Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,184
Watanzania kumbukeni kuweka ushahidi hata wa picha kwa kila tukio mabalo siyo jema wakati wa uchaguzi maana hawa jamaa wanadhani endapo wananchi watatoana macho wao haiwahusu.....we muache atoe macho kama kakamatwa ugoni siku ya kupanda kizimbani ikifika ataisoma namba
we muache atoe macho kama kakamatwa ugoni siku ya kupanda kizimbani ikifika ataisoma namba
Mkuu umenifumbua macho ajabu.Hata mtandao nec.go.tz wao una leta wasiwasi kama kweli NEC ni chombo kitakachotuhakikishia uchaguzi huru na wa haki. Hivyo ndivyo mtandao wao unavyo-share IP na mmoja wa wagombea uraisi! Kwa namna hii maswali ni mengi sana... kwanini? Na kama ni IP ni ya serikali kwa nini campaign team ya mgombea itumea IP hiyo? je huku si kukiuka sheria za uchaguzi? Wasiwasi wangu ni hapo ndipo kura zinaweza kuchakachuliwa! Lazima tuchunge kura zetu katika kila stage
Hii ni hatari sina imani hata kidogo na hawa watu wa NEC kwani wanaganga njaa na kulinda wale waliobadilisha katiba ili waendelee kuongoza NEC.Mkuu umenifumbua macho ajabu.
sasa hebu ona hii nduluge,
ni kiashiria kwamba kuna mutual agreement ya kubadilishana mawasiliano hapo.
I am soooo doubtful na hili NEC la lewis na kiravu ambao tangu imeanzishwa wao wapo madarakani kutokana na uzoefu wao kuwafaa sana ccm na si taifa
Tume ya uchaguzi ambayo ipo chini ya ccm imekuwa ikifanya kazi kwa maelekezo ya ccm katika vipindi vya chaguzi kama hivi.
Ikumbukwe kwamba pale kenya yule mkuu wa Tume ya Uchaguzi KEC aliamua kusoma matokeo ya kura anayoyajua yeye wala hakufuata mtiririko wa matokeo ya kura yalivyojiri hivyo akaiingiza nchi kwenye machafuko kwa UJASIRI WAKE WA KIJINGA.
Endapo kaka yangu Lewis makame na komredi mwenzake Rajab Kiravu wakijijasirisha kufanya kama wafanyavyo miaka yote basi wajue kwamba pamoja na mtawala wa sasa kufanyiwa booking The Hague, Lewis atakuwa ndiye mtuhumiwa namba moja endapo kutatokea hamaki ya wananchi kukataa kuchakachuliwa kura zao.
Yes Mtuhumiwa namba moja ni Lewis Makame, orodha inaendelea.
Hata mtandao wao nec.go.tz una leta wasiwasi kama kweli NEC ni chombo kitakachotuhakikishia uchaguzi huru na wa haki. Hivyo ndivyo mtandao wao unavyo-share IP na mmoja wa wagombea uraisi! Kwa namna hii maswali ni mengi sana... kwanini? Na kama ni IP ni ya serikali kwa nini campaign team ya mgombea itumea IP hiyo? je huku si kukiuka sheria za uchaguzi? Wasiwasi wangu ni hapo ndipo kura zinaweza kuchakachuliwa! Lazima tuchunge kura zetu katika kila stage