WHY JK must now crack the whip to protect himself.....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Nothing questioned JK's political leadership skills than Edward Lowassa's emphatic oral defence at CCM NEC in the just concluded adhoc gathering.......................

Lowassa's emotional outburst; though often inadvertently self-incriminating, lacking legal considerations......................has placed JK at the epicenter of official graft now threatening to splinter ccm into scattered shards................................

What did Lowassa achieve from that?

a) Though bemoaning presidential succession politics as behind his current political woes, lowassa regimented himself behind the real face of official graft well encompassed by Mkapa and Sumaye..........................in leveling accusation against the face of newblood in ccm well encapsulated by Nape Nnauye and Chiligati

Albeit Mkapa did not utter a word but reading from his facial gesticulations and remonstrations demonstrated beyond doubt that in many ways he was empathizing with lowassa's narratives!

Sumaye's verbiage clearly confirmed that the old guard was not going to yield power to the new blood without a concerted fight for survival.....................

b) lowassa in many ways is a double-speaker..........while at Bunge House when confronted with Mwakyembe report that had placed him at the heart of Richmond/Dowans maelstrom,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,what Lowassa did was to self-incriminate himself, at the gist of his vehement defence was his admission that indeed he was the one who had formed an illegal entity that he christened Government Negotiating Team.........also abridged as GNT..................contrary to the procurement act!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Lowassa though a Premier at the time had no legal authority to temper or even meddle with the procurement act. Paradoxically, it is this legal alien in "GNT" that provided arbitrators with a leeway to award DOWANS with billions of shillings based on a flimsy ground that that act was not binding since even the government had violated it!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

c) Almost risible is the feeble attempt by Lowassa to mud-sling the incumbent president in JK over the most heinous graft allegations this nation has so far, endured....................

Lowassa alleges that he was the one who phoned Jk advising him to end the Richmon contract ........lowassa can hardly substantiate this surmise let alone his decision of staying in office after JK had reneged and had pussyfooted to heed Lowassa's call for prompt action...the problem for Lowassa such a surmise at this wee hour only raises more questions than do provide for the Damascus light.............................


i) For start, when it comes to momentous government decisions, is this a case of a phone call to an erstwhile buddy or a call for cabinet meeting to thresh-out the conundrums then besieging the government?

Lowassa can hardly substantiate this surmise let alone exculpate himself for bypassing the ministerial cabinet.............this was a case of abuse of public office nothing more and nothing less.............

ii) During the Mwakyembe report on Richmond/Dowans scams, Lowassa did not accuse JK of procrastinations rendering his brickbrat against JK now looking misplaced or an afterthought...........at best.......

iii) Perhaps more alarming is when Lowassa reminded JK of Hassan Mwakawago dossier that had implicated JK in mega scandals in 1995 ccm presidential nominations process..............................The snag for Lowassa has always been that he was economical with the truth because lowassa had even worse "dossier" that was prepared beforehand by TISS that was too incriminating against him even to attract the dire interest of nyerere...................we all know that cc ccm went on to clear Jk but Lowassa was not, and this explained why Jk went on to face Mkapa in the final ccm presidential nominations' jigsaw and lowassa was dumped in the preliminaries......................................

iv) In all this Lowassa's cold calculating mind misleads him to believe that the easiest way to extricate himself from this political muzzle is to implicate Jk hoping to subdue JK's political zeal of dealing a lasting blow to the face of official graft inside ccm and help his party standing a better chance of recapturing power; at least in the public opinion flora, in 2015 without the need to seek both NEC and TISS invidious intervention..............................

If JK succumbs to Lowassa's bag of trickery then ccm will be tamed into the former's cloak of protecting the architects of official grand graft. This will be a recipe of ccm losing bigtime 2015 presidential and parliamentary elections to chadema.................hands down.....really.......

What are JK political options?


a) Reaffirming his wavering support to the new blood now firmly captured by Nape nnauye...........Jk ought to publicly reiterate that nape and Chiligati have the full support of CCM CC..............................................Actually not mincing words, it is important that I point out that Jk was wrong to allude both nape and Chiligati may be under investigations to whether they had abided to party policy when going after the jugular of the lynchpin of official graft in ccm.,.

b) He needs to immediately reconvene the cc as a matter of urgency in order to relinquish Lowassa, chenge among others of ccm parliamentary seats................and suspend their membership pending further procedures...just to remind their supporters ccm is serious on slaying the graft dragons now conspiring to take power by sheer force of dirty cash and negative propaganda..................

c) If JK feels he is unwilling or incapable of dealing perpendicular with Lowassa's intransigence...........then he is the one who has to be shown the door for gross incompetence.............

d) last but not least I am still mesmerized by Dr. msabaha's valediction following the Mwakayembe report on the ministry he was once in-charge........While still clutching a " I am Mr. Clean" image............for obvious reasons...........Dr. Msabaha saw the Damascus light when he conceded that politics was a game of perceptions........................and the truth really has no part in it.....................and public opinion ought to be treated like.............."Ceaser's wife being above reproach"..........................the guy left the political scene with his head held high............................I keep wondering when Jk and Lowassa in particular will read and re-read................. Dr. msabaha's Hansards for not only guidance but also for using that wisdom as an example to emulate.............................
 
lowassa is playing a dirty game that can be summarized as "scratch my back and I will scratch yours too...."
 
