#COVID19 WHO: Athari ya Kirusi cha Omicron ipo juu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limesema leo kwamba athari inayotokana na aina mpya ya kirusi cha Omicron bado iko juu baada ya idadi ya maambukizo ya virusi vya corona kuongezeka kwa asilimia 11 kote duniani wiki iliyopita

Katika taarifa yake ya kila wiki kuhusu udhibiti na kuenea kwa virusi vya corona, WHO imesema kuwa kirusi cha Omicron kinahusika na ongezeko la kasi la virusi hivyo katika mataifa kadhaa ikiwa ni pamoja na yale ambayo tayari yalikuwa na udhibiti wa kirusi cha Delta

WHO imeongeza kuwa ushahidi thabiti unaonesha kuwa kirusi cha Omicron kina ukuaji wa haraka zaidi kuliko kile cha Delta na uwezo wa kuongezeka mara mbili katika muda wa siku mbili hadi tatu huku ongezeko la maambukizo likishuhudiwa katika mataifa kadhaa yanayozijumuisha Uingereza na Marekani

Chanzo: DW Swahili
 
Back
Top Bottom