Wote wanaomini mtazamo wako wanatoka ccm na kwao ni faraja bila uhalisia.
@.
Impossible to a new political part like ACT to get more than 1million votes, (poor estimates) since you have taken into consideration only one factor (new member ZZK).
Your estimates is not clear and valid enough to convice voters because it is not recent data (2010) perhaps u could use recent data as well as other recent research to make your argument strong, this could avoid biases, also there could be no room to question your objectivity also your competence.
You didn't provide your recommendations towards your opinions provided,
Kwanini kuna hii imani lakini? Kwamba kila anayekubaliana na zitto au kuwa mfuasi wa Zitto ni mtu wa Ccm?? Ccm hawahawa waliojeruhiwa na Zitto bungeni kwa miaka nenda rudi leo wawe na mahaba na Zitto??
Hamuamini kuwa wapo watu wanafikiri na kutenda tofauti na nyinyi??? Na bado hamuamini kuwa Chadema ilikuwa na wafuasi wengi nyuma ya mgongo wa Zitto?? Hamuamini ya kuwa kuna vijana wengi waliovutiwa na siasa kwa mgongo wa zitto na wengine leo hii ni wabunge na nafasi nyinginezo za kisiasa??? Hamuamini ya kuwa kwa kadri zitto anavyosurubiwa kwa kuitwa msaliti basi mashabiki na wafuasi wake wameamua kukaa kimya na mapenzi yao kifuani?? Mkiona kimya mwajua " mmemumaliza?"
Mjadala wa aina hii unasikitisha sana. Yaani tunaweka akili zetu kwenye mikakati ya ushindi kama vile ndio "mwisho wa yote" - an end in itself - badala kuwianisha na mustakabali mzima wa taifa. Sioni Kabisa umuhimu wa kufikiria ushindi wa chama chochote cha siasa kama hautaleta mabadiliko ya msingi kwa mwelekeo wa taifa hili. Kama UKAWA watamuhitaji Zitto ili almuradi washinde uchaguzi tu hata kama haendani na mtazamo wao (wa kuleta mageuzi) basi nao watakuwa janga jingine kulikumba taifa hili baada ya uozo wa CCM.
Kwanini kuna hii imani lakini? Kwamba kila anayekubaliana na zitto au kuwa mfuasi wa Zitto ni mtu wa Ccm?? Ccm hawahawa waliojeruhiwa na Zitto bungeni kwa miaka nenda rudi leo wawe na mahaba na Zitto??
Hamuamini kuwa wapo watu wanafikiri na kutenda tofauti na nyinyi??? ..."
Kwa jinsi ulivyomalizia uzi wako wewe mleta mada unaonekana kama unajishuku hivi. Hiyo mifano unayotolea kuhusu Kenya sidhani kama ungeitolea kwenye upande wa maendeleo.
Ni hivi hapa naona kama umekuja kuandaa watu kisaikolojia kwamba Ukawa watashindwa na unalazimisha sababu iwe ni Zitto.
Kama kweli unachokisema ni hicho mbona hao CHADEMA hawakushinda urais 2010 wakati Zitto akiwa bado cdm?
Umeweka na idadi kabisa ya wapiga kura kwa mujibu wa mtazamo wako, lakini ukiangalia ni kama vile mada yako inalazimisha kwamba bila Zitto basi Ukawa hawawezi kushinda urais!!
Hivi ni nani unaweza kumdaganya tena kwa hisia za kwamba bila Zitto CHADEMA hakuna. Wote wanaomini mtazamo wako wanatoka ccm na kwao ni faraja bila uhalisia.
Naomba nikupe mfano mrahisi wa karibuni, hivi majuzi kumefanyika uchaguzi wa serekali za mitaa, ukiachia mbali zoezi kuendeshwa kwa hila na mapungufu mengi, CHADEMA wamezoa viti vingi sana bila mchango wowote wa Zitto.
Sasa nashangaa unalazimisha data za mwaka 2010 unaacha za hivi karibuni kabisa na madhara yake kwa uchaguzi mkuu ujao.
Kama ni kweli usemacho nilitarajia uchaguzi huu uliopita miezi michache ndio ingekuwa sehemu ya wewe kujengea hoja na sio mwaka 2010 ambapo hata aina ya matokeo yalipatikana kwa vitisho na ugomvi mkubwa.
Kama unataka kumtetea Zitto wewe mtetee kwa njia nyingine na sio zaidi ya hapo.
Tanzania politics is based on what????
Where ZZK political forces came from???
Please explain more ndugu,,tunajifunza tu hapa
Ndio tatizo kubwa ya ndugu zangu wa Chadema, ukipingana nao kihoja au ukikubaliana na BAADHI ya hoja za ZZK wewe unakuwa ni adui wao na kibaraka wa CCM. Jambo ambalo si kweli,
Yapo mambo ya msingi ZZK amelifanyia taifa hili, kama alikosea kwenye chama chake na wakamuadhibu hiyo ni mambo yao ya chamani. Hata CCM wanagombana kila siku,,lakini sisi kama watanzania hayo si muhimu kwetu. Cha muhimu kipindi cha uongozi wake kasimamia madini na sheria zake; Uwajibikaji serikalini: Kachochea mwamko wa kisiasa kwa vijana wengi na mengineyo ambayo sote tumeyaona kama watanzania.