Pambaf zako, unatuletea ulongo hapa, Lowasa alikalia kiti cha u-PM wakati mradi unaendelea, alipendekeza mkataba uvunjwe-JK akakataa, sasa mbona wadanganya ati alipindisha procurement ACt. Usijidanganye, mwisho wa J K ni mwaka huu.
 
Pambaf zako, unatuletea ulongo hapa, Lowasa alikalia kiti cha u-PM wakati mradi unaendelea, alipendekeza mkataba uvunjwe-JK akakataa, sasa mbona wadanganya ati alipindisha procurement ACt. Usijidanganye, mwisho wa J K ni mwaka huu.

lowassa alipoona jk kakataa alichukua hatua gani za kujitoa kwenye nafasi ya u-pm na kujiuzulu kama asemayo haya ni kweli? halafu mbona kwenye hansard hakuna mahali ambapo Lowassa kamtuhumu Jk kuwa alikataa ushauri wake?
 
Sabodo amchambua Kikwete

• Asema ni kiongozi anayecheka na rushwa

na Waandishi wetu

MFANYABIASHA maarufu na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mustafa Sabodo, amesema tatizo la rushwa limezidi kushamiri nchini katika zama hizi kutokana na upole wa Rais Jakaya Kikwete.

Sabodo ambaye amejipambanua kama mdau mkubwa wa harakati za kimaendeleo, alisema kwa hilo, ni rahisi kumlaumu Rais Jakaya Kikwete kwani wanaomponza ni watendaji wake.

Aliyasema hayo jana nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuzawadiwa na wanafunzi wa Shule ya Michezo ya Tanzania Sports Catalyst TASCA) iliyopo Kigamboni, kutokana na mchango wake kwa shule hiyo.

Alisema watendaji wa Kikwete hawaonyeshi dhamira ya dhati kuichukia rushwa kama ilivyo kwa Rais huyo.

Sabodo ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alikipa Chama cha Demokrasi na Maendeleo jumla ya sh mil. 200, alisema ingawa rushwa ilikuwepo hata katika Awamu ya Kwanza ya Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere, lakini si kama ilivyo hivi sasa.

Alisema, hali hiyo ilitokana na ukali wa mwasisi huyo wa Taifa la Tanzania ambaye katika utawala wake, alipigania haki, usawa na utu.

"Kwa sasa hali imekuwa mbaya sana, yote hii inachangiwa na upole alionao Kikwete, hivyo hata watendaji wa juu sio wakali na hawapo tayari kuichukia rushwa na kuepukana nayo," alisema.

Akisisitiza kile anachokiamini, Sabodo ameonyesha kusikitishwa na adhabu ya faini ya sh 700,000 kwa aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Andrew Chenge, iliyotokana na kesi ya tuhuma za mauaji ya watu watu wawili.

Sabodo alikwenda mbali zaidi na kusema upole wa JK pia umekuwa ukilalamikiwa na wananchi ambao wamekuwa wakimwona kama anawalea mafisadi.

"Kuna kipindi nilikwenda Rombo, kukabidhi moja ya shule nilizojenga, lakini nilishangazwa na Rais Kikwete kumnadi hadharani Basil Mramba anayekabiliwa na kesi ya ufisadi.

"Watu wamekuwa wakimlalamikia JK kuwa anawakumbatia mafisadi na hata Mramba pia, lakini yeye alimnadi hadharani huku akijua bado ana kesi inayomkabili!" alisema.

Kwa upande mwingine, Sabodo aliunga mkono pendekezo la Katiba mpya na kupendekeza ziwe tatu; yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania.

Katika hatua nyingine, Sabodo aliwasisitiza wanafunzi hao kuzingatia elimu kwani maendeleo ya nchi yanawategemea wao, kinyume na hapo watashindwa kutimiza ndoto zao.

Naye Mhadhiri Mwandamizi Profesa Mwesiga Baregu amesema Rais Jakaya Kikwete anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na viongozi wa serikali yake kutoa kauli za kuwachanganya Watanzania kuhusiana na suala la Dowans.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu, alisema kuwa matamko mbalimbali juu ya suala hilo yaliyokuwa yakitolewa na serikali yameonyesha ni kwa kiasi gani viongozi hao wamekosa nidhamu kwa umma.

Alisema kauli hizo zimewagonganisha Watanzania, hivyo ni wakati muafaka kwa Rais Kikwete kusimama na kuomba radhi kwa umma juu ya suala hilo.

Alisema haoni umuhimu wa suala hilo kwenda kujadiliwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa linaihusu nchi nzima na si chama hicho pekee.

"Inawezekana Rais Kikwete anataka kuueleza umma kuwa suala hilo alinamhusu yeye au ni mzigo wa chama chake ndiyo maana akalipeleka huko; au anafikiria bado yuko kwenye uchaguzi akiamini ni jambo la utekelezaji wa ilani ya CCM," alieleza Profesa Baregu.

Alisema hata hivyo tamko hilo halijajitosheleza hivyo ni muhimu akalifafanua kwa uwazi kuliko kutumia maneno yanayohitaji ufafanuzi mpana.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), Abdallaha Kibunda, alipongeza hatua ya Kikwete kutegua kitendawili kuhusu suala la kampuni ya Dowans ingawa amechelewa.

