who is this muccadam????????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

who is this muccadam?????????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngambo Ngali, Dec 18, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amemjia juu mmiliki wa kiwanja cha Palm Beach kwa kumtaka aende mahakamani haraka na kwamba haogopi vitisho.
  Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka alisema hayupo tayari kumuomba radhi na kwamba, fedha alizotaka alipwe kama fidia ya kuchafuliwa, hatazilipa.
  Alisema yupo tayari kupelekwa mahakamani na kwamba, haogopi vitisho kwani anachokijua ni kwamba, sheria itafuata mkondo wake na si vinginevyo.
  Profesa Tibaijuka alisema maamuzi ya mmiliki huyo anayaheshimu kwani ana haki kwenda kumshtaki mahakamani.
  Alisema taarifa iliyotolewa na Muccadam kwenye vyombo vya habari inayodai kuwa tayari amemuandikia barua, haina ukweli kwani hadi sasa hajaipata.
  “Unajua huu mkasa haupo kwake peke yake. Ni watu wengi umewakuta. Ila yeye anataka kujifanya kama ni mtu special (maalum). Jambo hilo haliwezekani. Sheria itachukua mkondo wake,” alisema Profesa Tibaijuka.
  Alisema kiwanja hicho namba 1006, kina miaka zaidi ya 30 na kwamba, viongozi waliomaliza muda wao waliwahi kusema kuwa ni cha umma ila yeye anataka kutumia nguvu.
  Alisisitiza kuwa maeneo yote, ambayo ni mali ya umma yaliyonunuliwa na watu binafsi, lazima serikali itayarudisha.
  Alisema upangaji wa miji unatakiwa nidhamu na kusisitiza kuwa kesi ya kiwanja hicho ni rahisi sana.
  Profesa Tibaijuka alisema atafanya kazi kwa mujibu wa ramani iliyopangwa kwani hiyo ni moja ya kazi zake.
  Mwanzoni mwa wiki hii, Profesa Tibaijuka alifanya ziara kuzungukia maeneo ya umma na kubaini viwanja vya Ocean Road na Palm Beach vikiwa vimejengwa na kuagiza vibomolewe haraka kutokana na kuwa mali ya umma.
  Hata hivyo, mmiliki wa kiwanja cha Palm Beach, alikaidi agizo hilo, badala yake alimpa waziri huyo siku saba kumuomba radhi kwa madai ya kumchafulia jina kwa kuambiwa amenunua kiwanja cha umma kwa njia za kinyemela.
  Pia alimtaka waziri huyo kumlipa Sh. bilioni 2 na kutishia kwamba, atampeleka mahakamani asipotekeleza mambo hayo.  CHANZO: NIPASHE

  Mucadam ni nani, kwa nini atake special treatment?
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni muhindi mmoja ambaye anayejua haki hupatikana mahakamani.
  Tatizo la mawaziri wetu wanapenda maigizo sana,sikuona haja ya waziri kutembelea maeneo ya wazi ili kutoa tamko la serikali,anataka kuonekana mkali?hajui kuna watu ni wabishi by nature.huyo muhindi alishatambua kile kinachoitwa "worst case cenario"hivyo anafurahia jazba za Tibaijuka.
  Ushauri wa bure kwa mawaziri;wajitahidi kuwa execative zaidi mfano Tibaijuka angeweza kuwaita (mara moja) watu waliochukua maeneo ya wazi na kuwaamuru kuyarejesha tuseme ndani ya siku 7(kumbuka enzi za mrema)
  huu ndo ubaya wa kuchakachua serikali haitaheshimiwa kamwe!
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Dec 18, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  populism at work?
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kama kuna mtu mwenye picha naomba atuwekee na mm nimo nikiitafuta
   
 5. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hawa watu wamezoea kutumia mahakama kuvunja taratibu kwa sababu ya pesa zao, dawa ya watu hawa ni 'dark justice' tu!
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kama anajua sheria, mbona nasoma kuwa anatembea na barua za ikuluzinazohimiza apewe kiwanja badala ya hukumu za mahakama. Ikulu na viwanja wapi na wapi.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hivi hujui kuwa nchi hii yeyote mwenye cheo kikubws ana uhuru wa kufanya lolote alitakalo? Ndio maana unaona hizo barua za ikulu za kugawa viwanja
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bongo bana kuna mambo!!!!!!
   
 9. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Usituambie kuwa Mkwere naye anaandika barua za kugawa viwanja! Makubwa haya! Ama kweli Tz mna Rahisi!!
   
 10. m

  mams JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tibaijuka kaza buti usonge mbele. Tunataka tuone utendaji wa mahakama zetu na nguvu ya pesa.
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama ni barua za Mr Mkwere!!! Ni sku nyingi sana haya yalitokea...
   
 12. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  He is just a pain in the ass like Rostam Aziz
   
Loading...