DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 12,622
- 28,460
Mkuu ngoja niweke sawa kitu hapa.Mkuu km mimi nimemwelewa huyu mleta mada yeye anazungumzia kuhusu cycle ya kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine kwa hio ni kwamba hataki hayo anayoyapitia yeye ambayo tayari yapo kwenye lineage yake yafike kwenye kizazi chake kinachofuata maana kwa anavyoona yeye km yeye ni mtu wa tabia fulani basi lazima kizazi chake kitakua na tabia hizo yaan hio haifutiki mfano km ni mtu wa tungi basi kizazi chako kitakua cha tungi pia km ni mtu wa wanaume basi kizazi chako kitakua hivyo ukiwa mtu wa wanawake the same kizazi chako kitafuata njia ile ile uliyopita wewe hapo kabla ni km kinaongozwa njia ile ile uliyopita wewe hapo kabla, sasa yeye anataka njia hio ife anaiua vipi?
Namna pekee ya kuiua hio cycle njia pekee ni yeye asizae mtoto hata mmoja abakie yeye km yeye yeye akienda chini na cycle imefia hapo yaan hapo hakuna namna nyingine. Wapo watu wanafanya hivyo na hawana mtoto hata mmoja mpaka sana yaan anataka akifa yeye na cycle yake imekufa kabisa hakuna kizazi kitakachofuata nyuma kikipita njia zilezile km kizazi cha Tembo au Ngedere.
Siyo kweli kwamba njia pekee ya kuua cycle ni kutokuzalisha. Kuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba baadhi ya experiences za wazazi zinaweza kuacha athari zinazoweza kuonekana kwa vizazi vinavyofuata, lakini hiyo haimaanishi kwamba kila pattern haiwezi kuvunjwa.
Kuna experiment maarufu iliyofanywa na Brian G. Dias na Kerry J. Ressler kuhusu kurithishwa kwa sensitivity ya hofu kati ya vizazi. Walichukua panya na kuwafundisha kuhusisha harufu ya acetophenone, harufu ambayo mara nyingi huelezwa kama inayofanana na cherry blossom, na shoti kidogo ya umeme "mild electric shock", Kila walipokuwa wanawanusisha hiyo harufu waliwapiga shoti hiyo ya umeme ambayo ilikuwa inaumiza kiasi, Baadaye watoto wao, na hata wajukuu wao, walionyesha kuongezeka kwa sensitivity na fear response kwa harufu hiyo, ingawa hawakuwa wamepitia shoti ile ile,Kwa hiyo ni kwamba “watoto waliogopa viashiria vile bila kuwahi kuona shock” , lakini kisayansi zaidi ilikuwa increased sensitivity/fear to that odor cue, si lazima sawa na kuwa walijua tukio lote la shock... si kwamba watoto “walikumbuka tukio” moja kwa moja kama kumbukumbu kamili, ila vinasaba vyao vilikuwa na Kumbukumbu au information ambayo wao hawajawahi kukutana nayo ila iliwaambia wakinusa watapata tukio fulani.
Sasa point ya muhimu hapa ni hii, si kwamba watoto walirithi kumbukumbu kamili ya tukio lile, bali walionyesha increased sensitivity ya ile harufu kadri kizazi kinavyoenda. Utafiti ule ulipendekeza kuwa kulikuwa na mabadiliko ya epigenetic yaliyohusishwa na sperm ya wazazi, kwa hiyo si “memory” ya tukio lote moja kwa moja, bali ni aina ya biological information iliyoongeza uwezekano wa response fulani.
Kwa hiyo inaonyesha kwamba wakati mwingine unaweza ukawa upo ndani ya pattern inayokutisha au inayokuendesha bila hata kujua imeanzia wapi. Inaweza kuwa fear, trauma, tabia za uharibifu, au mazingira ya kifamilia yaliyokaa kwa muda mrefu sana. Lakini ukweli wa pili muhimu ni kwamba pattern haimaanishi sasa kwamba iko milele.
Kikubwa ni kuitambua hiyo pattern na kuanza kuivunja. Iwe ni pattern ya uzinzi uliopitiliza, ulevi, umaskini, violence, neglect, au hata mambo ambayo watu huyaita uchawi wa kifamilia, point ni kwamba ukishaijua una nafasi ya kuibadilisha. Kuvunja pattern hakumaanishi unafuta history yote ghafla, lakini unabadilisha direction ya maisha yako, mazingira yako, choices zako, na malezi yatakayofuata.
Ndiyo maana mimi nasema suluhisho si kutokuzalisha (Kuzaa) , bali ni mtu kujitambua na kujifunza kidogo kidogo kujiondoa kwenye hiyo pattern. Kwa sababu unapobadilika wewe, huwi media au intermediate host wa kupitisha mbele script ile ile kwa nguvu ile ile. Vizazi vinavyokuja havipokei mazingira yale yale, malezi yale yale, na responses zile zile. Hapo ndipo cycle inaanza kufa.
Kwahiyo yeye azae kama anataka, lakini ajifunze kwanza kuitambua hiyo pattern, aifanyie kazi, na aianze kuivunja. Maana cycle nyingi haziishii kwa kukata kizazi, zinaishia kwa mtu mmoja kuamua kuishi tofauti.