which is the best university in tz?

akrb

Senior Member
Mar 6, 2012
106
10
hi there! which is the best university in tanzania and the best course ,nimemaliza form 6 na nilikuwa nasoma combination ya eca.please members help me ...
 
Ukiuliza kipi ni chuo kikali zaidi bongo,utapata jibu la uhakika. Kwa sababu kila mtu atasifia chuo anachosoma au alichosoma. Au chuo chochote ambacho ana maslahi nacho. Alafu ukiuliza ipi ni course nzuri ya kusoma,hapo inategemea moyo wako unapenda nini na unahitaji nini. Ila inaonekana wewe unapenda masomo ya biashara kutokana na Combination yako ya A-level. Hivyo tafuta vyuo ambavyo vinatoa course hiyo kisha chagua utakachoona kinafaa.
 
Kama unataka kupata degree iliyoiva bac udsm na sua ndo best universities..ila kama unataka cheti tu nenda huko kwingne.over
 
UDSM, it is a university with international reputation and good ranking in East africa. cut off point yao iko juu,so inabidi uwe umefaulu vizuri.
 
kwa aliyesoma masomo ya ECA the best university in SAUT, maana walianza kufundisha mambo hayo tangia zamani wakiwa NTC, nenda hata Bodi ya Uhasibu watakueleza akina nani wanafaulu mitihani ya bodi yao baada ya kumaliza university. Kama ukikosa SAUT nenda Mzumbe ndo wa pili katika utaalamu huo wa uhasibu. SUA, UDSM, UDOM etc wote katika hilo si wa kwanza. Kama wataka kubadili fani na kuingia uhandisi wa aina yoyote, basi UDSM, Kilimo jaribu SUA ila nahisi ni wazuri kwa 'nutrition' zaidi kuliko mifugo na kilimo kwa ujumla. Vinginevyo kujiunga na vyuo waweza kuomba pia ushauri TCU.
 
Kama suala ni kuangalia ufaulu wa mitihani ya BOARD ya uhasibu,basi hahitaji hata kwenda university. Hata vyuo visivyo ktk hadhi ya university watu wanafanya review na kusit board exams na wanafaulu. Academics siyo mitihani ya board ya uhasibu tu. Package ya chuo kikuu ina mengi zaidi ya hayo mkuu. My take, mwache aende akasome Chuo kikuu siyo kukariri mitihani ya board ya Uhasibu!!!
 
Ni swali zuri sana.

Je, wewe unapenda kusomea mambo gani? Huu ni msingi wako. Sasa fuata ushauri hapo chini.

Nakushauri kwakuwa upo njema na mtandao; tafuta miongozo ya vyuo mbalimbali angalia kozi unazozipenda na lete hapa kozi nne unazozipenda tutakushauri uzuri na ubaya wake, pia nafasi ya wewe kupata udahili kulingana na pointi zako. Na baada ya kumaliza masomo yako utakuwa na nafasi gani ya kupata ajira au kujiajiri au kujiendeleza.
 
Kulingana na ranking za Tanzania udsm ndo the best universirty,ila kulingana na combination yako ya ECA naona unapendelea masomo ya biashara,kwa hivyo nakushauri ukasome Mzumbe BAF,sema uwe na uhakika wa kupata div 1 point 3 had 6,kwa hilo halina ubishi ktk uhasibu mzumbe is the best university na ndiyo maana katika mitihani ya ACCA chuo klichopunguziwa mitihani ni Mzumbe tu.,
 
Kulingana na ranking za Tanzania udsm ndo the best universirty,ila kulingana na combination yako ya ECA naona unapendelea masomo ya biashara,kwa hivyo nakushauri ukasome Mzumbe BAF,sema uwe na uhakika wa kupata div 1 point 3 had 6,kwa hilo halina ubishi ktk uhasibu mzumbe is the best university na ndiyo maana katika mitihani ya ACCA chuo klichopunguziwa mitihani ni Mzumbe tu.,au nenda UDSM au UDOM ingawaje wengi wanakidharau bt lecturer wengi wa pale hasa department ya accounting,business administration ni graduates wa Mzumbe na Udsm
 
Best katika nini mkuu? Majengo? Kufundishi? Migomo? Kama kufundisha hata vyuo vya mitaani vipo wanaweza wakakufundisha na ukawa mzuri. Kama Majengo mazuri nenda UDOM.

ILA KAMA UNATAKA KUSOMA UNIVERSITY NENDA UDSM.
 
Ni swali zuri sana.

Je, wewe unapenda kusomea mambo gani? Huu ni msingi wako. Sasa fuata ushauri hapo chini.

Nakushauri kwakuwa upo njema na mtandao; tafuta miongozo ya vyuo mbalimbali angalia kozi unazozipenda na lete hapa kozi nne unazozipenda tutakushauri uzuri na ubaya wake, pia nafasi ya wewe kupata udahili kulingana na pointi zako. Na baada ya kumaliza masomo yako utakuwa na nafasi gani ya kupata ajira au kujiajiri au kujiendeleza.

ok inshallah ntajaribu kufata hizo course
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom