Why "Vita vya Ufisadi" failed and will never win election.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Why "Vita vya Ufisadi" failed and will never win election..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Aug 31, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Watanzania tumekumbwa na bumbuwazi baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni mwishoni mwa mwezi. Ukweli ni kuwa tusishangae tuliloliona au lililotokea, lilipangwa litokee hivyo baada ya sisi "wapiga kelele" kupimwa na kuonekana kuwa Mtanzania kamwe hatachukua hatua zaidi ya kulalamika.

  Kosa kubwa tulilolifanya na tunaendela kulifanya ni kudhani kuwa tukiongelea ufisadi kwa nguvu zote, basi mafisadi wataogopa, Serikali itawajibika na CCM itatikisika. Hao tumecheza pata potea na ndio maana hata baada ya kufukua madhambi yote, hakuna hata mtu mmoja aliyefikishwa mahakamani na waliotuhumiwa wote sasa wanatudhihaki kiasi cha kusafishwa majina yao.

  Pamoja na alichosema Kingunge majuzi kuwa Wabunge wa CCM wanapotoka kuongelea ufisadi ni kauli ya kijinga na kipumbavu, lakini hiyo ndiyo hali halisi kuwa CCM na Serikali yake, havitishiki wala kuogopa vilio vya wanaodhulumiwa wanaotaka ufisadi ukomeshwe.

  Ni udhaifu huo huo kudhani kuwa kuongelea na kuukemea Ufisadi Tanzania tunakokufanya hapa JF na kumbi nyingine, ndiko kutaleta mabadiliko ya kungoa CCM, ndivyo vyama vya upinzani vilivyopotoka na kupoteza miaka 15 kujaribu kuing'oa CCM kwa kauli dhaifu za kulalama na si kuwa na sera za kimaendeleo kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye unyonge na umasikini ambao umemfanya aitegemee CCM na kuitumikia huku akidhulumiwa na kudhihakiwa.

  Ili kuleta mabadiliko ya kweli na kuing'oa CCM madarakani, inabidi tubadilishe mapigo na mbinu za medani.

  Kwanza inabidi tuanze kujijenga kumkomboa Mtanzania awe huru, huru wa mawazo, mwenye kujitegemea na kujivunia mali na ujuzi alionao. Kuna mtu anayejiita WUN humu ndani ambaye amesifia safari hii ya August 2008 kuja Marekani na kusema ni muhimu kuja kutafuta MISAADA!

  Tanzania ni nchi tajiri sana, kwa nini bado tunategemea Misaada? Ni lini tutaanza kujitegemea?

  Wanasiasa wetu na hasa hawa wa Awamu ya Tatu na ya Nne, wametuingiza katika mfumo wa uchumi huria bila kujiandaa kwa kuwa na uwezo mzuri wa uzalishaji mali hivyo kujenga Taifa linalojitegemea.

  Ni udhaifu wao wa Uongozi, Uvivu wa kufikiri na kubuni, Uvivu wa kuchapa kazi na kuwajibika na uzembe ulioandamana na ugoigoi ndio unaolea tabia ya kutegemea Misaada na wengine waje kutuokoa na kutuzalishia mali.

  Mwalimu Kichuguu kazungumza vizuri ni jinsi gani Awamu ya Kwanza ilifanya juhudi kujenga Taifa linalojitegemea pamoja na umasikini wa hali na mali tuliokuwa nao na kuachana na bidhaa za kuagiza. Serikali zilizofuatia zimeuza kila kitu kwa jina la Ubepari Uchwara, huku tukiongeza nguvu na juhudi za kuwa ombaomba.

  Ni kutokana na tabia ya kuwa tegemezi, ndivyo Mtanzania naye anaiga tembo kutoka Serikali na Wanasiasa wake na kuendekeza unyonge ambao unamfanya awe mjinga na masikini, asiye huru kufikiria na mwepesi kurubiniwa na msaada na takrima na hivyo kuendelea kukubali kuongozwa kwa kuchagua viongozi wabovu na kukitukuza chama kisichojali maslahi na maisha yake.

