While Zitto is being attacked pls read here

Kitila Mkumbo

Sahihi zaidi wapo tunaomuelewa na kile anacho ki present tunakielewa!asante mkuu kwa fikra elekezi!
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama Zitto ana matatizo na ku review mikataba, alichokuwa anaongelea Zitto ni kusababisha unecessary Panic kwa wawekezaji kwakuw abado sisi kama nchi tunawahitaji hawa.

Look here mister.

Hii tabia ya kusema tunawahitaji hawa wawekezaji zaidi kuliko wao wanavyotuhitaji ndio inatufanya kuingia mikataba mibovu; gesi na mafuta yetu yasipochimbwa kwa terms zitakazotunufaisha sisi , hiyo gesi na mafuta kwani yataoza?

Gesi na mafuta sio kama nyanya za Ilula!! Lazima tusimame imara kulinda maliasili ya nchi yetu kwa faida yetu na vizazi vijavyo; Acheni akili ya mkweree ya kuuza nchi na wanyama wetu bila kufikiria wajukuu zake watafaidika vipi baada ya yeye kwenda kwa muumba wake!!
 
Tatizo la mitanzania mingi inaacha kujadili hoja inajikita kumjadili mtu na wakenya wanazidi kutuacha kimaendeleo
 
kwaio wewe kama kiongozi wa chama unakub ali kwamba zito anachukiwa ndani ya cdm...bora wewe umeongea ukweli maana kosa lake atokei kaskazini.

Kiswahili jamani, tafdhali, hivi tatizo la shule za kata mpaka kwenye kiswahili? Anyway ujumbe umefika lakin
 
Hadi nahisi hatuna akili, yaani hatujadili hoja hata kidogo, ni Zitto Zitto Zitto. Inasikitisha na kukera
Tatizo la mitanzania mingi inaacha kujadili hoja inajikita kumjadili mtu na wakenya wanazidi kutuacha kimaendeleo
 
Labda tungeipata mikataba hiyo tukaona 'termination of agreemant' inasemaje.

Kuna baadhi ya mikataba kama ukizubaa makampuni ya nje huwa yanapenda kusema, huwezi terminate mkataba hadi wao waamue, so kama tulilala kwenye hii term tunaweza kupoteza vile vile.

Halafu Pan African kutotimiza obligations zao ni uzembe wa TPDC wenyewe, maana kama malipo halali hayajafanyika wao wako wapi?
 
Labda tungeipata mikataba hiyo tukaona 'termination of agreemant' inasemaje.

Kuna baadhi ya mikataba kama ukizubaa makampuni ya nje huwa yanapenda kusema, huwezi terminate mkataba hadi wao waamue, so kama tulilala kwenye hii term tunaweza kupoteza vile vile.

Halafu Pan African kutotimiza obligations zao ni uzembe wa TPDC wenyewe, maana kama malipo halali hayajafanyika wao wako wapi?

rudi tu chichat bidada,uku hupawezi...
 
Moja ya matatizo yetu kama nchi na wananchi ni kuchukia watu wanaofikiri tofauti. Tumezoea mazoea; ukiona mtu anaenda tofauti na mazoea tunaanza kumpa majina kibao: kanunuliwa, msaliti, anajipendekeza, hana ushirikiano, n.k.. Lazima tubadilike na kujua kwamba binadamu tu tofauti kimwili, kiakili na kila kitu. Ili tutoke hapa tulipo lazima turuhusu akili zifikirii sawasawa na tena tuhangaike kufikiri kitofautitofauti. Kama tunataka kila mtu afikiri kama sisi ni kuendeleza utamaduni wa kutumia akili za kuazima. Zitto ni miongoni mwa watu wachache hapa nchi aliyeamua kujipambanua na kuamua kufikiri kitofautitofauti. "Kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. Zitto analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea. Atabambikizwa majina yote ya ovyo kama usaliti, kujipendekeza, n.k. Tunamtia moyo aendelee kuhangaika kufikiri, wapo watakaomuelewa.
Mkuu, naamini wengi watampa support Mh. Zitto baada ya kujua anaongelea nini. kikubwa tuwaelimishe wananchi wajue anachojaribu kukipigia kelele ili na wao waongee lugha moja na Mh. Zitto na sisi tunaoamini he is doing the right thing.
 