Alisema kimya chake cha muda mrefu kuhusu sakata hilo ndicho kilichowafanya watu wengi kuzungumza mambo mengi juu yake na Dowans.

"Maelezo aliyoyatoa Kikwete yalikuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu na alitakiwa kuyatoa kabla watu hawajamchafua kwa suala hilo na hiyo ingesaidia kushusha imani ya watu kwake lakini badala yake alikaa kimya kwa muda mrefu," alisema Kibunda.

Alimshauri kutoyachelewesha mambo yanayoshusha hadhi yake kwani kufanya hivyo kunajenga dhana mbaya.

"Anapokaa muda mrefu bila kushughulikia tatizo mwisho wake huwa mbaya kwani hata utakapokuja kutatua tatizo hilo baadaye unakuwa umejenga maswali mengi," alisema Kibunda.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Masuala ya Haki za Binadamu na (Aford), Julius Miselya, alisema kauli ya Kikwete si ya ukweli kutokana na kuwepo kwa mitazamo tofauti ndani ya serikali yake.

Alisema kuwa kauli tata zilizotolewa na viongozi hao ni za kutaka kuwachanganya Watanzania hivyo hakuna ukweli unaoweza kuonekana juu ya kutaka kulipwa au kutolipwa kwa kampuni hiyo.

Alisema kutokana na kushindwa kuwa wazi juu ya kampuni hiyo ni wakati muafaka kwake kujiuzulu nafasi hiyo ili kuepuka kuendelea kuudanganya umma.

"Kumekuwa na kauli za kutofautiana hata katika hiyo Kamati Kuu; hakika kama ililijadili lile alilolisema Rais Kikwete maana haiwezekani Waziri wa Nishati na Madini asimamie kulipwa halafu wadai katika kikao hicho walipinga malipo hayo," alisema.
 
DOWUTA yataka mafisadi CCM kung'olewa bila ubaguzi


na Mwandishi wetu


amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), Abdallah Kibunda, amemshauri Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza haraka uamuzi wake wa kuwang'oa chamani wote wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi bila kujali nyadhifa zao.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Tanzania Daima kuhusu hatua ya Mwenyekiti wa CCM kueleza dhamira yake ya kukifumua chama hicho kama mkakati wa kukijengea uimara mbele ya safari.
"Nampongeza Kikwete kwa hatua yake ya kutaka kukisafisha chama, kama anataka kukiimarisha chama hicho namshauri achukue haraka hatua hizo madhubuti kukinusuru kwani kimekuwa kikinyooshewa kidole kwa muda mrefu sasa," alisema Kibunda.
Kwa mujibu wa Kibunda inashangaza kuona kiongozi fisadi akiteuliwa kuingia katika chombo cha maamuzi ya juu kama vile Kamati Kuu ya CCM na kusema kwamba watu hao hawafai hata kidogo kushirikishwa katika maamuzi.
Alishauri chama hicho kuwa na mchanganyiko maalumu wa kuwa na wanachama vijana wa jinsia zote pamoja na wazee wenye hekima.
Pia alishauri chama kurejesha taratibu zake za miaka ya nyuma kuwa na chuo cha kufundishia makada wa chama kwa kuwa wengi waliopo wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi.
Wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya CCM yaliyofanyika Dodoma, Kikwete ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema chama hicho kitafanya mabadiliko makubwa ikiwemo kuwaengua watendaji mzigo na wanaopakana matope.
 
• Aonya hatari ya matabaka, ahamasisha vijana nchini kupambana

na Mariana Mathias

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Fredrick Sumaye, amewataka vijana kuwa na uzalendo wenye faida kwa kuhakikisha wanapiga vita rushwa na ufisadi ulio katika jamii kwa kile alichokieleza kuwa "ndio janga kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya taifa".

Sumaye alitoa hamasa hiyo katika mahafali ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari Pugu jijini Dar es Salaam akisisitiza kwamba rushwa na ufisadi vilivyotamalaki katika jamii ni matunda ya ubinafsi wa watu wanaopenda kujilimbikizia mali kwa manufaa yao.

Kwa hiyo, aliwataka vijana kutokuwa wabinafsi na badala yake wajenge maadili mema ili kuwa na taifa la kizalendo ambalo wananchi wake hawapendi rushwa na ufisadi.


Akionekana kuzungumza kwa tahadhari kubwa Sumaye alionya kuwa ufisadi na rushwa katika nchi hujenga matabaka mawili: moja ni la wananchi wengi wasionacho na tabaka la pili ni la wachache walionacho ambalo limekuwa likiwanyima haki na fursa walio wengi katika kupata huduma za jamii.


Alisema utajiri wa nchi ukijikusanya kwa wachache ni hatari kwa taifa kwani kundi hilo kubwa la wanyonge linaweza kuingia katika mgogoro mkubwa wa kudai haki yake.


"Ufisadi na rushwa ni janga katika nchi zinazoendelea ndio maana haziwezi kuondokana na umaskini kwa sababu ndani yake kuna tabaka la wachache linalonyonya nguvu ya wenzao walio wengi," alisema.


Alisisitiza ni lazima ukuaji wa uchumi uonekane katika mabadiliko chanya kitaifa kwa kuwa na vijana wazalendo wanaojali maslahi ya nchi yao.