  Hotuba ya Kikwete na kauli ya Kingunge ni vitu tosha kutufundisha kuwa Mafisadi, hawatatikisika mpaka pale ambapo Uhai wa CCM kuendela kuwa chama tawala utakapoingia matatani na mashakani.

  Kwa kipindi cha mwaka mzima, hoja kuu hapa JF zimekuwa ni kupiga vita ufisadi. Anza Richmond, rudi IPTL, Rada, Ndege, Kiwira, TRC-TRL, Buzwagi, Karamagi na makontena, EPA, ATCL na mengine mengi ambayo hata ushahidi wa wazi upo, hakuna hata hatua moja imechukuliwa na Serikali na kiongozi mkuu amekaa kimwa huku akihuzunika kwa marafiki na wasaidizi wake wakituhumiwa na wananchi, lakini badala ya huzuni hiyo kuwa ni hasira ya kulaghaiwa na aliowaamini, ni huzuni kuwalinda!

  Inabidi tukae chini tutumie akili zetu vizuri na tusikubali kuingizwa mjini tena. Changa la macho limetupwa kwetu mara nyingi na tumeingia kichwa kichwa.

  Sina maana tukae kimya kuhusu ufisadi, bali natoa nasaha kuwa tusitegemee kuongelea ufisadi kuwa ndio njia pekee ya kupatikana mabadiliko Tanzania au kushinda uchaguzi.

  Hili si kwa JF pekee, ni kwa wote ambao wanataka mabadiliko ya kweli kwa Tanzania!

  Tujipange upya na kuanza kujiuliza, ni vipi kwanza tutaweza kumfanya Mtanzania awe huru na kujitegemea?

  Siku Mtanzania ni huru, mwenye uwezo wa kufikiri bila kurubuniwa na ana kiburi cha kujitegemea, ndipo siku hiyo ukombozi utawasili na harakati za kuing'oa CCM na kufikisha Ufisadi kwenye sheria zitafanikiwa.

  Kama tutashindwa kumpa Mtanzania huyu uhuru na kumjenga ajitegemee, basi ndoto za kuingoa CCM na kubweka kwetu kwa utaalamu kuhusu ufisadi ni kazi bure!

  Bob Marley alisema "emancipate yourselves from mental slavery" nami nawaambia wenzangu, "lets emancipate ourselves from mental dependency"!
   
 2. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yes in deed Rev.

  Tuji ng'ong'ozoe na tuwasaidie wenzetu (watanzania) kufanya hivyo kutoka kwenye UTUMWA huu wa fikra.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Ufisadi ni kesi ya tumbiri inayoamuliwa na nyani. Ili tuzamishe ufisadi, ni lazima tuhakikishe kuwa hakimu wa kesi siyo nyani tena. Sasa hapo ndipo ugumu ulipo kwa sababu ikifika wakati wa uchaguzi tu, khanga, kofia, t-shirt, pilau pombe na pesa zinatolewa hovyo hovyo kwa wanachoi ambao mwishoni hugawa kura zao bila kufikiri, tunajikuta na nyani kwenye kiti cha enzi tena.

  Umewahi kusikia wimbo huu uitwao Mr. Politician ulioimbwa na Nakaaya Sumari?
   
 4. T

  Thomas David Member

  #4
  Aug 31, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  For some elites in Tanzania whom they call themselves the leaders, the ruling elites, the government; admitting that they are off truck as far as leadership and accountability is concerned may be unthinkable, but the reality is undeniable that they are! In a sense, they are the agents or servants whom we charged to protect and keep the constitution - our agreement-, the rule of law and now they are caught in the vicious circle, they are dysfunctional, and definitely they are blind, leading us-the- clueless. It is the urgency of the moment in the history of the United Republic of Tanzania that has been overlooked deliberately for some reasons.