Mazuri ya Zitto yalisahaulika pale alivyo weka wazi kutaka kuchukua nafasi ya Slaa, wapambe wa kina Slaa humu JF wakatumwa wamchafue.
 
Mbona wacha ngiaji kwenye mambo ya lugha za kigeni wanapungua, naamini asilimia kubwa ya mawazo aliyonayo Zitto ni mazuri kwa maendeleo ya Taifa letu ila kuna watu ambao wamefundishwa na wamelelewa na makundi ya watu fulani kubisha BUT Hon Zitto dont give up, you will overcome all tyranny.
Ah! Lugha ya wakoloni hiyo ndiomaana wachangiaji wengi wanaikwepa.
 
Mkuu, naamini wengi watampa support Mh. Zitto baada ya kujua anaongelea nini. kikubwa tuwaelimishe wananchi wajue anachojaribu kukipigia kelele ili na wao waongee lugha moja na Mh. Zitto na sisi tunaoamini he is doing the right thing.
tatizo viongozi wenzake wanamchafua kwa kuogopea viti vyao. Anapigwa vita kwa sababu ni peke yake mwenye nia safi CDM.
 
moja ya matatizo yetu kama nchi na wananchi ni kuchukia watu wanaofikiri tofauti. Tumezoea mazoea; ukiona mtu anaenda tofauti na mazoea tunaanza kumpa majina kibao: Kanunuliwa, msaliti, anajipendekeza, hana ushirikiano, n.k.. Lazima tubadilike na kujua kwamba binadamu tu tofauti kimwili, kiakili na kila kitu. Ili tutoke hapa tulipo lazima turuhusu akili zifikirii sawasawa na tena tuhangaike kufikiri kitofautitofauti. Kama tunataka kila mtu afikiri kama sisi ni kuendeleza utamaduni wa kutumia akili za kuazima. Zitto ni miongoni mwa watu wachache hapa nchi aliyeamua kujipambanua na kuamua kufikiri kitofautitofauti. "kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. Zitto analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea. Atabambikizwa majina yote ya ovyo kama usaliti, kujipendekeza, n.k. Tunamtia moyo aendelee kuhangaika kufikiri, wapo watakaomuelewa.

kusoma sana siyo kukomboka kiakili.taifa letu limefika hapa sababu ya ma profesional perperte kama kitila na zitto.hawa majamaa wawili kila mwanacdm makini anajua ni mandumila kuwili.ni vigumu sana mimi kufikiri sawa na hawa jamaa.wasilazimishe tukubaliane na ujinga.hivi nani asiyejua kuwa zk aliunga mkono ununuzi wa mitambo ya kifisadi ya dowans?nani asiyejua zk alipinga chadema kutoka bungeni kuonyesha kwao kutoridhika na mfumo wa uchaguzi tanzania?nani asiyejua kuwa zk amejitenga na viongozi wenzake wa chama?nani asiyejua kuwa zk huwa hashiriki matukio ya kitaifa ya cdm kama zinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010 jangwani,m4c,je ukaribu wa zk na r.aziz na jack zoka je?siasa si uadui lakini kuunga mkono unafiki wa zitto yakupasa uwe na akili ya maiti.hawa wote wametumwa kazi maalum chadema.tulishawastukia.
 
tatizo viongozi wenzake wanamchafua kwa kuogopea viti vyao. Anapigwa vita kwa sababu ni peke yake mwenye nia safi CDM.

Nafikiri viongozi wenzake kwenye hili hawahusiki kwani sijaondoka mahali wametoa tamko wala kafanya lolote, ila Neruda kusema kuwa ZItto anapaswa kusema yeye anamasilahi gani na mikataba iliyokwisha kusainiwa kwani anahusika kwa kuwa yeye ni mshauri wa masala ya kimchi I kwenye septa ya mafuta na gesi kwenye kampeni ya Mawakala ya MKono sasa yeye anaongea nini wakati Ndio alishiriki kukaa meza moja na wawekezaji?