Aliendelea kusema vijana wanatakiwa kujitoa kwa jamii katika kufanya kazi kwa ajili ya kusaidia wanyonge katika kupata huduma mbalimbali za kijamii.


Alisema umaskini, ufisadi, magonjwa kama ukimwi na rushwa ni matatizo yanayowakumba vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa katika uzalishaji.


"Naamini kuwa elimu ni karakana ya maisha kwa kujipanga katika maisha ya baadaye hivyo kupanga kufanya ufisadi na rushwa si matarajio ya shule. Elimu yenu mliyoipata muitumie katika ujenzi wa taifa….msipofanya hivyo mtakuwa wasaliti," alisema.


Nchi zenye maendeleo ziliweka misingi bora katika masomo ya sayansi hivyo ni vyema vijana kuongeza juhudi katika masomo hayo.


"Naamini kuwa ni vizuri kuwa na umuhimu lakini ni muhimu zaidi kuwa vizuri," alimalizia Sumaye.
 
Msuya: Kuna uwezekano CCM kung'olewa


Na Tumaini Makene

WAZIRI Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Bw. Cleopa Msuya amesema kwa jinsi vuguvugu la kisiasa lilivyo kwa sasa nchini, si ajabu chama kingine
tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua hatamu za kuongoza serikali.

Mbali na hilo, Bw. Msuya (80) amesema ni wazi kama hatua za dhati hazitachukuliwa kuweka mfumo mzuri wa kutatua matatizo ya wananchi, hususan vijana, hali kama iliyotokea nchini Tunisia na katika nchi nyingine za Misri, Algeria na Ivory Coast, inaweza kutokea Tanzania.

Lakini ameonesha matumaini kuwa mjadala wa katiba mpya ambao Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeuridhia, utasaidia hali kama hiyo isitokee kwani baadhi ya mifumo inayoweza kuepusha itajadiliwa kwa kina na hata kuwekwa katika katiba, kwa manufaa ya Watanzania.

Kwa mujibu wa Bw. Msuya, katika mjadala unaonedelea nchini juu ya katiba mpya, ni vyema ikafikiriwa kama kuna haja ya kuendelea kuwa na bunge moja, huku yeye akipendekeza kuwapo wa mabunge mawili, kama ilivyo nchini Uingereza.

Mzee Msuya aliyasema hayo juzi, alipofanya mahojiano maalum na magazeti ya Kampuni ya Business Times Ltd, inayochapisha Majira, Business Times, Dar Leo na Spoti Starehe, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Akionekana kufurahishwa na namna Watanzania wengi wanavyoonesha utayari wa kutafuta maisha, alisema hiyo ni changamoto kwa serikali kwani inao wajibu wa kuonesha njia sahihi na kuweka mazingira bora ya wananchi wake kutumia fursa nyingi zilizopo.

Pamoja na kuisifia serikali katika baadhi ya maeneo, huku akionesha imani kuwa inaweza kurekebisha ili kulikwamua taifa hasa kwa kutumia fursa anuai ambazo Tanzania imebarikiwa kuwa nazo, Bw. Msuya alionekana kushangazwa na kusuasua kwa ushughulikiaji wa mambo muhimu kiasi cha kuzua minong'ono kwamba 'kuna mkono wa mtu hapo.'

Maendeleo yatokane na vipaumbele

Mzee Msuya alisema kuwa Tanzania ina kila kitu kinachoweza kuifanya nchi yoyote kuendelea kiuchumi, akisema "kwa mfano kwa nini tusiwe Qatar ya Afika Mashariki kwa kuzalisha gesi na kuweza kuuza gesi yetu ya asili kwa majirani. Mwalimu alisema kupanga ni kuchagua."

Akifafanua suala la umuhimu wa vipaumbele katika kuiwezesha nchi kuendelea, Bw. Msuya alisema kuwa haiwezekani maendeleo kupatikana kwa kufanya kila kitu kwa wakati mmoja.

"Unajua masuala ya maendeleo you need (unahitaji) kupanga, Mwalimu (Nyerere) alikuwa akisema kupanga ni kuchagua...ukijaribu kufanya kila kitu kwa wakati mmoja huwezi, lazima uwe na specific (malengo) target on some issues. Nitawapatia mfano...

"Kuna wakati baada ya uhuru serikali iliamua kutumia fursa za kiuchumi kwa majirani zetu, ndani ya muda fulani tukaamua kujenga reli ya TAZARA kwenda Zambia kwa msaada wa Wachina, tukajenga barabara ya lami kwenda huko mikoa ya kusini na tukajenga bomba la mafuta, TAZAMA, ilikuwa ni mipango ndani ya muda fulani, mnaacha mengine mna-concetrate.

"You have to select priorities (lazima uwe na vipaumbele). Imekuwa ikiniuma sana mimi, lakini ni changamoto, maana sasa tunazo raslimali zaidi kuliko tulivyokuwa wakati ule, tunao watu, lakini results (matunda) hayaonekani, sisi sio landrocked kama walivyo baadhi ya majirani zetu, sisi si nusu jangwa kama kama Kenya kwa mfano.