  The 21st of August 2008 was the day the President of the United Republic of Tanzania addresses the Parliament of Tanzania. It was the day of hope for every Tanzanian who believed in the course of good governance and accountability that the head of state in his address to the parliament is going to held accountable all those who have looted our economy and shredded away more than 130bn Tanzania shillings from the External Payment Account Arrears - Central Bank of Tanzania - BOT. This hope has been turned into despair by the highest office of the land.

  In his address, the President of the United Republic of Tanzania - Jakaya Mrisho Kikwete appealed to Tanzanian that those who had returned the money will not brought before the court of law but those who did otherwise will be. In contrast, the PresidentÂ’s statement on what legal action should be taken has been divided Tanzanian people into classes. There is no such a thing again that no one is above the law. The have not, the poor, the voiceless, the people, are now the victims of the law while the bureaucrats and bandits are not. The highest office of the land, the Presidents, the Commander in chief, have blessed that; unacceptable, and unconstitutional grounds.

  The entrusted body by the people for the people to oversee and ensure that the rule of law is abided by every citizen in the country is now negotiating with the bandits. Shame on them! But there is one hope still on our hands; the history have been written, be it tomorrow, next month, two or 10 years down the line, all who had blessed the crimes and those committed it; we will indeed bring them to the justice, and have our defaulted agreement, the constitution, the rule of law restored to the way it used to be. God bless Tanzania!  Cheers,  Thomas David
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tufanyeje sasa ndugu zangu? maana watanzania wengi mpaka sasa wanaamini kila kinachosemwa na viongozi wao!! Juzi walikuwa wanaandamana kuunga mkono hotuba ya Rais Kikwete Bungeni..!!:eek:
   
 6. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Thomas,

  We heard that, now what should be done by JK and his Government?. We need to give solutions sometimes.........
   
 7. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Tazama akili yako ilivyo, tazama hisia zako zilivyo, tazama unavyofanya majumuisho bila kuyasadifu, unaishia kulalama bila hesabu, hebu wewe akili zako zikoje? Rev. Kishoka;siku zote nimekuwa nikikuamini sana tena sana Mkuu, ila ni kwa nini siku zote umejikita kuibua hoja na mwishowe tunabaki hatuna majibu? ni kwa nini?

  Rev. Kishoka; naomba sasa uache kulaumu, naomba sasa tuelekeze sauti zetu 2010, tujue ni nani atakayeleta changamoto 2010, sisi tunaendelea kupiga kelele CCM wanaendelea kutupuuza na kutucheka, wanatuona matahira, machizi, si wanatujua sisi ni wanyonge siku zote.

  Rev. Kishoka; si kipindi cha kuusemeea moyo hapa, ni kipindi cha kuhakikisha tunampata mtu(kiongozi) atakayewaumiza kichwa CCM, na ndiyo maana nikamuhasa Mwenyekiti wetu wa CHADEMA(mbowe) ajiweke pembeni na kisha tunao watu walio tayari kukiuunga chama hiki Mkono,lakini la ajabu ile thread ilimalizika hapa bila hata wewe kutia mkono, najua ni kwanini, si unajua tena, utakubali kulaumiwe? utakubali kupigiwa simu na jamaa? lakini hizi ni nidhamu za uwoga
  .

  Rev. Kishoka;napenda nikuulize hebu tukimpata mtu kama MALANDO,akajiunga chama chetu na kuanza kukibomoa CCM si tunaweza kuwapata wabunge wengi? ama tukimpata MWAKYEMBE na wengine wengi tunaweza kubadili sura na mtizamo mzima wa upinzani.

  Rev. Kishoka; naomba usiendelee kulialia, hawa CCM wanatupuuza, watufanya wajinga ni kipindi cha kujiandaa 2010 na si vinginevyo, be carefully brother
   
 8. M

  Mavanza Member

  #8
  Aug 31, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania wala tusijidanganye, mimi naona kungoja 2010 ni kujidanganya tu. Inabidi tuanze ku-create awareness kwa watatnzania hasa wa mijini, na njia pekee ni kuandaa maandamano ya kila wakati na migomo pale palipo na uonevu. Nimewapenda sana waalimu, wafanyakazi wa sekta ya umma. Migomo na maandamano ndiyo njia ya kuandaa ushindi wa 2010.

