Why UKAWA will loose the 2015 Election

Perhaps it's a typo in your title - I think you intended 'lose' instead if 'loose'. If so, please make a correction.

IT is a typing error: I have tried to correct it lakini sijafanikiwa bado:
 
eeet CCM wana 5million wanapermanet voters...? nani kasema?
 
Mnaweza Kumkejeli Jamaa mleta Mada but he has a point:
1.With Raila and Ruto together there was no way Uhuru angekuwa rais,kosa alilofanya Raila ni kuruhusu Ruto aondoke matokeo yake akaondoka na kura zake.
2.Back to TZ: ACT/Zitto inaweza isifikishe idadi ya kura ambazo mleta mada ameitaja lakini ina uwezo wa kupata kiwango ambacho kwa namna yeyote ile kitakuwa na Significant effect kwa Ukawa.
3.Mbowe and Chadema: Sidhani kama Mbowe ni Chadema na Chadema ni Mbowe but Ukweli ni kuwa its very hard to challenge Mbowe katika ile Position labda siku atakayoamua yeye kutoka: Since 2009 It has failed to sink into my mind kwa nini Zitto alipotaka kugombea Uenyekiti wazee wa chama wakaamua kuifinyanga Demokrasia(kumbuka the 'de' in Chadema stands for demokrasia) na kumnyamazisha Zitto chini kwa chini kuwa amuache Mbowe apite Bila kupingwa.Kimsingi lile ndio lilikuwa kosa la Chadema mengine yote ni Yatokanayo.Ilikuwa ni busara kwa wazee kumuacha Mbowe kumshinda Zitto katika sanduku la kura kuliko kilichofanyika.
 
Watu wengine wamezidi kutumika kwa kweli vichwa vyao kama tunguli tu hahaahhahaa ------
 

Kimsingi nakubaliana na wewe:
 
Tatizo tu ni kulinganisha Zitto na Rutto. Siasa za Kenya ni tofauti sana na za hapa kwetu. Kenya politics are driven heavily with tribal/ area and that is what Uhuru/Rutto collission banked on to win - nothing more. It is very different setting in our politics in Tanzania.
 

Hii imani haikuja kama bahati mbaya, bali ina mpaka viashiria vyake, kwa namna moja ccm na Zitto kwa upande mwingine wamekuwa wakiitumia hii kama kete yao dhidi ya cdm. Huo ndio ukweli na ushahidi upo. Hilo la Zitto kuwa na wafuasi ndani ya cdm silipingi lakini sio kwamba yeye ndio kawashikia akili kwamba eti akibadilika ni lazima na wao wamfuate, labda kama wanafaidika na Zitto binafsi. Kama wewe hapa ulipo ni mmoja wapo ya washabiki wake na hatuwezi kukuzuia kumfuata aendako kwani ni haki yako, ila ukumbuke hata huko cdm bado kuna viongozi wengi tu wamewavutia watu na watu wamewafuata na wataendelea kama ilivyo kwa wale watakaomfuata Zitto. Na hivyohivyo kwa vyama vingine. Kwa mfano leo ccm imepungukiwa sana na idadi ya wapiga kura nako huko Zitto alihama? Ama hayo maeneo wapinzani waliposhinda na kunyakua viti vilivyokuwa vikimilikiwa na ccm ni kwamba Zitto alikuwa amehama hiyo ccm. Suala la watu kuhama na kuingia halijalishi mtu mmoja kama wewe na wanaccm wengi wanavyolitumia kwa propaganda.
 

