white blood cells

kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,346
1,676
Kwa madaktari JF,
Je,mtu mwenye "white blood cells" chache mwilini na kadiri ya vipimo vya kitaalamu hana maaradhi yanayomsumbua kwa wakati huo,anapaswa afanye nini ili kuuwezesha mwili kuzizalisha kwa wingi zaidi ili ziweze kufikia viwango vya kawaida kwa mwanaume mtu mzima? Je, kuna dawa gani au vyakula gani vya kuwezesha hilo?
 
Kuna white blood cells za aina nyingi, na zote zina kazi tofauti kulinda mwili na magonjwa mbali mbali (aina ya granulocytes: neutaphils, basophils, eosinophils...aina ya agranulocytes: lymphocytes, monocytes, macrophages)...na hivyo sababu inazofanya aina moja kuwa nyingi au pungufu, sio lazima ifanye hivyo kwa aina nyingine ya WBC. Ungekuwa specific umeambiwa aina gani ya WBC imepungua, au kutoa profile ya aina zi=ote za WBC zikoje...ungeweza kupatiwa ushauri mzuri zaidi. Lakini ukisema tu WBC zimepungua...ni vigumu kutua zipi na lipi lifanyike!
 
kula vizuri,mazoezi,punguza mawazo,hasa kula vizuri mbogamboga,matunda na maji kwa wingi
 
Jamani mbona mmeniandama??? mi nimetoa shauri, kama unamaoni tofauti si utoe pia? Asante Dr Riwa kwa kunikosoa kitaalam, sito rudi tena. :)
 
Jamani mbona mmeniandama??? mi nimetoa shauri.

... Mkuu !
Mi tu umenikumbusha mbali hapo juu! Namkumbuka Dr wetu [ ACO]
enzi hizo tuko primary.

Ukifungua mlango tu kishaanza kuandika,ukiketi anakuuliza jina,umri,kabila,utokako... Then anakupa cheti ukachukue dawa kabla hujajieleza uumwacho.

Ajabu wenyewe tulikuwa tunampenda vile anavyovuta benchi fasta,ukifika hukai foleni muda mrefu...
Mwenyewe akawa anajiita Mzee wa SPOT DIAGNOSIS.

[ CAUTION: Simfananishi nawe,ila hilo jibu ulilolitoa kwa jamaa limenikumbusha enzi hizo za mwalimu,nimecheka hadi machozi].
 
Kuna white blood cells za aina nyingi, na zote zina kazi tofauti kulinda mwili na magonjwa mbali mbali (aina ya granulocytes: neutaphils, basophils, eosinophils...aina ya agranulocytes: lymphocytes, monocytes, macrophages)...na hivyo sababu inazofanya aina moja kuwa nyingi au pungufu, sio lazima ifanye hivyo kwa aina nyingine ya WBC. Ungekuwa specific umeambiwa aina gani ya WBC imepungua, au kutoa profile ya aina zi=ote za WBC zikoje...ungeweza kupatiwa ushauri mzuri zaidi. Lakini ukisema tu WBC zimepungua...ni vigumu kutua zipi na lipi lifanyike!

... Mkuu Dr Riwa,thanx for everything ! Naku admire sana mzee ! Tatizo simu yangu [Nokia E61 ì] haina pa kugongea LIKE [labda].... All in all kilichopo moyoni mwangu ni zaidi ya maneno yanavyoweza kuongea !!!
 
Pole.
Ni vizuri pia ukaweka bayana jinsi unavojisikia, mwilini una tatizo gani
Homa?
Kukonda?
Apetait mswaki?
Maumivu?
Uvimbe?
Vidonda?
Nini?
One cannot treat lab results, they treat patient!
 
Asanteni nyote kwa michango yenu wakuu!
Ni kwamba mhusika alifanya "full blood picture" na hakukutwa na ugonjwa wowote,pia vipimo vya "cancer" vilionyesha "negative" ila tu wbc zilikuwa pungufu ya 4000 ila zaidi ya 3000.Daktari mpimaji aliuliza kama mhusika ametumia dawa za malaria karibuni na jibu ni hapana.Kadiri ya maelezo ya daktari mpimaji chanzo chaweza kuhusisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na dawa alizotumia mhusika karibuni, baadhi ya "preservatives" zinazowekwa kwenye vyakula vya makopo, sumu mbali mbali zilizo ktk hewa, nk.
Ndio maana swali halikukita kwenye chanzo cha upungufu huo bali kwenye "way forward" kwa mhusika kuuwezesha mwili ku "boost" uzalishaji wa "white blood cells" wenyewe.
 