  Sasa wito wangu ni kuwa wanaharakati wote watuunganishe tuingie barabarani hata kama hiyo itafanyika bila kibali cha polisi, na huo ndio utakuwa mwanzo wa ukombozi wa mtanzania. 2010 inatakiwa kwenda tu kumaliza kazi. Tukienda kiamani amani hivi hatupati kitu 2010 kwani CCM wana mbinu nyingi sana.

  Tuvuruge miji yetu. Ndivyo walivyofanya wenzetu pote duniani ambao mapinduzi yalileta maana.
   
 9. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Rev Kishoka, mimi nadhani tatizo sisi middle class and educated lot, tuko bust trying to survive! But I agree with one thing, we have to reach adn educate the people and arm them with information. That is the first thing. Nitakutumia PM...
   
 10. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lipo jingine ambalo linaweza kuonekana dogo lakini linafanya kazi...hata wale waliokuzunguka ambao huwa hawana hakika na kwa nini hawatoi nafasi kwa upinzani. Tuwaelimishe jinsi bunge linavyofanya kazi na umuhimu wa kuwa na kura nyingi za hapana katika maamuzi ndani ya bunge...hata km basi watamtaka huyo rais wa CCM:( basi wawape wabunge wa upinzani nafasi ya kuleta challenge bungeni.

  Ndugu zangu siku moja walikuwa wanalalamikia sana upinzani kwa kile wanachoamini wapinzani wakishinda basi Tanzania itakuwa uwanja wa vita km nchi jirani na hivyo tutajikuta wakimbizi...nikawauliza swali moja tu wapinzani watapata faida gani wakipafanya hapa uwanja wa vita? hawakuwa na jibu baada ya mjadala mrefu mmoja akasema lakini CCM wamesema hivyo na ndio maana huwa tunawapa Kura kuepusha shari...Kauli km hizi zipo nyingi miongoni mwa wadanganyika waliokata tamaa, waliojazwa hofu. Naamini km si wote walibadilika siku ile basi nusu yao. Simaanishi walihamia upinzani la hasha ikumbukwe Watanzania wengi si wanachama wa chama chochote ila ni wapiga kura
   
 11. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tufanye hivi....

  Moja. Kuelimisha Umma.
  Kwanza kuandaliwa Maandamano au Mikutano ya hadhara nchi nzima kufafanua jinsi Raisi na serikali yake inavyoshindwa kuchukua sheria dhidi ya wala rushwa na wahalifu. Hivi vyama vya upinzani nashindwa kuvielewa ni kwanini hawakurukia hii nafasi na kuanza kushindilia madai yao-wanasubiri nini (2010)?

  Hii kazi itahitaji fedha. Lakini wapo wafadhili ambao wako tayari kuona nchi ikielimishwa. Kwa mfano hawa wafadhili wanaochangia asilimia 40 ya Bajeti ya serikali na sasa hivi wanashikilia mchango wao watakuwa tayari kusaidia katika hili. Mimi niko-tayari kuwa wa kwanza kuomba huo msaada.

  Itaendelea....
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu IssayaMwita,


  Kosa la kutaka kuujenga malengo kushinda uchaguzi pekee, limefanyika mara tatu na halikufanikiwa. Anza 1995, 2000 na 2005, upinzani umekuwa ukiweka nguvu kuchukua urais kwa kuitukana CCM na kulalamika bila kujenga hoja nzuri za kimaendeleo ambazo zingeweza mzindua au kumuamsha Mtanzania kutoka usingizi.

  Ukweli wa mambo ni kuwa CCM wanafurahia sana hali ya Watanzania kuwa masikini, wagonjwa, wajinga, wanyonge na watu tegemezi, kinyume na imani ya CCM iliyojijenga tangu Azimio la Arusha.