Huku akinukuu maneno ya Balozi wa Ujerumani, Bw. Guido Hertz, ambaye aliwahi kuhojiwa na gazeti moja nchini na kuonesha mshangao juu ya umaskini uliokithiri wa Watanzania pamoja na utajiri wa raslimali zilizopo, akisema "ni vigumu kuelewa wala kuielezea hali hii," Mzee Msuya aliongeza;

"Tuna kila kitu kinachohitajika...kuna haja ya kujitazama upya, tuna raslimali za kila aina zikiwemo za asili, are we putting them on the best use (tunazitumia inavyostahili ?)...tuna gesi ya asili, tuna akiba ya kutosha ya dhahabu, utalii pia...kuna hili ka kilimo kwanza, serikali imeshatamka ingawa kwa kuchelewa kidogo.

"Lakini nalo hatujalianza vizuri (la kilimo kwanza) kwa sababu hiyo hiyo ya kutopanga na kukosa vipaumbele...viwanda ni muhimu, suala la umeme ni critical (tatizo sugu) sasa lakini kuna possibilities (uwezekano) wa kugeuza coal (makaa ya mawe), umeme wa upepo na ule wa Rufiji ambao unazidi hata mahitaji yetu," alisema na kuongeza.

"Kinachotakiwa ni vipaumbele...sasa tuna raslimali watu ambazo zina ujuzi, maarifa na mafunzo. Suala la infrastructure (miundombinu)...ingawa serikali imejitahidi katika hili kwa kujenga barabara nyingi, lakini kuna tatizo la usafiri wa reli. Kuna kila haja ya kushughulikia reli ya kati, TAZARA na reli ya Tanga.

"Tujenge hizo ili mizigo kutoka bandarini isafirishwe, nasikia sasa wanajenga bandari sijui wapi, nyingine ya nchi kavu hapa...suala si kujenga bandari za nchi kavu, muhimu ni kujenga reli ili tuweze kuzifikia nchi jirani...ni changamoto ya kuanza kwa kutumia fursa zote hizo.

"Mimi nafurahi sana siku hizi unawaona Watanzania wanahangaika huku na huko, kila ukipita...hata hii ya machinga ni namna gani wananchi wanajitahidi, tunapaswa kuiona hiyo kama changamoto si laana, maana yake ni kuwa wananchi wako tayari kwa mabadiliko ya haraka, serikali inapaswa kusaidia hapo.

"Tufufue miundombinu yetu, hasa reli, spirit (ari) ya ujenzi wa barabara iliyopo sasa iendelezwe...concetrate on few key issues (kujikita katika mambo machache ya msingi) lazima tujue hilo...lazima tujue tunaondoka vipi kwenda mbele baada ya miaka 50 ya uhuru," alisema Bw. Msuya, ambaye pamoja na umri wa miaka 80 bado anaonekana kuwa na nguvu.

Akijibu swali juu ya ukuaji wa uchumi kitakwimu na kuongezeka kwa umaskini miongoni mwa wananchi walio wengi, alisema pamoja na kuwa serikali haiwezi kuwawekea watu fedha mfukoni, isipokuwa mpaka wanapojishughulisha kwa ajili ya kujipatia kipato, serikali inapaswa kuweka mazingira maridhawa ya shughuli hizo.

Alisema ni watu wachache wanaoweza kupata ajira rasmi za ofisini katika sekta ya umma na binafsi, kwani wengi wa Watanzania wanapata ajira katika kilimo, lakini tatizo limekuwa ni bei ndogo.

"Katika kilimo watu wetu wanajishughulisha kweli, lakini tatizo limekuwa ni bei ndogo, ukiulizia tatizo ni nini utakuta ni gharama za usafiri, tunahitaji kwenda kwa kasi...ndiyo maana nikasema masuala ya miundombinu ya uchukuzi ni muhimu.

"Kwa mfano hakuna haja ya soko kuwa Dar es Salaam tu, kila mkulima aje kupata soko hapa, mkulima aliyeko Rukwa anaweza kuuza nje ya nchi Zambia huko," alisema Mzee Msuya.

Akizungumzia juu ya mazingira ya uwekezaji nchini, alisema kuwa ni mazuri lakini kuna kila haja ya kujikita na kuweka kipaumbele katika miundombinu ya reli na bandari na upatikanaji wa umeme wa uhakika na rahisi, sambamba na mawasiliano ya elektroniki, ili kujiongezea uhakika na uwekezaji.

Alisema hata jiografia ya Tanzania ni fursa ya kipekee inayoweza kutumiwa na nchi kunufaika kiuchumi kwani inazungukwa na nchi nane, ambazo nyingine hazina bahari wala ziwa, hivyo kutokuwa na bandari, hali ambayo inazifanya kutegemea nchi jirani kama Tanzania.

"Miaka 30 iliyopita Dubai haikuwa lolote, it was just a small..., lakini wameibadilisha kuwa moja ya miji mikubwa kama Singapore. Miaka 50 ijayo Tanzania inao uwezo kabisa wa kuwa nchi yenye uchumi wa kati, tunaweza kuweka malengo ya kuwa kama Korea Kusini, hata kama hatutawafikia kabisa, lakini tunaweza.

Mjadala wa katiba mpya

Katika suala la katiba mpya, Mzee Msuya alisema kuwa kuna kila haja ya vyombo vya utendaji kazi hasa vile vya kisheria kufanyiwa mabadiliko ili vifanye kazi inavyopaswa.

