Who's the hell is Lewis Makame?


Ilisemwa siku nyingi kuwa Makame hastahili kuwa mwenyekiti wa hiyo tume hata kidogo. Kiravu umri wake wa kustaafu umefika na ameongezewa muda kigezo cha kuongezewa muda kilikuwa nini??? Je hakukuwa na watu wanaofaa kwenye nafasi hiyo. Kuna majaji wastaafu watatu ambao ni wajumbe wa tume je ilikuwa ni lazima wawe pale, hakukuwana watu competent kujaza hizo nafasi? Kiukweli hawa wote watamtetemekea aliyewapa ajira na aliyewa ajira ni, Raisi a Jamhuri ambaye ni Mgombea wa Uraisi.

Katika hali kama hii Unategemea nini?
 
Mkuu tumesema sana hilo lakini serikali ya sisiemu ambayo ndiyo inateua majaji wa mahakama ya rufaa wameweka pamba masikioni.
Neno lako nitalizungumza kwenye sanduku la kura hapo jumapili
 
we muache atoe macho kama kakamatwa ugoni siku ya kupanda kizimbani ikifika ataisoma namba
Wayasalimishe hayo mabox fake tunayoelezwa kutua huko ngerengere kabla hali haijabadilika. Sasa hivi hatuwaoni usoni, this is a new era.
 
Mzee una nafasi kubwa ya kuweka historia na kurudisha heshima yako iliyopotea.

Uwe tayari kuweka historia pale utakapotangaza rais mpya kabisa wa chama kipya kabisa nchi hii.

Kuvuruga uchaguzi kama miaka iliyopita is not acceptable and you may pay for that!

For me kura is not a secret issue, sijaona popote ilipoandikwa sheria kuwa iwe siri! upinzani wana kura zangu zote!!!!! Ila asiposhinda mtu wangu nitakaa chini na kujiuliza swali hili zito
Why on earth did upinzani decided to go for election knowing than NEC is belong to CCM??

Baada ya uchaguzi nadhani ni muda mwingine wa wale wote mnaojiita wanachadema kukaa chini humu ndani na kusafisha jukwaa ambalo limeoza kwa upupu wenu wa ushabiki na kushindwa kujenga hoja zenye mshiko! hakuna hoja, point, utetezi wote wa maana ulio na akili ya wazi unaofanywa na baadhi ya wanachadema inayoweza kuwafanya watu waseme JF ina great thinkers. I may forgive you because of stress and panic this time, but your mess is there! you will need to clean it ASAP whether Slaa will be president or not!

Chadema hoyee!
 
Haya wakuu.
kwa yaliyotokea kwenye vituo vya kupiga kura hayatoshi kuongezea kwenye fomu ya mashtaka dhidi ya makame and the gang?
 
Ucheleweshaji wa kutangaza matokeo unaashiria kuwa Lewis Makame anakaribia kuwa Kivuitu. Hali ninavyoiona si nzuri sana. Je jaji Makame atazinduka na kuacha matokeo ya uchaguzi yawe sawasawa na maamuzi ya Watanzania badala ya CCM na NEC?
 
Pengine tatizo ni uzee! Kuna vijana wengi tu wanaoweza kuendesha NEC kwa uzuri zaidi
 
Ishu ni kumtokezea tu huyu!
Kwanini hakemei mambo mazito hivi?
Nasikia Makamba yuko Shinyanga kujaribu kununua jimbo pale...sijui itakuwaje!
 
Hawa watu wanataka kuleta balaa hapa!!!

I wonder!!!:doh:
 
Hawa watu wanataka kuleta balaa hapa!!!

I wonder!!!:doh:

Tatizo NEC na CCM hawajifunzi. Wamejaa kiburi cha kifisadi, hawajui kuwa nchi siyo ya NEC wala CCM ni ya Watanzania. NEC na CCM wanataka kujaribu kuwachagulia Watanzania wabunge wao na Rais wao. Kama Watanzania wamemkataa JK na kumchagua Dr. Slaa ndivyo wanavyotaka na walivyoamua nchi yao iongozwe na si vinginevyo.
 
Mchakato wa kujenga demokrasia ya vyama vingi haufanikiwi kwa sababu ya matukio kama haya yanayaoendelea. Hapa ndiyo umuhimu unaonekana dhahiri kuwa iteuliwe Tume ya Uchaguzi ambayo wajumbe wake watapendekezwa na vyama vyote vya siasa ambayo ndiyo itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi inatiliwa shaka na vyama vya upinzani kuwa inapendelea upande wa chama cha Mapinduzi. Haki inaonekana haitendeki kabisa. Vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla wake hawana imani na Tume ya Uchaguzi. Kuna umuhimu wa kuwa na Tume ya Uchaguzi ambayo haitiliwi shaka hata kidogo.

Tazama, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anateuliwa na Rais ambaye naye ni Mwenyekiti wa chama Tawala CCM, anaingia katika kinyang'anyilo na wenyeviti wa vyama vingine. Uongo umebaridiri sura, zama hizi ni sawa na zile zama za Mwalimu ambapo, watu walikua wakiwekewa sura ya mtu na mgombea kivuli alaf wanaambiwa wanaambiwa wafanye uchagizi.

Laiti ningekua mimi ni Jaji Makame ningejuzuru katika wadhifa huo kuliko kutumika vibaya kama anavyotumika hivi sasa.
 
Hekima na busara vikitawala anaweza fanya ivyo otherwise atakomaaa mpaka 2015
 
Silipendi hili lizee mpaka basi na mwenzie kiravu wanafiki wakubwa.
 
Kwa uelewa zaidi,ni sawa na mechi ya simba na yanga then timu moja ndio inamchagua refa wake,kwa sababu zake na vigezo ambavyo si vya maridhiano na timu pinzani.Hapo ni wazi aliyemchagua refa ndio atashinda.Huyu Makame alishastaafu,lakini bado akateuliwa kuja kutuibia kura.Prof Mwesiga Baregu ambaye ni mtaalamu wa siasa aliyekwa akifundisha Udsm na mchango wake ulikuwa muhimu wa haki na maendelea saana katika nyanja ya elimu tena chuo chenyewe kilisema hana mbadala na kuna upungufu mkubwa wa wataalam hivyo huduma yake inahitajika sana.Serekali ikasitisha mkataba wake eti muda wa kustaafu umefika,wa muhim uhapa yupi?mwizi makame au mhadhiri BareguNafikiri hii serekali imekuwa sawa na wale wayahudi waliotaka Yesu asulubiwe mpaka kufa,na aachiwe baraba,muovu aliyekuwa kifungoni.Sasa hawa CCM wanatupeleka wapi? Nafikiri wadau wameliona na wakiingia mjengoni nafikiri swala moja wapo ni kuhakikisha swala la tume huru inayokubalika pande zote linafanyiwa kazi ipasavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…