  Ninapozungumzia CCM sina maana ya wakulima na wafanyakazi ambao wanatumika na kuburuzwa bila kujijua, nazungumzia lile tabaka la uongozi anzia uongozi wa vijijini mpaka Taifa.

  CCM wamejenga tabia ya ubabe na kunyanyasa watu kwa kutumia unyonge na umasikini wa Mtanzania. Ni kwa kutumia udhaifu huo, ndivyo CCM inavyoendelea kushika hatamu.

  Sasa kazi inayotukabili si kutafuta Mgombea,bali ni kutoa elimu ya kuimarisha Watanzania wawe huru na wenye kujitegemea ili waweze kuwa na uwezo wa kukataa kuburuzwa kiakili, saikolojia au kimali na tabaka la wanasiasa.

  Siku Mtanzania atakapoamka na kubainin kuwa ana uwezo kujitegemea na kujiamulia mambo bila woga au hofu, ni siku hiyo mapinduzi ya kweli yatatokea.

  Kama hilo la kuelimisha halitatosha, basi walichoamua ndugu zetu wa Pemba linaweza kutokea, watu wakachoshwa na kuamua kubadili mawazo. Lakini hili la kusubiri hasira ni hatari, maana itakapokuja serikali na chama kipya, Mtanzania atarudi kwenye tabia mbovu ya unyonge, umasikini na kukosa uhuru wa mawazo na uchumi.
   
 13. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Naomba usiiamshe asila yangu, naomba usiijaze akili yangu uoga, najua wewe hapa nyumbani haupo, najua umejikita sana kinadharia kuliko kujua hali halisi ya sisi watanzania wanyonge tunaoishi hapa nyumbani.

  Laiti ungepewa mabawa ukaruka mpaka hapa nyumbani(Mara-Tarime) ungenielewa sana na wewe ungekuwa mmoja wapo wa kujitoa maisha yako ili kizazi cha kitanzania kipone, haiwezekani Mchungaji sisi tuteseke na hii mitoto ya mafisadi ikineemeka, haiwezekani nakwambia.

  Tumeshasema haiwezekani!!! haiwezekani kamwe.

  Rev, Kishoka, wewe endelea kuvuta pumzi huko uliko na huko ukiyaandaa mazingira magumu ya wajukuu wako, unadhani kuna siku hawa mafisadi wataruhusu sisi watoto wa maskini tuwe na usemi? tutaendelea kupiga soga huku hii mibwenyenye ikila good time let we say no no!!!!,
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Aug 31, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka,

  ..nakubaliana na wewe kuhusu wananchi kuelimishwa kuhusu haki zao, na thamani ya kura zao.

  ..nadhani hayo mazungumzo na majadiliano yasiishie kwenye mtandao tu, bali yaingie mitaani --mijini na vijijini.

  ..i have also been thinking kuhusu hii dhana kwamba wapinzani waende vijijini.

  ..lakini kama hujaeleweka mijini hivi kweli vijijini watakuelewa?

  ..kumbukumbu yangu inaniambia Tanu ilianza mijini na kusambaa vijijini.

  ..Kaunda na Mugabe wote walianza kukataliwa na wananchi wa mijini.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Rev,

  Vita dhidi ya mafisadi vimeshindikana kwa sababu wote wanaongoza vita hivyo na wao pia ni mafisadi na wanajua fika kwamba ufisadi walioufanya unajulikana na hao mafisadi hivyo wakiwashughulikia ili kukidhi matakwa ya Watanzania dhidi ya mafisadi basi na wao wataanikwa hadharani.
   
 16. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..ya musa hayajatushangaza bado, tunasubiri ya firauni.