Pia alisema ni wakati mwafaka katika mjadala wa katiba mpya, Watanzania waanze kufikiria iwapo kuna haja ya kuendelea kuwa na bunge moja, huku yeye akionea mfumo wa mabunge mawili, ndiyo unafaa kwa sasa nchini kutokana na wabunge kupatikana kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii nchini.

"Sasa hata wasomi wanakimbilia kwenye siasa...tunao wabunge wanatokana na NGO sijui wapi huko, hivyo ni vyema watu wakafikiria hilo.

 
‘CCM kinapitia wakati mgumu'
Saturday, 29 January 2011 08:33

Elias Msuya na Fredy Azzah

KIKIWA kinatimiza miaka 34 tangu kuzaliwa kwake Februari 5, 1977, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelezewa kuwa, ingawa kimeendelea kushinda nafasi ya urais nchini, kinakabiliwa na wakati mgumu.

Wakizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, wabunge wa CCM walisema chama hicho hakiwezi kufa kwa sasa, lakini kinapitia tu wakati mgumu kama ilivyo kwa vyama vingine duniani.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, alisema kwa kipindi cha miaka 34 ambacho CCM imekuwa madarakani, kimefanikiwa kufikia malengo yake hasa kwa kushinda chaguzi zote.


"Chama chochote kile duniani, malengo yake ni kushika dola. Kwa kipindi chote CCM tumefanikiwa kushika dola. Hata kwenye michezo, kama timu inashuka daraja mwenye timu huivunja," alisema Lukuvi.

"Chama cha siasa ni taasisi endelevu, sio kwamba tumeongoza kwa maziwa na asali. Tunapitia kwenye milima, misitu na vichaka.

Ni jukumu letu kujitambua ili tuendelee kushika dola," alisema. Kuhusu suala la Dowans ambalo limeonekana kukigawa chama hicho kabla ya wabunge wake kukutana na kuweka msimamo wa pamoja, Lukuvi alisema hilo haliwezi kukigawa chama."Chama hakiwezi kugawanyika kwa ‘petty issues' (mambo madogo madogo).

Chama kupitia mwenyekiti wetu alishasema jambo hilo sio kubwa. Ni uhuru wa maoni tu, kama ni mawaziri kupingana watakuwa wamevunja kanuni zao, sio chama," alisema.

Naye Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib, alisema sio kwamba CCM imepoteza mwelekeo, bali kinakwenda kulingana wakati ulivyo.

"Sioni kama chama kimepoteza mwelekeo, kinakwenda kulingana na wakati, dunia imebadilika, mahitaji yameongezeka, vionjo vimeongezeka kwa hiyo chama kinakumbana na mazingira ya wakati huu," alisema. Alikitetea chama hicho kuwa, hakiwezi kuleta pepo duniani na kwamba, matatizo yapo duniani kote sio Tanzania pekee.

Kuhusu suala la Dowans, Khatibu alisema kilichotokea ni uhuru wa maoni sio kugawanyika kwa chama. Naye Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Stella Manyanya, alisema kwa kipindi cha miaka 34, chama hicho kimefanya mambo mengi mazuri ambayo yameifikisha nchi hapa ilipo, na bado kina uwezo wa kuongoza miaka mingi ijayo.

Hata hivyo, Manyanya alisema changamoto anayaoiona ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi, ni suala la mawasiliano.
 
lowassa is playing a dirty game that can be summarized as "scratch my back and I will scratch yours too...."

A game that he might even win seeing that Kikwete is lossing control in both the CC and NEC. Kikwete sent his soldiers to do his dirty work but in the end he fails to stand by them. Who will he send next? Why is Nape and Chilligati under investigation for CC decisions? Is it fair for these two to take blame of the problems caused by the indisicive nature of their weak chairman?
 
Pambaf zako, unatuletea ulongo hapa, Lowasa alikalia kiti cha u-PM wakati mradi unaendelea, alipendekeza mkataba uvunjwe-JK akakataa, sasa mbona wadanganya ati alipindisha procurement ACt. Usijidanganye, mwisho wa J K ni mwaka huu.

Kwanini ulisainiwa? mbona husemi unasema kuvunjwa tu? uliposainiwa alikuwa wapi Lowassa? sasa alipoona inamyeshea ndiyo ajidai kuufuta, hapo ndipo nnapompendea Kikwete.
 
A game that he might even win seeing that Kikwete is lossing control in both the CC and NEC. Kikwete sent his soldiers to do his dirty work but in the end he fails to stand by them. Who will he send next? Why is Nape and Chilligati under investigation for CC decisions? Is it fair for these two to take blame of the problems caused by the indisicive nature of their weak chairman?

tyop of your game boy............where have you been hiding denying us this gem of pure wisdom?
 
‘CCM kinapitia wakati mgumu’
Saturday, 29 January 2011 08:33

Elias Msuya na Fredy Azzah

KIKIWA kinatimiza miaka 34 tangu kuzaliwa kwake Februari 5, 1977, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelezewa kuwa, ingawa kimeendelea kushinda nafasi ya urais nchini, kinakabiliwa na wakati mgumu.

Wakizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, wabunge wa CCM walisema chama hicho hakiwezi kufa kwa sasa, lakini kinapitia tu wakati mgumu kama ilivyo kwa vyama vingine duniani.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, alisema kwa kipindi cha miaka 34 ambacho CCM imekuwa madarakani, kimefanikiwa kufikia malengo yake hasa kwa kushinda chaguzi zote.


