakujifunza Uongozi na kuangalia wenzake waliotangulia?

Wengine mtasema yeye ni mgeni kama MWenyekiti wa CCM. Lakini Kikwete si alianza kazi kama kada wa chama, akiwa katibu wa chama Singida, je alishindwa kujua jinsi ya kuongoza chama cha siasatangui ngazi ndogo kama wilaya?

Hata tukimgeukia Pinda, Karume, Lowassa na wengine, wamekulia katika mfumo mmoja, ambao una sera, falsafa na itikadi moja. Iweje washindwe mpaka leo kupiga vita Ujinga, Umasikini na Maradhi na badala yake kukimbilia shot cuts na kuziona ndio tiba na kinga ya matatizo ya Tanzania?

Mimi na wewe hatupingani kimawazo katika hili, bali ni uwasilishaji wetu umekuwa na tofauti kidogo tu.

Nafurahi kuwa unachukua muda kusoma na hata kunipa wasifu kama uliousema.

Rev. Kishoka,
Awali ya yote naomba nikupe pole kwa kunielewa tofauti kwenye posting yangu iliyopita. In fact niliona nina wajibika kusema kuwa mimi na wewe tunatofautiana katiaka masuala mengine kama binadamu wa kawaida. Hii note ilikuwa ni muhimu sana ili isije ikaleta dhana potofu kutokana my personal observations nilizokuwa nimezitanguliza. Kuna nyakati kama hufanyi jambo kama hilo unaweza ukamletea usumbufu mlengwa. Lakini mantiki kubwa pamoja na kukukubali haikuwa na maana kuwa siwezi kutofautiana nawe. Nafikiri Rev. utakuwa umenielewa.
Katika hili ambalo umelianzisha kimsingi ninakubaliana nawe na ndiyo maana nimekazia kwa kutoa maelezo ambavyo tunataka kuleta mabadiliko kwa kutumia short cut. Napingana na dhana nzima ya wanasiasa ya kutaka kwenda Ikulu kwani hiyo siyo suluhisho la kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanzania. Well, on the other side I have no problem na Rais aliyekuwepo madarakani, tatizo langu hata akiwekwa Rais mwingine awe mzuri kuliko aliyekuwepo sasa hivi itakuwa kazi bure kama opposition haina mikakati ya kubalance power katika nchi hii. Nashindwa kuelewa tatizo kwa opposition ni nini? ni tamaa? au kuna biashara inayofanyika Ikulu? Kazi ya msingi ya opposition ni kujenga base ambayo ndiyo itakayoleta changamoto katika siasa za ushindani. Leo hii tunaikejeli CCM lakini tunasahau kuwa nguvu waliyonayo wameipata kutoka kwa wananchi kupitia sanduku la kura. Kwahiyo wananchi ndiyo wenye nguvu na wanaoweza kuamua hatima ya nani awe madarakani. Opposition bado inafikiria kuwa kuunda vyama kutengeneza sera na kusubiri uchaguzi mkuu ndiyo njia ya kubadilisha/ kuleta siasa za ushindani, kama mawazo yao ndiyo hayo basi kila siku watakuwa na kazi ya kuijibu CCM hadi vyama vyao vinakufa! Ni lazima ijulikane plan B ni ipi, kama ulivyosema kuwa hawa jamaa wamegombea kwenda Ikulu tangu 1995 bila ya mafanikio.
Naomba niwe mkweli kabisa, mwenendo wa opposition sasa hivi unakiimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kadri siku zinavyokwenda, pia isisahauliwe kuwa CCM is big, tough na ina watu wengi wazuri na wabaya. CCm ina uwezo wa kujibadilisha kadri siku zinavyokwenda.
Narudia kusema kuwa Vyama vya siasa vya Tanzania vijiimarishe ili kufikia kiwango cha kubalance power kwa kufanya hivyo huenda pia tunaweza kuona mabadiliko makubwa katika utendaji wa serikali.
 
Pundamilia,

Kutofautiana mawazo ni ubinadamu na ni demokrasia.

Kwenye hili la viongozi wa Tanzania, mategemeo ya Mtanzania alipomchagua Kikwete yalikuwa ni kuanza kuamka kwa maisha yake kwa kauli za Ari, Nguvu na Kasi mpya.

Lakini Kikwete na CCM hawakutuambia Ari, Kasi na Nguvu mpya zilikuwa zimelekezwa kwenye kitu gani!