  ..i'm afraid it'll be too late.
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  IsayaMwita,

  Sikutishi ndugu yangu, bali ninakuwa mkweli na kubaini hali halisi. Kukaa kwa Mtanzania iwe ni Mugumu, Sirari, Malampaka, Micheweni, Reading, Tokyo au New York, hakuondoi ukweli ulioko kuwa mageuzi ya kweli kuleta mapinduzi yataanza kwa kumfanya Mtanzania awe huru wa mawazo na kuamua na kisha kujitegemea.

  Kukimbilia kuchagua sura ndiko kuliko waponza Watanzania 2005. Tulimchoka Mkapa, tukamkimbilia Kikwete kwa ajili ya sura.

  Uongozi ni sera na siasa, si sura au kukimbilia urais. Ushahidi tunao wazi wa mtu aliyekimbilia Ikulu na kazi inamshinda, sasa iweje nasi tuingie mkenge kwa mara nyingine na kulenga kukimbilia Ikulu na kuweka nguvu zetu katika maendeleo kwenye mwaka wa uchaguzi pekee?

  Hasira yako iweke katika kufundisha jirani zako maana ya kujitegemea na kufanya mamuzi kwa kutumia uhuru wa kufikiri na si kuburuzwa.

  JokaKuu the Serpent General,

  Watanzania kila kona ya nchi wanafahamu hoja za ufisadi. Watanzania wamesikia ni jinsi gani viongozi na wahujumu walivyotuhujumu na kama kawaida, wameendelea kuhusudu, uongozi wa kifisadi wa CCM. Mfano mzuri ni Kiteto, maandamano kuwaunga mkono Lowassa na karamagi na maandamano kuunga mkono hotuba hewa ya Rais wiki iliyopita.

  Sasa suala si vita ya kwenye magazeti au mtandao, bali ni vita vya mawazo na ndio chimbuko la kuanzisha mada hii na kutoa kauli kuwa kwa Tanzania kubadilika, itabidi kwanza Mwananchi abadilishe fikra na kuanza kuwa huru na kujenga juhudi kujitegemea.

  Wun kasifia misafara ya kwenda kuomba misaada inayofanywa na Kikwete, karibu 31% ya Watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi na kupiga kura ni wajinga (hawajui kusoma au kuandika), 52% ya Watanzania ni masikini wa kutupa. Sasa kazi si kupiga vita Ufisadi pekee, bali ni kumpa Mtanzania elimu na nyezo za kuondokana na Ujinga na Umasikini.

  Serikali na CCM wana sera ambazo wamezisema kwa miaka 45 kuwa ni muhimu kuondoa ujinga na umasikini, lakini sera zao hazifanhyi kazi ama kwa kuwa ni mbovu au kukosekana kwa nia ya kweli kufanikisha sera hizo kutoka kwa wanasiasa na viongozi wake.

  Bubu Ataka Kusema,

  Mafisadi na Viongozi wamefanya makusudi bila woga Ufisadi wakijua wazi kuwa kama Taifa, wananchi hatutakuwa na uwezo wowote zaidi ya kupiga kelele. Watanzania tunasifika kwa Amani, Utulivu na Mshikamano. Mafisadi walijua wazi tutapiga kelele, tutanung'unika na kisha wataendelea kupeta.

  Mafisadi na viongozi hawaogopi kuanikwa hadharani, ndio maana Lowassa na Chenge walipokelewa kama Wafalme, na bado wanataka kurudi kwenye madaraka, kwa kuwa wanatufanya sisi wajinga na wapumbavu.

  Kauli ya Vijisenti ilikuwa si dhihaka tuu, bali kutudharua na kutuambia kuwa hatuna manufaa kwao ila kura zetu. Mali asili na Hazina ya taifa ni yao na si yetu, zetu ni kura kuwapa wao kula huku sisi tukikomaa katika Umasikini na Unyonge!
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Aug 31, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka,

  ..umenifanya nifikiri zaidi na zaidi. pamoja na hayo sina jibu/jawabu kamili.

  ..tunaweza tusiwaelewe wananchi wa Monduli, lakini Lowassa amepeleka maendeleo[shule,maji,majosho,...] huko kupita Wabunge wengi tu Bunge la Jamhuri.

