Why Doctor Mpoki Ulisubisya?

Serekali ilitaka kumuuwa Lissu period
 
Acha kupotosha umma, Madaktari bingwa wa usingizi kwa sasa wanazidi 30 na sio kwamba hawafiki kumi!! Ni kweli hata hao waliopo ni wachache sana!! Pili Mpoki hajafanya lolote ktk kuongeza idadi yao na yy amesababisha madr 3 wataaluma yke kuresign baada ya kuwahamisha kwa chuki zke binafsi!!. Kuondolewa kwake ni sahihi kabisa maana hajaacha legacy yoyote hapo wizarani zaidi ya kuwa mzururaji tu!
 
Acha shallow thinking, walidhani by 38 bullets (walizommiminia hao wanaogawa vyeo) ameshakufa/atakufa within no seconds....
 
Yote ni dhana tupu, Nawe cha kupotosha umma, amehamishwa kwa vile hakumuua Lisu!
 
 
Yawezekana, hali Ya Mh.Lissu inaendelea kuimarika na atarejea karibuni. Sehemu ya hotuba yake ya kwanza Live, atawashukuru sana team ya Madakitari wa Tanzania wakiongozwa na Dr.Mpoki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Habari mzima umeona swala LA Lisu tu? Kuna nini katika issue ya Lisu ambayo inatia upofu kuona ushauri mpana wa Mwandishi wa hii habari?
 
Kila siku wanapenda kutunga vitu. Wewe ungeleta hoja yako tu kuwa abaki Tanzania kwa sababu ulizozitaja hapo juu baas.
 
Hakuwahi kuwa Balozi kabla kwanini apangiwe kazi ya kuanzisha ubalozi mpya wakati ni mgeni kwenye hiyo eneo? Kuanzisha ubalozi mpya apelekwe mbobezi na yeye apangie kwenye Balozi ambao ni well established
 
Nadhani Hata makanisani na misikitini CHADEMA wako waliwatuma Polisi wasimuombee Lissu, na wasiwaombee mabaya waliotaka kumuua Lissu!

Tanzania ya Leo si ya Jana ndugu, wasomi wapo mtaani hawana kazi, propaganda za kizamani hazina nafasi, you need to update your propaganda.
 
Uko sahihi kabisa.
Taaluma yake bado inahitajika Sana hapa nyumbani kuwahudumia Watanzania kuliko kumpeleka huko ubalozini na kuacha ombwe la kitaaluma hapa nyumbani. Maana kufanya hivyo ni matumizi mabaya ya rasilimali watu ni sawa na kutumia maji ya kunywa ya familia kumwagilia shamba la jirani. Ni vyema wanasiasa watambue mchango wa wataalamu hawa kwa nchi yetu
 
Ukweli ni kuwa serikali ilitaka kumuua Lissu, hilo halina ubishi hata mtoto mdogo anaweza akaelewa. Lakini wazalendo kama Dr Mpoki wakazuia hilo lisitokee. Taarifa nilizonazo ni kuwa Dr Mpoki ndiye aliyeshauri apelekwe Nairobi na viongozi wa CDM wakalosimamia kwa nguvu zote, Spika akaunga mkono kabla hajajua mpango mzima.

Dr Mpoki nenda tu popote Jiwe atakapokupeleka, hata huko Mungu anaweza kukutumia kuokoa maisha ya mtu fulani.
 
Cuba inajulikana kwa kutoa madaktari bigwa duniani hili halina ubishi. Mleta mada, kwa nini hauoni matokeo chanya kwa uwezekano wa Dkt Mpoki kuwa Balozi katika nchi inayotoa madaktari bora duniani!? Dkt Mpoki atafaa sana kuwa kiunganishi muhimu kwa nchi yetu na Cuba katika sekta ya afya.

Mleta mada acha kuandika hisia zako za kichochezi kupotosha umma wa watanzania.
 
Ndugu mwandishi! Ninauhakika kabisa unafahamu nchi ya Cuba ilivyo juu katika maswala ya utabibu (human medicine) unaanzaje ku guess and second guess maswala ya kuokolewa maisa mh. Lissu uache kuamini Dr. Mpoki atapewa agenda maalum kuunganisha vijana wa kitanzania kusomea na kubobea katika taaluma kama yeye huko Cuba ? Hivi unadhani tabibu huyu mmoja ndio panacea kwa matatizo ya watanzania kimaradhi? Tunajua ni mzuri sana kwenye field yake lakini tunahitaji wengi zaidi labda ndio maana atapangiwa kwenda Cuba to organise for that ! Hata kama haitakua agenda lakini kwa usomi na weledi wake basi hata kua mchoyo atawaungamisha vijana wetu huko ! And please remember ! Nobody is indispensable in this world ! Hata uwe nani , ukifa unazikwa na maisha yanaendelea kama kawaida. MSILILETE EXAGERATIONS AND GUESSES ZA AJABU HUMU !
 
Gharama ilotumika kumsomesha huyu dr, utaalamu mkubwa na adimu alionao na umuhimu wake kwenye sekta ya afya unaenda unampa kazi ambayo haihitaji hayo mambo hapo juu!!!! Unatoa maprofessor na doctors vyuoni unaenda unawaangia kazi za ajabu ajabu. Kutukana nimeshindwa ngoja niishie hapa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…