Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?



Ndigu zetu, hivi kumbe habari zote zinafahamika na sie tumekaa kimya tuu.

it's good kwamba zinaanza kujulikana..... Tunaomba akina Said Kubenea na waandishi wengine wenye uzalendo wazifanyie kazi zianze kuunguruma.
 
The TTCL story doesn’t end here,it still continues. From reliable sources it is said that the same CELTEL/ZAIN owners in collaboration with Government officials they put a condition that TTCL NOT BE ALLOWED GO MOBILE as they,TTCL shall paralyze other MOBILE OPERATORS in Tanzania especially ZAIN. You may notice that in ZAIN the following big heads have a good number of shares: SALIM AHMED SALIM, ROSTAM AZIZI, JOSEPH SINDE WARIOBA,MO IBRAHIM,EDWARD LOWASSA and JK !
As that is not enough, The Tanzania government owes TTCL about 7 billion Tshs. BUT the Government is reluctant to settle the debt!!Reasons??The government coffers have no monie!!???But they are ready to pay the Ghost RICHMONDULI alias DOWANS Company a total of 94/= billion Tshs.

Sheeewww!!
Kumbe sie wajinga ndio tuliwao!! Wakati wakubwa wanakula nchi .. sisi makelele tu.
Haya mambo sasa yako wazi ... ina maana hawa akina JK hawaoni hata aibu wajiuzulu? wanasubiri nini?
 
Wanandugu,

Nashukuru kwa mkubwa hapo juu kwa kutoa ufafanuzi wa undani, mimi nilibahatika kufanya kazi pale kwa muda mfupi,na sasa nipo kwenye upande mwingine wa dunia, niligundua mambo mengi sana.

Kwanza tuwe wakweli, suala la utaalamu upo wa kutosha, na kuna watu wana vichwa vikali huwezi kuamini, na ukitaka kuamini hilo, strategies nyingi zinabuniwa pale, lakini kutokana na uchelewesho wa utekelezaji na ule mwimbo wa ukosefu wa fedha, utashangaa zimeibuka kwa makampuni mengine binafsi (si ajabu kwa sababu kwenye bodi yao Zain wapo ndani).

Kuna miradi ambayo najua ilipangwa pale, kwa ajili ya masuala ya kitaifa, nimeshangaa plan zile zile wamepewa makampuni binafsi (na wanazitekeleza), utajiuliza zimetoka wapi?. sasa hawa tutawaita ma ' Idiot' kweli?. Idiot ataigwa mikakati na ufundi wake?.Sishangai sana kwa sababu ya mchanganyiko wa bodi na utaratibu wa kupeleka 'strategies' wizarani kwa approval...., hapo sasa!.

Hivi hamjiulizi kuwa hao tunaodhani wanaakili (WAZUNGU) waliishapewa TTCL kuiongoza, wakaamua kuingia mitini, wakijua kuwa itakuja kuwafia mbeleni baada ya kukosa ushirikiano toka serikalini?

Suala kubwa kwa TTCL ni uwezeshwaji, haya makampuni tunayoyasifia, jiulize yamepata mikopo mara ngapi toka yameingia kwa ajili ya new investments (mengine yalikuwa yanakufa kabisa, mikopo ikayasaidia) na shughuli za kimasoko. Lakini nilishangaa kuwa TTCL haipewa nafasi hata mara moja ya kupata mkopo, tena hawataki 'fadhira' za bure, ni mkopo lakini tumejiuliza kwanini hawapewi?. kwa kipindi chote hicho wamekuwa wakijiendesha kwa pesa zao wenyewe, bila msaada.

Leo hata ukiwambia TTCL wajitangaze, hawana uwezo wa kutosha kumudu soko bila kuwekeza kuongeza mtandao, kwa kudunduliza billi za kila mwezi hawawezi kwenda popote, na hata ukimpeleka MALAIKA aongoze hapo, bila uwezeshwaji atakimbia tu, kila kitu atakiona cha moto.Kuna fikra potofu kuwa TTCL ipo kila sehemu, si kweli, haijafika sehemu nyingi, na hata kule walipo utakuwa ina uwezo wa kutoa huduma kwa wateja wachache tu. Pia dhana ya kuchanganya kuwa sehemu yeyete waliopo mobile itafanya kazi si kweli, inahitaji uwekezaji mpya kabisa kwani ni technologia ambazo haziingiliani na fixed lines.

Wakati umefika watanzania kuamka na kuacha uvivu wa kufikiri, tujaribu kuyachunguza mambo kwa undani. Makampuni ya umma yenye roho ngumu kama TTCL pengine yanatakiwa YAFE, ndiyo maana hayana support, pengine kama alivyosema mchangiaji hapo juu kuwa "hata kile kidogo walichonacho kinamendewa"


Uzalendo Kwanza,
 
Please kama inawezekana tupate scanned copy ya hiyo barua!
Anyway CCM must go!
 
CCM must go and the whole top TTCL leadership must follow!
 


GIS,

Kwanza nikupongeze kwa mchango wako mzuri kuhusu TTCL.
Ulichosema mkuu ni a 100% correct. Napenda tu nizungumzie hii sehemu niliyo-bold kwa rangi 'damu ya mzee'.