  ..sasa tutawaelimisha vipi wananchi wa Monduli kwamba Lowassa hafai katika uongozi kutokana na kuhusika kwake na Richmond na kashfa nyingine nyingi tu?

  ..halafu uzingatie kwamba CCM haitakuja iboronge kama walivyofanya ZANU na Mugabe. they will always keep the peace, na wataleta maendeleo kiduchu, but just enough kupata kura za wananchi.

  ..kazi yetu sisi wanaharakati ni kuwashawishi wasiridhike na maendeleo kiduchu, yanayoletwa kwa mwendo wa konokono na CCM.

  ..labda tuige ile injili ya Obama kule south chicago ya "America as it is vs America as it should be." sasa hapo kwenye America weka Tanzania.

  NB:

  ..najua sijakupa jawabu lolote lile, lakini that is just some thought process.
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Serpent General,

  Hakuna jibu ambalo wewe au mimi tunaweza kulitoa zaidi ya kufikiri kwa makini ni nini cha kufanya.

  Miezi kadhaa iliyopita na hata katika Waraka wa Mchungaji, niliuliza je Mtanzania anatafsiri gani ya maendeleo na anataka maendeleo ya namna gani?

  Kwa mfano wako wa Lowassa, ni rahisi sana kwa sisi ambao tumepata upeo mkubwa wa Maendeleo ya kweli kwa kutembea duniani, kuendelea kupata kigugumizi kushindwa kuwaelewa Watanzania walioridhika na maendeleo kiduchu.

  Je hayo maendeleo kiduchu yameshibana na utamaduni wa kutegemea misaada?

  Kwa mfano wa Lowassa, je maendeleo aliyoleta Monduli ni ya kufanya jamii ijitegemee na kujitoseleza na kuweza kuuza bidhaa na huduma kwa wengine au ni maendeleo ya kukidhi kinachohitajika dakika hii na si kesjho

  Je alileta maendeleo kwa kutoa msukumo wa kuongeza uzalishaji mali au ameleta maendeleo ya picha ambayo yameamabatana na misaada mingi kiasi kuonekana kwa mba hali si mbaya ni ya kawaida kwa kuwa hakujaharibika kitu?

  Tujiulize, Lowassa akifutika kwenye mnyumbuliko, je Monduli wataendela na maendeleo tunayodhani wamefikia? je kama Lowassa au Sokoine, sawa na Msuya, Kawawa, Salim, Warioba na Malecela au viongozi wengine ambao wamewahi kuwa viongozi wa Serikali wasingekuwa katika nyadhifa na nafasi zao, ni maendeleo gani yangekuwapo?

  Tujiulize, ni maendeleo gani ambayo Monduli wanayo ambayo yanaweza kuwa yameleta mabadiliko ya kweli na hivyo kusema wameendelea na kujitegemea?

  Ni shule ngapi, hozpitali, vyuo, viwanda, na kwa kiwango au kiasi gani uchumi wa Monduli umekuwa na hata kufikia hatua ya kujitegemea bila kuitegemea Serikali?

  Tunarudi pale pale ni vipi tunatoa maana ya maendeleo, na mafanikio yake na vipimo vyake.

  Kuna upotofu uliojijenga Tanzania kuwa kwa kuwa tuna magari na magorofa Dar Es Salaam, basi tumeendelea. Sawa na kauli za kusema kuwa kuwa na ndege ya kisasa kwa Rais au ATCL ni maendeleo, lakini itabidi kujiuliza,ni maendeleo gani ikiwa Uwanja wa Ndege Dar hauna maji ya kutosha? Hata hapo Dar Es Salaam penyewe penye kusifika kuwa ndiyo shina la maendeleo, ni maendeleo gani ikiwa hakuna maji, uchafu umekithiri, uholela wa mipango mbinu na tofati ya umasikini na vijijini ni sawa?