Sasa ni jukumu letu sisi kama Taifa si kutegemea Serikali na Vyama vya siasa kutuongoza au kutupa mwamko wa kujiendeleza na kuwa huru.

Ni jukumu letu wenyewe, kuanzia nyumbani, mtaani, kijijini, kata, tarafa na hivo injili ya Maendeleo kusambaa kwa Wilaya, Mkoa hata Taifa.

Siku Mtanzania atakapokuwa huru wa mawazo, fikra na kuamua na zaidi akawa ni mwenye uwezo wa kujitegemea na si kutegemea mtu au kushawishika kutokana na unyonge na umasikini, ndio siku Wanasiasa wa Tanzania wataamka na kuanza kufanya kazi zao kama wanavyopaswa!

Nimeanzisha mada hii ili kuwakumbusha ndugu zangu kuwa tusiendeleze makosa ya kudhani kuwa kupigia kelele Ufisadi ndio njia pekee ya kuing'oa CCM na kuleta mabadiliko nchini.

Ufisadi ni tatizo moja ambalo ni gonjwa limeushambulia Uongozi wa Tanzania.

Lakini kuna magonjwa mwengine mengi kama Kutowajibika, Ufanisi mdogo, Uzembe, Uvivu, kukosa Ubunifu, Ufuatiliaji mbovu, nidhamu mbaya ya kazi, ufujaji mali na mengine mengi ambayo si kuwa yameukumba Uongozi tuu, bali yamesambaa hata kwa Wananchi!
 
Mkandara amelisemea vizuri sana hili.

Tatizo la sisi Watanzania,hata tulio humu ni umaskini.Mtanzania kila siku anakumbushwa kuwa yeye ni maskini.Kila saa anaambiwa kuwa serikali haina pesa...haina pesa za kuwa na madawa kwenye zahanati,madawati mashuleni,pembejeo kwa wakulima,kuwalipa mishahara on time walimu etc.Lakini hapohapo anamuona waziri anatembelea gari mpya lenye gharama ya zaidi milioni 120,wakati lile la zamani ni zuri sana tu,billions zinaenda kukarabati ikulu na nyumba ya waziri mkuu

Maana hata nyumbani,watoto wako wakijua kuwa baba ni maskini,na kila saa unawakumbusha,basi hata hela ya pipi wataogopa kukuomba,watajiridhisha tu kuwa wewe ndio baba,na unachokula wewe ndio wanaokula wao.Sasa kama baba kuna siku ukakata dili,lakini ukafanya siri kwa mke na watoto,ukaonekana kwenye bar unatumia,wakigundua watapiga kelele.Watapiga kelele za njaa na hasira.

Watanzania tunapiga kelele za njaa tu!Hatuna hasira,tusijidanganye.Wenye hasira tumewaona,angalia Kenya,Malaysia,Nigeria jinsi wanavyolipua oil pipelines kila siku,kwamba kama kupata tupate wote na pia kama kukosa, basi tukose wote.
Leo nimesoma kwenye gazeti la This Day kuwa Gaddafi anataka pesa zinazopatikana kutokana na mauzo ya mafuta ziende moja kwa moja kwa wananchi.Libya ina watu milioni tano,na inazalisha pipa milioni 3 kila siku,kijuujuu ni kwamba kila mtu ana nusu pipa la mafuta kila siku!


Serikali inasema kuwa katika miaka 5 imekusanya 78m dollars kutokana na mauzo ya dhahabu yote inayochimbwa nchini.
EPA imekwapuliwa 133m dollars in three years! Imagine this, kuwa watu wajanja wakishirikiana pamoja na viongozi wachache wameiba pesa nyingi katika miaka mitatu kuliko mauzo ya dhahabu ya nchi nzima ya miaka mitano nchi ambayo ni ya tatu kuwa na dhahabu nyingi Africa..to make it worse,wamesamehewa! Walioiba simu,kuku wanasota jela

Moja kati ya solutions ambazo mimi naona ni kwamba,kama nilivyosema kwenye post moja huko nyuma,this country needs a complete overhaul....gradual overhaul.Sio mambo ya reshuffle.Since it seems kuwa we are stuck with CCM for the forseable future,within CCM the majority are not happy with whats going on.Kwa sababu,majina tunayoyasikia kila siku ni yaleyale,Rostam,LOwassa,Karamagi.Sasa hayo ambayo hatuyasikii ya hao wasiopenda ni mangapi? Ni mengi sana,lakini uoga/umaskini unawafanya wakae kimya.They need to recruit the youth! Achana na Umoja wa Vijana wa CCM....hawa ni walewale 'yange..yange nipe kucha nyeupe na mi ntakupa nyeusi....' old nursery rhyme.Vijana wawape mwamko mpya..wawaamini,wawagroom,kama ilivyokuwa inafanyika zamani.This country has a serious lack of patriots within the upper echelons of power.