Kama alivyosema Riwa,

Taarifa kama hiyo haina maana yoyote kubwa na haiwezi kumsaidia Daktari kufikia diagnosis yoyote. Hata daktari aliyempa hayo majibu ama haelewi anachoongelea au ameamua kumwambia hivyo mgonjwa kwa kuhisi kwamba mgonjwa mwenyewe labda hawezi kufahamu undani wa tatizo lake.

Kama una majibu yenyewe, basi jaribu kuyaweka hapa ili tuone hasa ni aina gani ya cell nyeupe zilizoathirika.....Pamoja na kwamba hiyo inaweza kuwa meangful, bado haiwezi kutoa hitimisho hadi mambo mengine yanayohusu mgojwa (history of the desease, findings on examination and further lab investigatiins) yapatikane.

Kwa sasa jaribu kutafuta specialist wa mambo ya damu (haematologist) ili akupe ushauri zaidi. Ukikwama tuwasiliane ili nikuelekeze kwa jamaa anayefanya kazi muhimbili akusaidie.
 
Pole.
Ni vizuri pia ukaweka bayana jinsi unavojisikia, mwilini una tatizo gani
Homa?
Kukonda?
Apetait mswaki?
Maumivu?
Uvimbe?
Vidonda?
Nini?
One cannot treat lab results, they treat patient!

Mhusika sio mgonjwa na hajisikii vibaya kwa namna yoyote,aliamua tu kufanya uchunguzi wa kina wa afya yake.Vipimo alivyofanyiwa vinathibitisha kuwa mwili wake uko "fit" kwa maana ya kwamba "organs" zote zinafanya kazi bila hitilafu yoyote, na pia hana maradhi yoyote yatokanayo na "bacteria" wala "virus".Ni kwamba tu "White Blood Counts" zilikuwa chini ya 4000 japo ni juu ya 3000!
Ni kwamba yeye anataka tu kuimarisha zaidi hiyo afya yake kwa kuuwezesha mwili wenyewe uzalishe "maaskari" wa kutosha!
 
Kumbe ulikua umesha enda kwa daktari? Umetuuliza kwa kututega au?
 
Kumbe ulikua umesha enda kwa daktari? Umetuuliza kwa kututega au?

Sio kutega mama, nataka kupata darasa kama kuna namna ya kuuwezesha mwili ku "boost" uzalishaji wa wbc kama vile ambavyo mtu anashauriwa kula vyakula fulani kuimarisha ubongo, au nguvu ya macho, au uzalishaji wa mbegu za kiume nk. nk
 
hongera kwa kuwa nazo chache ingawa si nzuri sana,uchache huo unaashiria hauna infections sana ila una deffciciency ya wbc,nakushauri utumie vyakula vyenye vitamibi na proteiin za kutosha na madini mbalimbali ya chumvi kama vile iron.DR.sikira(Riobizo)from muhimbili university
 
Asante sana Dr. Sikira, naona we umenielewa vema na unaniongoza ktk njia niliyoitarajia!
Naomba uniweke sawa zaidi kuhusu vyakula vilivyo na wingi wa:
i. Vitamin B
ii. Protein (nje ya nyama, samaki na maharage/kunde)
iii. madini mbali mbali ya chumvi
nk nk
 
Chembchembe nyeupe za damu katika mwili hufanya kazi ya ulinzi kawaida binadamu mwenye afya anakuwa na WBC 4500-11000mm3 hivyo vitu vinvyoweza kusababisha kushuka ni pamoja na VIRAL INFECTION, Miale kama kwa wale wanaotumua Radiotherapy pia LEUKAEMIA yaani kansa ya damu pia Parasitic infection kama Minyoo vile Magonjwa ya ini Chemotherapy hayo ni baadhi ya matatizo ya jumla yanayoweza kusababisha white blood cells zishuke na unote kuwa si HIV ndio inashusha white cells la .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom