WHO: Takriban nusu ya watu duniani watakuwa na matatizo ya macho kufikia 2050.

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
Na Dr.Kenge MD,
Jini makini,vidole Madini
2024,

Tabasamu la furaha linashamiri nyusoni kwa wengi.Ni saa ya Kirumi inaposoma kukamilika kwa Majuma 365 ambayo kwa wanajiografia wanasema "Earth completes its orbit within 365½ days" .Kukamilika kwa mzunguko wa dunia ambao ndani kuna misimu minne ikiwemo Kiangazo,kipupwe n.k.Hakika kukamilisha Siku 365 huku ukipumua ni jambo la kushukuru sana.Kwani tunapitia mengi kwa nyakati tofauti.

Kadharika,Wengine wamejawa na hudhuni kutokana na mabalaa,Majanga na Maradhi kadha wa kadha yanayofanya tusifurahie kukamilika kwa kalenda ya kirumi/Kisayansi.Tuzidi kupambana na changamoto zinazotukabili ili tufikie malengo yetu 2024.

W.H.O
Shirika la Afya duniani WHO limekua msitari wa mbele kuhakikisha Afya ya dunia kwa ujumla inaimarika.Tafiti zinaonesha kwa mujibu wa WHO "kufikia 2024 Takriban 50% ambayo ni nusu ya dunia watakua na matatizo na macho(Vision defects)"

Currently(Hivi sasa) Tafiti zinaonesha "Takribani 20% ya dunia wameripotiwa kuwa na matatizo ya Afya ya macho" Hii ni takriban watu Billion 2.2 dunia nzima.Hivyo ukisimamisha watu 10 basi wawili kati yao wanamatatizo ya macho.Kwahiyo kufikia 2050 idadi itaongezeka.Ukisimamisha watu 10 basi wa tano kati yao watakuwa na matatizo ya uoni.
_fd9a103d-84a3-4d6b-82c5-6ed9232435e9.jpeg

Kutokana na Taarifa hizi.Case za macho ndio zinaongoza kuripotiwa kwa sasa ambapo kuanzia 2019 Covid-19 ilipiku na sasa Imerudi Top as the most reported global case.

SABABU?
Sababu ni nyingi kuna zinazoelewela na zisizoeleweka lakini kwa uchache sababu ni kama:

1.Athari za mwanga wa vifaa vya kieletronic(Blue rays)
Mapinduzi ya Technology hayajawahi kumuacha mtu salama.Licha ya kwamba Vifaa kama Simu,PC,Tablets n.k vinatusaidia kurahisisha maisha ya kila siku.Vilevile Vifaa hizi hutoa mionzi ambayo ni hatarishi kwa Cell za macho hivyo kupelekea matatizo ya Uoni kwa watu wtumizi wa muda mrefu.

2.Urithi/Genetics
Gene au Vinasaba kama Familia inahistoria ya kuwa na matatizo ya macho kwa wazazi(Baba au Mama) basi na kwa watoto wako hatarini sana kupata matatizo ya macho.

3.KAZI
Madereva wa masafa marefu hasa mida ya Usiku..secretaries.Watu wanaofanya kazi kwenye Kompyuta n.k pia wapo hatarini kupata matatizo ya Macho.

4.UMRI
Watu wenye umri kuanzia miaka 45+ wako hatarini kupata matatizo ya macho.

5.MAZINGIRA.
Kwa wanajiografia watakubaliana kwamba kuna muda jua na vitu vya angani hutoa mionzi hatarishi sana (UV-Light) ambazo hupelekea matatizo mbalimbali kama kansa ya ngozi,Macho n.k
_bc5b8929-51ac-4ee9-8fe4-9bd7a19ede91.jpeg

TIBA
Hapo zamani kidogo Kulikua hakuna Tiba mbadala ya macho zaidi ya kuvaa miwani.Lakini mapinduzi ya Techlojia ambayo tulisema ni hatari.Lakini ndio yaliyoleta Tiba mbadala mbalimbali kama vile operation za macho kwa kutumia Laser technology(LASK)ambayo ni gharama kubwa ,Contact Lens na Miwani za kawaida ambayo ndio inaonekana ni Tiba rahisi na Salama

ZINGATIA
Unaweza kuchukua Tahadhari kabla ya hatari.Hapa mabeberu(wazungu) wanazingatia sana
mfano:
Beberu Kabla ya kutoka anahakikisha anajua hali ya hewa anapoelekea kama ni Jua utamuona na Sun-glass wao wanaita Sunny days

kama ni mvua(Rainy days) utamuona na miwani ya mvua au beach utamuona na miwani ya kuogelea.

kwenye Kazi za Kutumia vifaa kama Simu,PC kuna miwani maalumu zinaitwa "Bluecut rays" hizi zinazuia athari za mionzi ya manga

Pia kuzingatia Matumizi ya vifaa vya mawasiliano kama Simu kwa muda mrefu ambayo wengi ndio addiction kabisaa.

Hivyo 2024 tuzingatie Afya ya Macho na magonjwa mengine ili tuishi vyema

Nawasilsha
Wako Mtiifu,KENGE 01
kazi kweliKweli / Job TrueTrue
CC Mjanja M1
 
Sawa gani ya kutibu kwa ambae tayari anavaa miwani apone asivae miwani?
LASK
Ni operation ndogo inafanywa na Technology ya Laser kushape cornea(lens) zako...Pia watu huogopa aina hii ya Tiba japo haina madhara na inatibu kwa 80% unatupa miwani...Bei yake imechangamka jicho moja ni $1000 double $2000
 
LASK
Ni operation ndogo inafanywa na Technology ya Laser kushape cornea(lens) zako...Pia watu huogopa aina hii ya Tiba japo haina madhara na inatibu kwa 80% unatupa miwani...Bei yake imechangamka jicho moja ni $1000 double $2000



Inafanyika wapi? Nchi gani ?
 
Hapahapa TZ niliona jamaa wanajiita Internationa eye care kama sikosei..Lakini unaweza kuulizia CCBRT ...Kama kipato kinaruhusu nenda SA,India



Ahaa okey!

Hao international eye ni Tuckish bila shaka itakuwa ni wale wa hapo Victoria Bagamoyo road

Nimekuelewa
 
Back
Top Bottom