Namtahadharisha ZItto Kama nilivyofanya wakati wa mhando , kuwa akae kimya kwani sasa anajionyesha wazi rangi zake na nawaambia viongozi wenzake kwenye chama kuwa wanapaswa kujua hayuko upande we wanna hi tena .

Ntarejea
 
WIMBO WA KUTENGANISHA 'WAZO' NA 'MTOA WAZO' NI MTAMU SANA LAKINI SI KWA MASIKIO YOTE WAKATI WOTE NA KWA MAZINGIRA YOTE KWA USAWA ULE ULE

Siku zote MAWAZO MAPYA(new ideas) huumbwa na mtu na ukweli huu hata rafiki yangu Dr Mkumbo analifahamu vema.

Sasa kwa kuzingatia mantiki kwamba hata siku moja mawazo mapya kamwe hayana uwezo wala miguu ya kujisimamia yenyewe isipokua ni mpaka awepo mtu mahala mwenye moyo, muda na msukumo wa kulisimamia hilo wazo jipya ndipo lenyewe liweze kufanyiwa kazi na matunda kuweza kuoneka, basi hadi hapo misingi hoyo yote kati ya UJUMU kwa upande mmoja na MUUMBA UJUMBE kwa upande mwingine ni sharti kutazamwa kwa pamoja pindi mtu unapokua serious kufanyia tathmini wazo husika.

Hivyo basi, Great Thinkers kidogo napata shida wengine mnapojaribu hapa kutusukuma tumini ya kwamba njia pekee na sahihi kwa nyuzi joto za vipimo vyenu ni kule kufanyia tathmini wazo tu (Idea Appraisal) bila kutekeleza nayo tathmini ya muumba ujumbe (Idea Orijinator Appraisal).

Sote tunakubaliana kwamba, kwa mfano tu, kunapozungumziwa mtu kuibuka na wazo la tuseme kitu 'MPANGO MZURI WA MATUMIZI YA RASILMALI ARDHI' - hadi hapo ujumbe tunao juu ya mambo gani yatakiwa kupewa kipaumbele katika watu husika kuweza kutumia rasilmali hiyo kwa faida zaidi kwao. Nasema hadi hapo huo ndio ujumbe unaotakiwa kujdiliwa.

Pamoja na yote, itakua ni ajabu ya kihistoria kwa watu wanaojiita Great Thinkers kuhiari tu kuacha kumjadili pia mtoa wazo ili tupate kujua MAZINGIRA ALIMO NA JINSI GANI MAZINGIRA HUSIKA itakua imechangia kushawishi na kuumba mtazamo wake mzima hadi kuzaliwa kwa wazo hapo juu ya matumizi bora ya rasilmali ardhi. Ili kupata kuendana na hoja yangu hapa ni muhmu kutambua ya kwamba wazo la 'MATUMIZI BORA YA RASILMALI ARDHI' itakua ni ile ile ila ufanisi wa utekelezaji wake unatuamuru kwamba kwanza lazima tujiridhishe na mtoa wazo pamoja na mazingira anamotoka ili sasa tunapotengeneza mkakati kuwepo na uumano kati ya na mazingira ambako wazo husika lahitajika kutekelezwa kwa mafanikio.

Naam, ninachomaanisha hapa ni kwamba wazo hapo juu japo ni maridhawa kweli kweli ila utekelezaji wake katika mazingira halisi ni mpaka upate kwanza jibu kwamba mtoa wazo hilo la 'MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI' ni nani hasa yeye na anatokea wapi ambapo kuna historia gani vile: Ukweli ni kwamba wazo la 'mpango wa matumizi bora ya ardhi' itakua na mantiki tofauti kabisa kwa sisi wa Mbagala ukitulinganisha na wale wenzetu wa ADA Estate Dar es Salaam, nasema japo wazo au ujumbe ni ule ule hapo juu ila utekelezaji wake ni mpaka ujue kwanda undani wa mtoa ujumbe kama anatokea penye ardhi yenye rutuba Sumbawanga au Tukuyu au mtu huyo anatokea Same au Tundra kabisa.