“Chama chochote kile duniani, malengo yake ni kushika dola. Kwa kipindi chote CCM tumefanikiwa kushika dola. Hata kwenye michezo, kama timu inashuka daraja mwenye timu huivunja,” alisema Lukuvi.

“Chama cha siasa ni taasisi endelevu, sio kwamba tumeongoza kwa maziwa na asali. Tunapitia kwenye milima, misitu na vichaka.

Ni jukumu letu kujitambua ili tuendelee kushika dola,” alisema. Kuhusu suala la Dowans ambalo limeonekana kukigawa chama hicho kabla ya wabunge wake kukutana na kuweka msimamo wa pamoja, Lukuvi alisema hilo haliwezi kukigawa chama.“Chama hakiwezi kugawanyika kwa ‘petty issues’ (mambo madogo madogo).

Chama kupitia mwenyekiti wetu alishasema jambo hilo sio kubwa. Ni uhuru wa maoni tu, kama ni mawaziri kupingana watakuwa wamevunja kanuni zao, sio chama,” alisema.

Naye Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib, alisema sio kwamba CCM imepoteza mwelekeo, bali kinakwenda kulingana wakati ulivyo.

“Sioni kama chama kimepoteza mwelekeo, kinakwenda kulingana na wakati, dunia imebadilika, mahitaji yameongezeka, vionjo vimeongezeka kwa hiyo chama kinakumbana na mazingira ya wakati huu,” alisema. Alikitetea chama hicho kuwa, hakiwezi kuleta pepo duniani na kwamba, matatizo yapo duniani kote sio Tanzania pekee.

Kuhusu suala la Dowans, Khatibu alisema kilichotokea ni uhuru wa maoni sio kugawanyika kwa chama. Naye Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Stella Manyanya, alisema kwa kipindi cha miaka 34, chama hicho kimefanya mambo mengi mazuri ambayo yameifikisha nchi hapa ilipo, na bado kina uwezo wa kuongoza miaka mingi ijayo.

Hata hivyo, Manyanya alisema changamoto anayaoiona ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi, ni suala la mawasiliano.


Dowans ni swala dogo? Kwa maoni yangu Kashifa ya watergate ilikuwa ndogo zaidi, lakini Rais wa dola kubwa duniani ilibidi ajiuzulu. Kwa taarifa yako Roma ilikufa kifo kama cha CCM inakoelekea. Wamelewa madaraka, wanafikiri they are Invincible sawa na Roma ya wakati huo. Wakati ma- Viking na Visigoth wakiingia mjini, Roma ilikuwa imelala usingizi wa mvinyo. Wakateka mji kirahisi. Hata hawa wamelewa pesa iliyotokana na ufisadi. Kama sodoma na gomora hawawezi kuacha maraha yanayotokana na utajili huu. Wakati upinzani unaingia madarakani watakuwa bado wamelala fofofo. Hata hivyo si wanaishi kwa nguvu za dola tu? siku polisi wakishituka wame - Kwishne.
 
Kwanini ulisainiwa? mbona husemi unasema kuvunjwa tu? uliposainiwa alikuwa wapi Lowassa? sasa alipoona inamyeshea ndiyo ajidai kuufuta, hapo ndipo nnapompendea Kikwete.

mpende JK pale atakapomtimua lowassa na kijikundi chake.....................sasa hivi JK anayumbishwa na Lowassa, Sumaye na Mkapa kiasi cha kwamba anataka hata kuwarudi Nape na Chiligati.........................inasikitisha sana.......
 
Dowans ni swala dogo? Kwa maoni yangu Kashifa ya watergate ilikuwa ndogo zaidi, lakini Rais wa dola kubwa duniani ilibidi ajiuzulu. Kwa taarifa yako Roma ilikufa kifo kama cha CCM inakoelekea. Wamelewa madaraka, wanafikiri they are Invincible sawa na Roma ya wakati huo. Wakati ma- Viking na Visigoth wakiingia mjini Roma ilikuwa imelala usingizi wa mvinyo. Wakateka mji kirahisi. Hata hawa wamelewa pesa iliyotokana na ufisadi. Kama sodoma na gomora hawawezi kuacha maraha yanayotokana na utajili huu. Wakati upinzani unaingia madarakani watakuwa bado wamelala fofofo. Hata hivyo si wanaishi kwa nguvu za dola tu? siku polisi wakishituka wame - Kwishne.[/QUOTE]

hawa polisi bora liende watashtuka lini? Nionavyo ni kuwa hawa polisi mpaka tuwatie kiboko ndiyo watashtuka........
 
mpende JK pale atakapomtimua lowassa na kijikundi chake.....................sasa hivi JK anayumbishwa na Lowassa, Sumaye na Mkapa kiasi cha kwamba anataka hata kuwarudi Nape na Chiligati.........................inasikitisha sana.......

Kikwete hayumbishwi na hao, Lowassa ni team moja na Kikwete, siasa ni mchezo mbaya sana, Kikwete kishamaliza muda wake wakugombania madaraka, na zile za kusema uliniambia nilikwambia ni "game" za kisiasa.

Hapo Lowassa anatolewa kimasomaso, fikiri kwanini anaongelea kuuvunja mkataba? kwanini asiongelee kusainiwa? Ukipata jibu lilete.
 