Kwamba maeneo yote ambako Mtanzania yoyote anayetumia simu za Zain/Airtel AJUE KUWA ILE MINARA ILIFANYIWA KAZI YA UPEMBUZI YAKINIFU na ENGINEERS WA TTCL. Upembuzi yakinifu ninaozungumzia ni DETAIL SURVEYS kwa ajili ya kuweka hiyo minara(i.e Towers+Power supply+BTS).

Kazi hiyo ilifanyika wakti Zain wakijiita Celtel Tanzania as a SISTER COMPANY or subsidiary company to TTCL. Kwa hiyo ma-engineers wa TTCL walishirikishwa kama vile WANAFANYA KAZI YA TTCL. Baada tu ya survey ile PESA YA TTCL NDIYO ILIYOTUMIKA KUAGIZA/KUNUNULIA MITAMBO HIYO GSM NA ILIKUWA IKIINGIZWA NCHINI KWA JINA LA TTCL NA SI CELTEL TANZANIA!

Ni baada tu ya hawa Celtel kumwaga BTS zao kwa mgongo wa TTCL na kuanza kutengeneza FAIDA KUBWA, ndipo wakatangaza NDOA YA CELTEL na TTCL kuvunjika. Hakuna kigogo yoyote aliyehoji uhalali wa Celtel kufanya vile. Ukiuliza ni kwanini jibu liko wazi: Vigogo walipanga iwe hivo.

Nakumbuka wakti uke Mwandosya akiwa Waziri wa Mawasiliano alikwenda kuzindua kituo cha Celtel/Zain huko mikoani na BILA AIBU AKAWAAMBIA WANANCHI KUWA WATU WAACHANE NA SIMU ZA TTCL ZA MEZANI MAANA ZIMEPITWA NA WAKTI!!!Think about that statement, a government Minister anaiponda Kampuni ya Serikali tena iliyokuwa inaibeba hiyo Celtel aliyokuwa akiipigia debe. Shame!!!

Mr. Mwandosya wakti huo akiwa Waziri wa Mawasilianao alichangia kwa sehemu kubwa sana kuimaliza TTCL! Nitaeleza baadaye ni vipi Mwandosya alichangia KUIANGAMIZA TTCL. Kwa sasa naishia hapa.
 

Daah, hii inauma sana. Imenitoa chozi!!!
 
Nope! Wamekwisha!....just wait n see. God have not forsaken us yet!

Nashukuru kuwa una matumanini kwenye mazingira ya kukata tamaa kabisa. Tumaini lako lienee kwa kila mtu anayesoma ili tuchukue hatua zinazostahili. It is just pathetic. Uozo wa nchi hii umekithiri mno hata hatujui tutajinasuaje. We need a miracle.
 
Ukisoma habari za Shingo na Gis.., kwakweli machozi yanakulengalenga unless wewe una-matatizo ya Uzalendo..., wapi waandishi wetu wa habari.., haya mambo si ya kufichaficha, Ugonjwa haufichwi bali huwekwa wazi ili tuutafutie dawa am sure wazalendo wangejua haya huenda wateja wa hizi network za kifisadi zingekosa wateja
 

Ni kweli. Hizi habari zilitoka pia kwenye former forum i.e BCS. Hata jina la binti huyo liliwekwa kwenye mtandao.
 
So what should we do ili tuiokoe kampuni yetu?

Hapa ni kujiuliza, kati ya watu unawaowafahamu ukiwamo wewe mwenyewe, ni wangapi wanatumia ttcl mobile? Wengi wetu tumedandia mitandao ya mafisadi na kuwaneemesha hao mafisadi, huku shirika letu lenyewe likifa. Tubadilike tutumie ttcl
 
Hapa ni kujiuliza, kati ya watu unawaowafahamu ukiwamo wewe mwenyewe, ni wangapi wanatumia ttcl mobile? Wengi wetu tumedandia mitandao ya mafisadi na kuwaneemesha hao mafisadi, huku shirika letu lenyewe likifa. Tubadilike tutumie ttcl
Tatizo hata tukitumia TTCL hawa jamaa bado wataziibe huko huko dawa na kuwaondoa hao wezi
 
Huyo kwenye rangi nyekundu ndiye aliyeua TTCL kwa ushirikiano na makaburu weupe na weusi(akina Nigel na Makenzie)
 

Ukimsoma Kishongo na Gis hapo kwenye post za juu, am sure utabadilisha kauli...,
 
Hii issue inafanana sana na ile ya TANESCO. Wengi wamekuja hapa na majibu kama yale ya Ngeleja juu ya TANESCO na DOWANS. Tusiubebeshe mzigo uongozi wa TTCL, tuangalie mazingira wanayofanyia kazi. Ni wangapi, kwa mfano, wanajua TTCL wanalipa kodi kiasi gani, na haya makampuni mengine yanalipa kiasi gani? Tatizo ni waroho wachache tulionao, na hii ya TTCL, sawa na ile ya TANESCO, ni vema yakapelekwa bungeni ili tuone kama kuna njia ya kufanya ili yamnufaishe mwananchi kwa kuwa ni mashirika ya umma.
 
Nasikia Ephraim Mafuru aliyekuwa Vodacom amehamia TTCL kama Mkurugenzi Mkuu,
Je ni kweli na anaweza kuleta mabadiliko chanya na kuifufua TTCL?
 

Rostam Aziz na Lowasa siyo shareholders wa Airtel ( Celtel, Zain) ila wako VODACOM na Rostam Aziz alikuwa major shareholder ila sasa nasikia kapunguza share kwa kuwauzia Vodafone
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…