Sasa kurudi kwenu wenzangu Wakuu TIQO, Pasco, Geza Ulole na a high calibre Educationist, Dr Kitila Mkumbo, ni kwa misingi ya arguements zangu hapo juu ndio maana wengu humu kamwe hatuwezi hata siku moja kuhiari kusamehe kutazama picha ya ndugu yetu 'Zitto and The Transitions from a dependable social justice fighter hadi kuwa mtu asiyeaminika kwa jamii, ndipo kutazama kwetu wazo lake na pengine jinsi gani historia hiyo nyuma yake ilivyochangia kushawishi mtazamo wako katika kuumba ujumbe husika.

Hadi hapo wakuu naomba sana huu wimbo mtamu wa kumtenganisha wazo na mtoa wazo ueleweke kuwa si jambo ambalo ni sahihi na yenye kipimo sawa kwa mazingira yote hivyo hatuna budi kufikiria kabla hatujajikuta tu kwere chorus bila hata kujiuliza kwamba hicho tunachokiimbi ndicho hasa kina mantiki gani hiyo.

Nakaribisha wenye mawazo tofauti na ya kwangu waweke hoja zao mezani kwa nini Zitto asihukumiwe na tabia yake ya kutokua a consistent, champion-for-public-good, team-player and a transparent leader himself


Tatizo la mitanzania mingi inaacha kujadili hoja inajikita kumjadili mtu na wakenya wanazidi kutuacha kimaendeleo
 
There is nothing wrong for someone to have his own views different from other people but one has to be consistent in his views on similar issues!! Tukumbuke kuwa zitto was in the forefront kutaka mikataba ya madini iwe reviewed and he was rewarded by Kikwete when he was included in the Bomani committee which recommended the changes in those mining contracts; now when Prof. Muhongo advocates the review of the gas and oil exploration contracts the same Zitto comes out crying that it was not in the best interests of our country to review those gas and oil contracts!!! Zitto's stance on this issue smacks of hypocrisy and incosistency in his arguements!!

U have a point mkuu,nashangaa wa2 wanang'ang'ana eti anachukiwa ndani ya chama,jamani tuckurupuke
 
Mr.Muhongo apparently seems to be serving two masters, one is the society of poor tanzanians who seems not to have been benefiting from the abundant natural resources available in the soil of their country, the other is the so called the "special ones" these are the hypocrite politician leaders who pretend to be serving the tanzanians while in reality are collecting wealthy for their families and careless for the big tanzanian population which is in extreme poverty.

Mr. Muhongo obviously appears to be in jeopardy, because according to the rotten governing system of tanzania under ccm it is not that easy to please both masters. In Tanzania, you can not work to please the poor and in the meantime please the greedy politicians, you will must crash, and to me it won't take time before Mr. Muhongo crashes. We have witnessed a lot of bogus mineral contracts signed by the ccm politicians who are in power, their excuse has been very annoying and awkward " because we are new to this mineral sector". this is for sure a foolish reason to be given to the public by people whom we trusted to be our readers, if they were not ready to handle this mineral sector, what made them step into it???? however the answer is as clear as day light, their intention is to benefit themselves leaving the large tanzanian population in poverty. unfortunately, knowingly or unknowingly, Mr. Muhongo now seems to serve the "special ones". this has made him start refusing even what he spoke loudly before cameras and microphones. this justifies openly that the PROFESSOR is already in pockets of politicians. on the other hand, people seem not to understand Mr. Zitto, because people are used to noisy politics instead of logical politics. it is now time for tanzanians to turn to logical politics and not noisy politics.
 
Point yako kubwa sana.

Hivi mwerevu akimuona kilaza anapayuka ana haja gani ya kumjali?

Na akimjali nani wa kuchunguzwa zaidi??

think Judy Think

asante kwa kunitambua hadi kujua nakopendelea kuwa, wee ni nani?

mie ndio wa kishua...aka kiboko yenu
 
Back
Top Bottom