Hakuna Marefu yasiyo na ncha kitatoka tu madarakani
 
Mleta Mada natofautiana na kufanana na wewe hivi:
1.Sidhani kama ACT au Zitto kama ulivoamua kusema kwamba atashinda urais 2015,sijaona uhalisia hapa kwa sababu Zitto by any means hawezi kuwa amefikisha umri wa kugombania urais by October,Lakini pia kwa yeyote atakayegombea uchanga wa chama unahusika moja kwa moja kutokupata ushindi kwa ACT.Lakini Mtazamo wangu ni huu;
2.ACT inaweza kushinda uchaguzi 2020:
a)Kumbuka Chadema imepata Pigo kubwa sana kuondoka kwa Zitto(wapo watakaokataa lakini ni uhuru wao),hivyo Chadema kwa sasa inatumia mgongo wa UKAWA kuonekana kama bado iko strong as before.
b)Baada ya uchaguzi mkuu(ambao naipa CCM asilimia kubwa ya kushinda),hakutakuwa na kitu kinaitwa UKAWA nakuunga mkono kama ulivosema hata origination yake haikuwa kwa ajili ya uchaguzi bali katiba,kutokana na hilo Basi tutaruri kulekule kwenye vyama tofauti kama ilivyokuwa awali,thn hapo ndipo udhaifu wa Chadema utakapoanza kuonekana wazi(kumbuka Zitto alisema kuna wabunge Zaidi ya 10 kutoka Chadema watajiunga na ACT sidhani kama hakuna ukweli juu ya hili therefore Chadema itakuwa taaban na ACT itakuwa on the rise ukizingatia walivojipanga and without forgetting the 'Zitto factor'
3.Anayesema ACT bado sana sio mhalisia,kumbuka imewachukua Chadema only 5 years kutoka wabunge 4 hadi 46(sina uhakika sana na hiyo figure) so the same thing can happen to ACT.Kumbuka Tanzania kuna vyama vya siasa 22 lakini katika uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka huu overall results za NEC imeiweka ACT nafasi ya 5,hiyo ni kabla hata ya kuzinduliwa rasmi.
4.ACT inaonekana kuja kitofauti zaidi katika kutangaza sera zao na kuwafikia wananchi: Kumbuka tuko katika Internet and Social media awareness generation,Kwa haraka haraka tu toka uzinduzi wao nimegundua ACT wametambua umuhimu wa ICT and Social Media Platforms katika kujijenga.Kuna mchangiaji alisema "Kitaenda wapi chama cha Facebook hiki?",Hakika hajajua nguvu ya Facebook katika Prosperity sio tu ya Chama cha siasa lakini hata Kibiashara.Labda huenda anaitumia FB kwa ku-upload Photos only.Utafiti Rasmi ulionyesha kwamba kitu kimoja kilichochangia Barack Obama kushinda ni jinsi walivyojitangaza kupitia Social Media platforms Including Facebook na kuwafikia vijana wengi(Kumbuka Vijana wa sasa its all about Internet).
 

Kaka naomba nikuulize ,,Unaweza ukazitaja hizo region zako ambazo umesema Zitto campaigned heavily ,,,Swali la mwisho mkuu hivi kwanini sasa CCM walishinda uraisi kwenye jimbo lake ? ....Au hakufanya campaign nzito jimboni mwake ?

Kiukweli Zitto ni ushawishi lakini nadhani unapoanza kutoa hesabu zako kuonyesha ushawishi wake ,,ndipo unapoanza utata
 

Mkuu, sijatamka kokote kwamba ZZK atashinda uchaguzi 2015. I said, He will be the KingMaker, in other words atapiga uRuto.
 

Kawe,Ubungo,Iringa mjini,Rukwa na mengineyo
 

Hivi ni malengo ya ACT ni kupambana na CHADEMA tu badala ya chama tawala?am confused, how can we support a party that aims at fighting against other opposition parties?Convince me to support this party with this kind of their thinking!
 

Why should we believe on what you are telling us?
 
Am so astonished with what kind of a poor analysis this is..... It sounds crazy comparing Kenyan politics with our own...

I thank you for the courage of posting your thread. But for your information Zitto is totally nothing in our politics....
He is very much closer to his political death!! If you are his die-hard supporter you better look for a replacement...

Anyway you are free to exercise your legal rights to freedom of speech. But be as it may; only the clueless people out there will support your inferior theory!!
 
"Mkuu, sijatamka kokote kwamba ZZK atashinda uchaguzi 2015. I said, He will be the KingMaker, in other words atapiga uRuto. "

Nimekupata kaka But maelezo yangu yanabaki kama yalivyo
 
Huu ni -----

Siasa za Kenya ni za kikabila hivyo mtu anaondoka na kabila lake....

Tanzania hakuko hivyo

Lakini stori ya CDM na zito imeisha ...ni vyama tofauti now

Kama Lengo la hicho chama kama alivyosema supreme leader wake ni kuwa kama chadema basi ni very myopic kwa sababu chadema yenyewe haijafika inapotaka

Watanzania watatoa majibu.....Watu wanadhani siasa za Field hapa Tz NI Mchezo
 
"Hivi ni malengo ya ACT ni kupambana na CHADEMA tu badala ya chama tawala?am confused, how can we support a party that aims at fighting against other opposition parties?Convince me to support this party with this kind of their thinking!"


MKUU: Sio lengo la ACT kuwa mpinzani wa Chadema unakosea,ACT Mpinzani wake ni chama chochote kile,Ila kwa sasa huwezi ukaepuka atmosphere ya kuonekana Chadema na ACT ni vyama vinavyokinzana(Japo ukweli sio huu na itaisha tu hii hali),hii ni kutokana na Chadema-Zitto saga
"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…