Pia,kuna umuhimu wa kurudi kule kwa zamani ambako wabunge kweli wanatoka na kuishi kwenye majimbo yao.Sio mtu Mjita lakini kaishi maisha yote Dar,then anarudi Majita kununua nyumba haraka kuonyesha kuwa anaishi huko.Hawa wa sasa hawana uchungu na majimbo yao au watu waliowachagua,they have hidden agendas,na njia rahisi ndio hio thru ubunge.Tukipata wabunge wengi ambao kweli wanawajua watu wao vizuri,wanaishi nao kweli hata kuiba wataona vibaya na muda watakosa,lakini swali ni hili,je Zanaki akisimama na Rasta Aziza ambaye ataleta pilau na sherehe na pesa za kugawa,huyo Zanaki atashinda kwa hoja tu?
Ni kwenye majimbo machache sana ambapo hilo linaweza kutokea.Tuliona yalitokea hapa Dar wakati NCCR iliposhinda Ubungo,CUF ikashinda Kigamboni etc.Lakini toka hapo,we have been sitting in the drivers seat facing forward while our eyes are permanently glued to the side mirrors!
 
Revd, kwani Radio ya Mwanakijiji haiwezi kutoa matangazo kupitia Redio za Kawaida? Nakumbuka wakati wa Mapambano ya ukombozi huko Kusini ya ANC na SWAPO, RTD ilikuwa inarusha matangazo Namibia na Afrika Kusini.

Kama njia hiyo ikiwezekana, WaTz watapata elimu kubwa kujua kinachoendela nchini na hasira zao watazitumia 2010
 
jamani hivi tanzania watu wanaona yanayotokea nchi kama thailand sasa. Au hawapati habari za dunia
 
Watanzania waoga kuchafuka, fukuto kila likitokea kwa wengine, tunafumba macho kwa woga.

Siku tukiachana na huo woga, walioko madarakani wakae chonjo!
 
Tatizo la Tanzania sio viongozi peke yake ni pamoja na raia wake kwani sisi na hao viongozi hatuna tofauti yoyote zaidi ya kwamba wao wamekalia viti na kulia mezani wakati sisi tumetandikia janvi na kusukumiwa sahani la Pilau..Hapo mikono mingi kila mmoja wetu anawahi pande la nyama lililofukiwa ndani ya pilau..Jaribu kujiuliza kwa nini ktk mapishi ya pilau nyama hufukiwa badala ya kukwa juu ama kando ili kila mmoja wetu apate kipande chake...

haya ndiyo makuzi yetu sisi tumekuwa tukiishi maisha ya kimaskini hivyo hata mbinu zetu hutazama kile kilichopikwa kuweza kuupumbaza umma...
Tatizo moja kubwa mabalo hadi sasa hivi naliona ni kwamba sio kweli Umma haufahamu bmabaya ya Uongozi wetu isipokuwa wananchi wamebanwa na Umaskini wa hali na mali..hivyo resoning yao inakuwa mbali sana kwanza shibe na CCM wanafahamu vizuri kwamba sisi tuna jaa...
Tactic ni ile ile kuuweka mpunga wa pilau (jina kubwa) kama vile madini sote mioyo yetu itapendekeza kuona madini yetu yakichimbwa hali ndani ya madini hayo hakuna nyama isipokuwa vipande vichache sana ambavyo haviwezi kutosheleza. Huko ktk meza yao ndio kuna nundu, vitu vya ndani na nyama zimewekwa ktk sahani ya pekee wakila huku wakipiga soga. Sisi midomo imejaa mpunga mkono mmoja una pande la nyama mwingine unaenelea kufukua pilau.. by the time pilau limekwisha hakuna aliyeshiba..Kwa upande wao viongozi hakuna anayetaka kuondoka juu ya meza hiyo kurudi ktk janvi lisilo kuwa na mwaliko, hivyo ni lazima uonyeshe umuhimu wake kubakia hapo mezani..hakuna mtu anayetaka kwenda kupigania pilau janvini mkuu wangu.