Dowans ni swala dogo? Kwa maoni yangu Kashifa ya watergate ilikuwa ndogo zaidi, lakini Rais wa dola kubwa duniani ilibidi ajiuzulu. Kwa taarifa yako Roma ilikufa kifo kama cha CCM inakoelekea. Wamelewa madaraka, wanafikiri they are Invincible sawa na Roma ya wakati huo. Wakati ma- Viking na Visigoth wakiingia mjini, Roma ilikuwa imelala usingizi wa mvinyo. Wakateka mji kirahisi. Hata hawa wamelewa pesa iliyotokana na ufisadi. Kama sodoma na gomora hawawezi kuacha maraha yanayotokana na utajili huu. Wakati upinzani unaingia madarakani watakuwa bado wamelala fofofo. Hata hivyo si wanaishi kwa nguvu za dola tu? siku polisi wakishituka wame - Kwishne.

Naona kuna watu wanajaribu kila njia kuliingiza jina la Dowans katika yaliyozungumzwa lakini habari za kutoka kikaoni tulizozipata mwanzo, haikutajwa Dowans, ilitajwa Richmond. Kwanini watu wanapenda kucheza na maneno?
 
The key moment: Bunge liligunduwa kuwa RICHMOND ni kampuni feki inayotakiwa kulipwa na serikali ya Tanzania...Kampuni ambayo ina uhusiano na either JK or EL(EL alijiuzulu)

Kabla hayajawa magumu,EL akamvutia waya JK,

JK akamwambia haijalishi,shughuli iendelee,(kwa maana ya kutoa a "go ahead")wakati huo JK akiwa safarini.

Na sasa aliyejiuzulu kasema ukweli,lakini shida moja tunafikiria kwa tofauti na issue hii imekuwa ya kichama zaidi.

Na huku maamuzi yalikuwa ya kiserikali!
 
MWANGWI WA TSUNAMI YA LOWASSA KUPASUA JIPU KWA MAFISADI ORIJINO KULE DODOMA WANANCHI TUNASEMA TUSISIKIE KAPATWA NA HOMA ZA AJABU AJABU, KWIKWI WALA KUDAIWA KUUMWA NA MMBU HUKU TUKIENDELEA KUTAFAKARI UKWELI USI NA MASWALI ULIKOLALA

Wa-Tanzania wenzangu, ni ukweli gani zaidi tunaotegemea kuupata zaidi ya huu juu ya salata la ukwapwaji mkubwa wa kodi zetu kimazingaombe kila kona ya taifa letu?

Wenzangu kama wengine pengine hamkumuamini Jemadari wetu yaani Dr wa Ukweli (Mhe Dr Slaa) juu ya nani nayetuibia, na pia kushinwa kuunganisha nyuzi juu ya kuli ya mwisho ya Rostam Aziz ile ya 'Siasa Uchwara' na hata hichi kimbunga kikali cha Tsunami kilichokipiga Mafisadi Orijino kule Dodoma toka mdomoni mwake mwenyewe Lowassa na kushindikana kubishiwa chochote na yeyote; wananchi bado tunasubiri ujumbe mwingine toka angani au ndio tusemeje??

Kwa kiwango hiki cha ukweli na ukweli mtupu uliomwagwa kwenye mkutano wa CCM Dodoma kushindikana kukimbiliwa kukanushwa na wahusika wa ufisadi wa Richmond / Dowans, wananchi sasa tunasema TUSISIKIE HATA KIDOGO KWAMBA LOWASSA KAUMWA HATA NA MMBU maana mambo yote sasa hadharani sawasawa na jinsi CHADEMA kilivyowahi kutueleza sote kama taifa na hadi ikulu ikataka kupasuka. Leo hii tumebahatika kupata ukweli wote right from the horse-mouth!!!

Nasema Wa-Tanzania tusisikie hata tone kwa Lowassa kapatwa hata na homa isioelezeka undani wake HUKU WANACHADEMA tukiendelea kutafakari kiundani zaidi, kuja kuwashauri viongozi wetu wasikivu jambo gani lifwate, na huo ndio ukweli wa mambo. Ukweli juu ya ufisadi wa ikulu imekuja na mtikisiko mkubwa ambao mwangwi wake hautozimika hivi karibuni.

Wanaharakati ukimya wetu juu ya hili
ni unafiki na usaliti wa UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA unaoonekana wazi kudhalilishwa kiasi hiki na hawa manyang'au ndani ya CCM.

Ngojeni kidogo tutarudi jukwaani tukikamilika zaidi juu ya sakata hili lenye uvunda wa kishetani. Uweza Tunao juu ya haya yote ilmradi kila mmoja wetu ajue haki yake na kutetea ubinadamu, haki na utu kwa kuwa ndio tunu ya kweli ya taifa letu kutuelekeza kwenye amani isiyolazimishwa.

Yote juu ya yote, hata na wewe Lowassa bado haujanikuna akilini kwa kuficha ugonjwa wote huu kwa kipindi hicho chote hadi sasa ambapo 'umaiti wa kisiasa' ulipoonekana kukukodolea macho ndipo sasa unaanza kupiga mayowe na kuamua kupasua jipu 'kabla haujakata kauli'.
 
Back
Top Bottom