  Sasa tukipima maendeleo na kuchunguza kauli za wanasiasa wetu, utagundua kuwa wao wameridhika kutupa maendeleo kiduchu na hivyo kutudumaza. Lakini wao wenyewe wanajiendeleza kwa ushindani wa hali ya juu na hata kuzidiwa na tamaa na kuwa wanyang'anyi.

  Njia pekee ya kumkomboa Mtanzania na Tanzania kurejea kwenye uimara ni kumpa Mtanzania uhuru wa fikra na kutambua kuwa anaweza kuwa na maendeleo bora kuliko aliyonayo.

  Tumuulize Mtanzania ni kwa nini aendelee kwenda kukata kuni porini ili kupika chakula, tumuulize kwa nini aendelee kutumia mafuta ya taa ambayo ni ghali kuangaza nyumba yake huku akipumua moshi mchafu wa mafuta ambao unahatarisha mapafu yake na maisha yake, tumuulize Mtanzania kwa nini atembee maili moja kwenda kuchota maji ndoo moja?

  Sasa kama utamwambia Mtanzania na kumuonyesha kuwa anaweza kuwa na nishati ya jua, kutumia kupikia na kuangaza nyumba yake na hata kusaidia mitambo ya kusukuma maji, na kuwa na muda wa ziada kuzalisha mali na kuishi kwa maendeleo kama kiongozi mwakilishi wake, kwa nini Mtanzania huyu asishawishike?

  Ukimwambia Mtanzania kuwa nishati ya umeme itokanayo na jua au upepo itamsaidia kuwa na hifadhi nzuri za chakula chake kwa majokofu au maghala ya umeme kwa nini asishawishike?

  Ukimpa mtoto wa Kitanzania aliyeko vijijini hata mijini shule yenye umeme na akaweza kuwa na maabara, kompyuta, redio na vitendea kazi vingine vya kumfanya awe mbunifu, yenye maji safi, kwa nini mtoto huyu asijijenge kwa kuwa na fikra endelevu na si tegemezi? kwa nini usimpe nafasi mtoto huyu kujiandaa kwa ukamilifu kuwa taifa la kesho kwa kumoa uhuru wa mawazo, fikra, kujitegemea na ubunifu na hivyo akajiondoa kutoka Umasikini na Ujinga ambao ameurithi kwa vizazi zaidi ya vitatu?

  Si kuwa Serikali na CCM hawana mipango ya kuondoa umasikini. Mipango ipo, ila hawana nia ya kufanya lile wanalopaswa kulifanya. Sababu za wao kupuuza kufanya wanalopaswa kufanya ili kuimarisha maendeleo ni woga wao wa kukosa watumwa na wafuasi wa kufuatilia kila wanaloambiwa kuwa hivi ndivyo ilivyo! CCM wanaendeleza alichofanya mkoloni kwa mwafrika, kumfanya awe mnyonge inferior na inferiority complex!

  Ndio maana vita vya ufisadi havitafanikiwa bila kubadili uongozi na serikali. Ndio maana maendeleo hayatafanikiwa.

  Kama vile mbinu za medani zilivyobadilishwa wakati wa kugombea Uhuru na kufikia Tanzania kupata Uhuru wake, ndivyo nasi tunavyopaswa kufanya ili tupate uhuru wa mawazo, fikra na kujitegemea ili kumshinda adui ujinga, maradhi na umasikini.

  Siku Mtanzania atakapoamka na kujua kuwa anauwezo zaidi ya ule anaoambiwa kuwa anao, siku hiyo itakuwa nisiku ya furaha na faraja!
   
 20. T

  Thomas David Member

  #20
  Aug 31, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  There is no such a thing called solution at this point......The solution was to adhere to the rule of law in which they took an oath to keep and protect it,.. but that is not the case now...

  They know what to do since then they assumed the highest office of the land!!We could have not trusted them if at all they knew nothing!! JK shy away from taking the difficult path,but wananchi,if they a keen enough will do it come 2010...Just keep hope alive!!
   
Loading...