Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,354
- 18,627
Rwanda na mataifa mengine 11 yatanufaika na ufadhili mpya wa Marekani kwa ajili ya dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Kupitia ushirikiano wa Marekani na shirika la Global Fund zaidi ya watu wengine milioni moja duniani watapatiwa dawa hiyo iitwayo Lenacapavir.
Hapo kabla Marekani ilifadhili utoaji dawa hiyo kwa watu milioni mbili katika mataifa 9 duniani. Ufadhili mpya uliotangazwa jana, umeziongeza nchi nyingine 12 ikiwemo Rwanda, Morocco, Thailand, Fiji na Jamhuri ya Dominica.
Wanasayansi wanasema dawa hiyo inayotolewa mara mbili kwa mwaka kwa njia ya sindano imethibitika kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia 99.9.