Kwa hiyo mkuu wangu sio kwamba napinga kuwaelemisha wananchi lakini nadhani elimu hiyo itanguliwe na kuwapa shibe hawa maskini ili wapate nguvu ya hata kusikiliza hizo hotuba laa sivyo watakuwa wanalala usingizi na kuitikia kama vile wanakuelewa kumbe mawazo yao yote yapo ktk kuweka kipande cha mkate mezani kwa familia zao. Waswahili husema mazungumzo huja baada ya shibe!

Mkandara,

Sisihemu si wameshatuwahi kugawa Kipunga kila mara na hivyo watu wameshafanya mazoea?

Mbinu ninayoifanyia utafiti si hotuba tena, bali ni vitendo ambavyo vitamfanya Mtanzania atamani kuwa Huru wa mawazo, fikra na kuamua mambo na kukubali na kuhimili maisha ya kujitegemea.

Sasa kama leo hii, kuna watu wasomi na akili zao wanasifia safari ya 8 ya JK kuomba misaada, kazi ya kumbadilisha mawazo Mtanzania itakuwa ngumu mno, na inahitajika ifanyike kwa haraka.

Kama nilivyosema, kelele za ufisadi ni sawa na kutumia Ubua kumuua Tembo, tubadilishe fomati, wao wanakimbilia 4-4-2 sisi tuende na 3-5-2!
 
Mkandara amelisemea vizuri sana hili.

Tatizo la sisi Watanzania,hata tulio humu ni umaskini.Mtanzania kila siku anakumbushwa kuwa yeye ni maskini.Kila saa anaambiwa kuwa serikali haina pesa...haina pesa za kuwa na madawa kwenye zahanati,madawati mashuleni,pembejeo kwa wakulima,kuwalipa mishahara on time walimu etc.Lakini hapohapo anamuona waziri anatembelea gari mpya lenye gharama ya zaidi milioni 120,wakati lile la zamani ni zuri sana tu,billions zinaenda kukarabati ikulu na nyumba ya waziri mkuu

Maana hata nyumbani,watoto wako wakijua kuwa baba ni maskini,na kila saa unawakumbusha,basi hata hela ya pipi wataogopa kukuomba,watajiridhisha tu kuwa wewe ndio baba,na unachokula wewe ndio wanaokula wao.Sasa kama baba kuna siku ukakata dili,lakini ukafanya siri kwa mke na watoto,ukaonekana kwenye bar unatumia,wakigundua watapiga kelele.Watapiga kelele za njaa na hasira.

Watanzania tunapiga kelele za njaa tu!Hatuna hasira,tusijidanganye.Wenye hasira tumewaona,angalia Kenya,Malaysia,Nigeria jinsi wanavyolipua oil pipelines kila siku,kwamba kama kupata tupate wote na pia kama kukosa, basi tukose wote.
Leo nimesoma kwenye gazeti la This Day kuwa Gaddafi anataka pesa zinazopatikana kutokana na mauzo ya mafuta ziende moja kwa moja kwa wananchi.Libya ina watu milioni tano,na inazalisha pipa milioni 3 kila siku,kijuujuu ni kwamba kila mtu ana nusu pipa la mafuta kila siku!

Zanaki,

Ndio maana nimesema, Mtanzania inabidi aanze kutafuta uhuru wa mawaz, fikra na kujitegemea na kukwepa misaada, kama anataka kujikwamua kutoka unyonge. Ni hasira za kuwa masikini na mjinga zitumike kwa uchanya wa kujibidiisha na kujituma ili apunguze utegemezi.

Kwa kuwa kikubwa kwa sasa ni kufuta umasikini, ukisha ukabili umasikini, ni rahisi kuuhinda ujinga na maradhi. Lakini tukitegemea eti tushinde ujinga, wakati hatuna nyenzo au motisha ya kutosha kufanya kazi na kujipatia kipato bora na kuushinda utegemezi, elimu yetu ni bure huku tukiwa masikini!

Ndicho tulichofanya kama makosa kukimbilia kuisomesha na kudharau kabisa shughuli hata zile duni (primitive) za kuzalisha mali ili kuwa na msingi imara wa kujitegemea!
 
Back
Top Bottom